Makosa hatari yanayomgharimu Tundu Lissu!

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,250
2,000
Niliwahi kumpigia chapuo Ndugu Tundu lisu kuwa ni mmoja wa wanasiasa waliotakiwa kushika Uongozi waTaifa hili mwaka 2015 kama kijana na kama mtu mwenye msimamo ulio thabiti..sikukosea bali yeye mwenyewe ameshindwa kujitambua na kujipanga na hatimaye kuipoteza sifa hiyo adimu kwa sababu zifuatazo na ambazo zitaendelea kujitanabaisha kadri muda unavyojiri.

1-Tundu lissu hajawahi kumkubali Mwalimu Nyerere...na mbaya zaidi amewahi kumtusi hayati mwalimu Nyerere.

2-Tundu lissu haamini katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar na huu ni uvunjifu mkubwa wa katiba.

3-Tundu lissu alikosea sana kukubali kuwa mmoja wa wanachadema waliompokea mtuhumiwa mkuu wa ufisadi lowassa na hatimaye kugeuka kuwa mtetezi wake...leo hii lowassa hii lowassa amempinga kuhusu swala la hatua za Rais dhidi ya makanikia.

4-Tundu lissu amekosea tena kutokana na hulka yake ya jazba na arrogance kwa kukinzana na swala la kitaifa la juhudi za Magufuli katika kuliondoa Taifa kutoka mikono ya wizi wa mabepari.

5-Tundu lissu ameshindwa kuwa na msimamo thabiti na wa kiadilifu dhidi ya viongozi wa chama chake mfano Mbowe ambao ametuhumiwa kwenye ukwepaji kodi,madawa ya kulevya na uzinzi.

Kwa hayo machache nasikitika kumuona Tundu lissu akipoteza talanta na fursa adhimu ya kuwa Rais wa nchi hii.

Pengine Tundu lissu angekuwa ndani ya CCM ingewezekana kufichwa kama hazina ili asiingie kwenye makosa ya kijinga ambayo yamemgharimu.

Iam sorry my broda TL but these are bitter medicines and we all have to swallow!

Niliwahi kuandika juu ya Tundu lissu....mwaka 2015 kabla ya gia za angani....Tofauti yangu mimi na yeye kwa sasa imekuja kwenye msimamo aliouchukua dhidi ya fisadi mkuu kwani naamini ndicho kilichombadilisha Tundu Lissu na ambacho kimembadilisha forever and ever!

Again sikukosea kutokana na muda niliokuwa nikiandika thread ile lakini pia kutokana na aina ya wagombea waliokuwa wakipigiwa upatu ndani ya CCM(Ukimuondoa Magufuli) na ndani ya Ukawa Original.

Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
112,076
2,000
Kama Lissu hana sifa ya kuingia Ikulu iweje CCM wamuogope kiasi hiki!? Waruhusu katiba mpya ya rasimu ya Warioba kisha kuwe na Tume ya uchaguzi waone vile Watanzania watakavyofanya kweli kukipiga chini chama cha wahuni na mafisadi.

marcus rojo

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
1,496
2,000
Mrema hana uwezo wa Lissu, hivyo ni makosa kabisa kumfananisha Mzee wa Kiraracha na hazina ya Taifa.
Yani jamaa anamfananisha mzee wa kiraracha na Tundu Antipas Lissu, hahahahaha uwezo wa Lissu ni mara mia ya babu Mrema hata yeye anajua ukichanganya na senile dementia aliyonayo basi hakuna kitu tena! Tuache mlinganisha lissu na takataka za lumumba.
 
The Businessman

JF-Expert Member
Jan 9, 2014
7,412
2,000
Kasome kwanza historia ya Tundu Lisu ili umweelewe vizuri na hutapata shida.

Tundu Lisu ndio MTU pekee aliyebaki wa kuweza kumkosoa Magufuli hadhalani.

Lakini Wasomi wengine na Wanaharakati wameamua kugugumia kimyakimya huku wakishuhudia uvunjwaji wa wazi wa Katiba.

Acheni ujinga wa kutaka kuungwa mkono kilazima kwa makosa mliyoyafanya wenyewe.

Kwangu Mimi Tundu Lisu bado atabakia kuwa MTU wangu Bora kabisa wa Kizazi hiki. Lengo lenu mnataka Tundu Lisu asalimu amri, na akisalimu amri basi adhma yenu ya kutawala kibabe itakuwa imetimia maana mnaona ndio MTU anayewasumbua ndio maana hamuishi kumtajataja.
 
ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,803
2,000
Niliwahi kumpigia chapuo Ndugu Tundu lisu kuwa ni mmoja wa wanasiasa waliotakiwa kushika Uongozi waTaifa hili mwaka 2015 kama kijana na kama mtu mwenye msimamo ulio thabiti..sikukosea bali yeye mwenyewe ameshindwa kujitambua na kujipanga na hatimaye kuipoteza sifa hiyo adimu kwa sababu zifuatazo na ambazo zitaendelea kujitanabaisha kadri muda unavyojiri.

1-Tundu lissu hajawahi kumkubali Mwalimu Nyerere...na mbaya zaidi amewahi kumtusi hayati mwalimu Nyerere.

2-Tundu lissu haamini katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar na huu ni uvunjifu mkubwa wa katiba.

3-Tundu lissu alikosea sana kukubali kuwa mmoja wa wanachadema waliompokea mtuhumiwa mkuu wa ufisadi lowassa na hatimaye kugeuka kuwa mtetezi wake...leo hii lowassa hii lowassa amempinga kuhusu swala la hatua za Rais dhidi ya makanikia.

4-Tundu lissu amekosea tena kutokana na hulka yake ya jazba na arrogance kwa kukinzana na swala la kitaifa la juhudi za Magufuli katika kuliondoa Taifa kutoka mikono ya wizi wa mabepari.

5-Tundu lissu ameshindwa kuwa na msimamo thabiti na wa kiadilifu dhidi ya viongozi wa chama chake mfano Mbowe ambao ametuhumiwa kwenye ukwepaji kodi,madawa ya kulevya na uzinzi.

Kwa hayo machache nasikitika kumuona Tundu lissu akipoteza talanta na fursa adhimu ya kuwa Rais wa nchi hii.

Pengine Tundu lissu angekuwa ndani ya CCM ingewezekana kufichwa kama hazina ili asiingie kwenye makosa ya kijinga ambayo yamemgharimu.

Iam sorry my broda TL but these are bitter medicines and we all have to swallow!

Niliwahi kuandika juu ya Tundu lissu....mwaka 2015 kabla ya gia za angani....Tofauti yangu mimi na yeye kwa sasa imekuja kwenye msimamo aliouchukua dhidi ya fisadi mkuu kwani naamini ndicho kilichombadilisha Tundu Lissu na ambacho kimembadilisha forever and ever!

Again sikukosea kutokana na muda niliokuwa nikiandika thread ile lakini pia kutokana na aina ya wagombea waliokuwa wakipigiwa upatu ndani ya CCM(Ukimuondoa Magufuli) na ndani ya Ukawa Original.

Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)
hiyo namba 3 ujue Lowasa hakuwa fisadi bali ccm wabaya walitengeneza propaganda za kumchafua wakawapelekea wapinzani wakaamini lakini Lowasa alipohamia chadema alianika Ukweli wote na kusema kuwa mmiliki wa Richmond ni Kikwete, usiendelee kukariri ya zamani angalia ya sasa,
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
112,076
2,000
We acha tu Mkuu lol! Eti Mzee wa kiraracha ni wa kufanananishwa na hazina ya Taifa!

Yani jamaa anamfananisha mzee wa kiraracha na Tundu Antipas Lissu, hahahahaha uwezo wa Lissu ni mara mia ya babu Mrema hata yeye anajua ukichanganya na senile dementia aliyonayo basi hakuna kitu tena! Tuache mlinganisha lissu na takataka za lumumba.
 
ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,803
2,000
Kasome kwanza historia ya Tundu Lisu ili umweelewe vizuri na hutapata shida.

Tundu Lisu ndio MTU pekee aliyebaki wa kuweza kumkosoa Magufuli hadhalani.

Lakini Wasomi wengine na Wanaharakati wameamua kugugumia kimyakimya huku wakishuhudia uvunjwaji wa wazi wa Katiba.

Acheni ujinga wa kutaka kuungwa mkono kilazima kwa makosa mliyoyafanya wenyewe.

Kwangu Mimi Tundu Lisu bado atabakia kuwa MTU wangu Bora kabisa wa Kizazi hiki. Lengo lenu mnataka Tundu Lisu asalimu amri, na akisalimu amri basi adhma yenu ya kutawala kibabe itakuwa imetimia maana mnaona ndio MTU anayewasumbua ndio maana hamuishi kumtajataja.
naunga mkono hoja kwa 100% hata JK aliwahi kusema ni mara 100 Slaa awe Rais kuliko Lisu kuwa mbunge huko ccm wakimsikia Lisu hubanwa na tumbo la kuendesha.
 
ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,803
2,000
Umesahau pia kuwa TL amekuwa msaliti kwa kuiweka nchi rehani ya kisiasa kulazimisha kupewa taarifa za kuikandamiza nchi yake dhidi ya mabepari
Hizo ni propaganda ni uongo mkubwa umepikwa ili kuwahadaa watanzania, tokea 1998 anapambana kulalamikia mikataba ya madini alikuwa msariti? Acheni hizo watanzania wa sasa wapo makini sana hata mje na uzushi gani juu ya Lisu mtaonekana wajinga tu.
 
2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,031
2,000
Niliwahi kumpigia chapuo Ndugu Tundu lisu kuwa ni mmoja wa wanasiasa waliotakiwa kushika Uongozi waTaifa hili mwaka 2015 kama kijana na kama mtu mwenye msimamo ulio thabiti..sikukosea bali yeye mwenyewe ameshindwa kujitambua na kujipanga na hatimaye kuipoteza sifa hiyo adimu kwa sababu zifuatazo na ambazo zitaendelea kujitanabaisha kadri muda unavyojiri.

1-Tundu lissu hajawahi kumkubali Mwalimu Nyerere...na mbaya zaidi amewahi kumtusi hayati mwalimu Nyerere.

2-Tundu lissu haamini katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar na huu ni uvunjifu mkubwa wa katiba.

3-Tundu lissu alikosea sana kukubali kuwa mmoja wa wanachadema waliompokea mtuhumiwa mkuu wa ufisadi lowassa na hatimaye kugeuka kuwa mtetezi wake...leo hii lowassa hii lowassa amempinga kuhusu swala la hatua za Rais dhidi ya makanikia.

4-Tundu lissu amekosea tena kutokana na hulka yake ya jazba na arrogance kwa kukinzana na swala la kitaifa la juhudi za Magufuli katika kuliondoa Taifa kutoka mikono ya wizi wa mabepari.

5-Tundu lissu ameshindwa kuwa na msimamo thabiti na wa kiadilifu dhidi ya viongozi wa chama chake mfano Mbowe ambao ametuhumiwa kwenye ukwepaji kodi,madawa ya kulevya na uzinzi.

Kwa hayo machache nasikitika kumuona Tundu lissu akipoteza talanta na fursa adhimu ya kuwa Rais wa nchi hii.

Pengine Tundu lissu angekuwa ndani ya CCM ingewezekana kufichwa kama hazina ili asiingie kwenye makosa ya kijinga ambayo yamemgharimu.

Iam sorry my broda TL but these are bitter medicines and we all have to swallow!

Niliwahi kuandika juu ya Tundu lissu....mwaka 2015 kabla ya gia za angani....Tofauti yangu mimi na yeye kwa sasa imekuja kwenye msimamo aliouchukua dhidi ya fisadi mkuu kwani naamini ndicho kilichombadilisha Tundu Lissu na ambacho kimembadilisha forever and ever!

Again sikukosea kutokana na muda niliokuwa nikiandika thread ile lakini pia kutokana na aina ya wagombea waliokuwa wakipigiwa upatu ndani ya CCM(Ukimuondoa Magufuli) na ndani ya Ukawa Original.

Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)
We jamaa inabidi ukapimwe akili!
Mbona unaandika kama mtu fulani mwenye power ya kuamua nani atakuwa nani kwenye Nchi hii! Ipo kama vile wewe ukishasema ndio final, you can decide for the state.... Or you have power of attorney to decide nani awe president wa nchi hii
 
ZILLAHENDER MPEMA

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
2,058
2,000
Hilo unaloliita "fisadi kuu"ni lipi hilo?Kwa nini fisadi hilo msilitupe korokoroni katika ile mahakama yenu ya mafisadi iliyogeuzwa makazi ya popo mbwa,vimbulu na mapaka shume?

Bahati mbaya kwako unajaribu kuihadaa nafsi yako mwenyewe!Hivi kiongozi wa chini anawezaje kuwa " fisadi kuu"kwenye uchafu uliojadiliwa na kupitishwa na Cabinet iliyo chini ya uenyekiti wa Rais wa nchi?Kwa nini "fisadi kuu" asiwe yule mwenye maamuzi ya Mwisho juu ya mambo yote yahusuyo nchi na ambaye ndiye aliyesimamia maamuzi yote ya kipumbavu yanayoligharimu Taifa letu hadi leo?

Nafikiri "fisadi kuu"ni lile lililojianzishia ACACIA yake na kujimilikisha mgodi wa kiwira kinyume na sheria za nchi,kupitia fisadi hilo ndimo kulimozaliwa uchafu wote ambao wagonga meza wa wakati huo na ambao pia walikuwa sehemu ya Cabinet,leo wanatulazimisha tuwaone wazalendo kwa kutuhadaa kuwa wanapambana na wahujumu uchumi wakati mikono yao ilishiriki 100% katika kuwapokea majambazi wa kiuchumi wanaopora Rasilimali zetu.

Eti leo mtu anakurupuka kwa mwendokasi wa ukilaza wa " permanent head disorder" ya mazao ya korosho na kutuuliza nani aliyeturoga huku akijuwa fika tumerogwa na ccm na serikali yake na yeye alishiriki kuitikia "tawile" katika vikao vya kishirikina vya kuiroga nchi yetu kiuchumi,kutuuliza tumerogwa na nani wakati wewe ni sehemu ya wachawi wenyewe yaweza kuwa ni kejeli ya kiwango cha lami!

Eti kuna watu wanashangilia na kusifia kuwa ........,hivi hamjuwi kuwa hao mnaowavika ushujaa leo mikono yao imejaa damu za hatia kwa kuunyonga utajiri wetu kupitia chama na serikali ileile ya ccm?Wapumbavu wanawageukia kina TL na kuwasakama utadhani TL ndiye aliyelifikisha Taifa hapa lilipo,ajabu zaidi tukihoji na kuomba katiba ibadilishwe ili ituruhusu kuwapiga mawe hadi kufa viongozi wakuu wawili walioshiriki,kusimamia na kubariki Wizi huu,anatokea kiongozi mwingine ambaye pia alikuwa mgonga meza na mwana cabinet anafura na kuliagiza bunge liwafurushe wote watakaohoji uadilifu wa viongozi wastaafu na yeye atahitimisha kwa kuwadhibiti ndani ya dk5 pale watakapojaribu kupaza sauti zao nje ya bunge.

Mwenye akili timamu hawezi kuchukuliwa na hadaa hii ya kiwango cha lami,atahoji na kudadisi ujasiri huu wa kilaghai umetoka wapi na utatufikisha wapi ikiwa anayeusimamia ujasiri huo ameshajiapiza kutofukua makaburi?

Nitakuwa wa Mwisho kuimba na kusali sala za "litania ya watakatifu" ili kumtukuza mtakatifu wa ccm aliyeshiriki kulihujumu Taifa,lakini leo anajifanya yeye ni "malaika wa nuru" aliyeletwa kuja kulitoa Taifa letu gizani.Mimi si sehemu ya wanafiki na sidanganyiki kipumbavupumbavu.
 
nyamalagala

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
743
1,000
Mnatembelea steps za T. L kila kukicha
Halafu wajidai kuwa wazalendo.Magufuli ajifunze kushukuru vijana jasiri kama TL aliyepuliza kipyenga tangu 1998 kuhusu utaratibu mbovu wa mikataba ya madini. Pia kijana mwingine anayepaswa kushukuriwa ni ZZK kwa kushikilia kidete hoja ya uwazi katika mikataba ya nadini.baada ya kumshukuru hapo hapo wamuombe msamaha kwa kumfukuza bungeni 2007 wakati akikaza nati za hoja Yake juu ya mikataba ya madini.Poor JMP na wenzake wa Chama Cha Makanikia (CCM) waliokalili kuwa kila wasemacho wapinzani hakina msingi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom