Makosa hatari yanayomgharimu Tundu Lissu!

Makosa hatari yanayomgharimu Tundu Lissu!

Kwa hiyo Mbowe hakosolewi kwa kuwa kafanya mengi mazuri?
Unaachaje kumkosoa Mbowe iwapo ana mfululizo wa tuhuma ambazo wanachadema wamekuwa wakizishikia bango?

Ukwepaji kodi...Uzinzi...Ufisadi n.k
Kukwepa kodi na ufisadi ni makosa la jinai. Kama unafahamu, mkosoe kisha mshitaki. Kama serikali haijamuona Mbowe kuwa mkwepa kodi na fisadi, unatarajia Lissu awe na kipaji maalum cha utambuzi wa makosa hayo? Uzinzi ni suala la maadili binafsi linalomhusu yeye na familia yake; si kosa la jinai na halituathiri kama taifa. Kama wewe ni kiongozi wake wa dini kaongee naye umuweke sawa. Tukitaka kuulizana habari za uzinzi sijui tutakapoishia. Kwa kifupi, hayo yote uliyotaja si mambo ya kumshughulisha Lissu. Ufisadi katika madini, umeme, ujenzi, n.k. ndiyo masuala yanayotuathiri sana.
 
Kama Lissu hana sifa ya kuingia Ikulu iweje CCM wamuogope kiasi hiki!? Waruhusu katiba mpya ya rasimu ya Warioba kisha kuwe na Tume ya uchaguzi waone vile Watanzania watakavyofanya kweli kukipiga chini chama cha wahuni na mafisadi.


Wahofia ujinga wake na ukichaa wake mkuu. Si kama wanamuogopa
 
Kwa hiyo kwenye Katiba mpya ndio tutaandika kuwa Acacia waache udanganyifu?

Msilete majibu too general to answer specific issue...

Katiba ya sasa inaruhusu wizi,udanganyifu na ukwepaji kodi?
yes katiba mpya pamoja na tume huru ya uchaguzi ndio italeta majibu maana CCM watafanya kazi kwa waledi sasa hivi hata wakifanya utumbo libuva2 atawatangaza kama wameshinda tu ndio hawajali wameuza nchi kwa wazungu ile wapate sapoti yao ili wajuwe bila ya ccm hakuna madini ya bure
 
Dah Andiko hili linasikitisha sana
Nionavyo mimi liko shallow sana
Tuanze na sababu yako namba
1.Tundu lissu hajawahi kumkubali Mwalimu Nyerere...na mbaya zaidi amewahi kumtusi hayati mwalimu Nyerere.
Hivi ni lazima kumkubali Mwalimu? unaamini kila unachokusoma kuhusu mwalimu ndicho kweli kilichofanyika
Hiki ni kizazi cha kuhoji na siamini kama kuhoji baadhi ya maamuzi ya kipindi cha mwalimu ni kutokumkubali mwalimu
Binafsi ninapata shida juu ya maamuzi fulanifulani lakini haimaanishi simkubali Mwalimu
TAL hakuwahi kusema hamkubali mwalimu,na amekua akirejea matamshi ya mwalimu mara kadhaa hii yote inaonesha anamuheshimu.
2.Kutokuamini juu ya muungano hayo ni binafsi ila kuuvunja hapo tunaweza kusema ndio ukiukwaji wa katiba
3.EL sio kiongozi wa serikali,maswala yake na kupokelewa na chama chake sidhani kama ni ya muhimu sana wapo wengi tu upande wa pili ambao wako kwenye tuhuma mbali mbali na bado ni viongozi wakubwa nchini.
4.Binafsi naunga mkono Juhudi za Mh Rais lakini siamini kwamba wote tunatakiwa tuseme ndio wale wanaotoa hoja za tofauti wanatusaidia kupanua uelewa wetu juu ya mambo haya. hatuwezi kua na taifa ambalo wote tunasema ndio litakua ni la mazezeta.
5.Hilo la mwenyekiti wa CDM nadhani akipatikana na hatia katika hayo ndio tuhoji.

Katika hotuba yake ya uchochezi Zanzibar Tundu Lissu alisema Karume aliuwawa kwa sababu ya kuhoji muungano. Ina maana aliuliwa na Nyerere.
Sielewi kwanini kauli hiyo hajatakiwa kuifafanua kama si kufungwa jela.

Hiyo kauli ingekuwa imesemwa na mtu wa CCM pasingetosha magazetini.

Yaani Tanzania ya leo wapinzani wana nguvu za shetani. Wanakubalika kirahisi kama ambavyo binadamu hupenda kufanya mabaya kuliko mema.
 
Katika hotuba yake ya uchochezi Zanzibar Tundu Lissu alisema Karume aliuwawa kwa sababu ya kuhoji muungano. Ina maana aliuliwa na Nyerere.
Sielewi kwanini kauli hiyo hajatakiwa kuifafanua kama si kufungwa jela.

Hiyo kauli ingekuwa imesemwa na mtu wa CCM pasingetosha magazetini.

Yaani Tanzania ya leo wapinzani wana nguvu za shetani. Wanakubalika kirahisi kama ambavyo binadamu hupenda kufanya mabaya kuliko mema.

..hotuba yake ya Znz ilikuwa inajibu hotuba nyingine ya kichochezi iliyotolewa kabla ya hapo.

..ccm wana nguvu zaidi.

..kwa mfano sasa hivi wanashirikiana (mazungumzo) na acacia ili wasishtakiwe mahakamani wakati tume imebainisha kuwa acacia wanatuibia.
 
Katika hotuba yake ya uchochezi Zanzibar Tundu Lissu alisema Karume aliuwawa kwa sababu ya kuhoji muungano. Ina maana aliuliwa na Nyerere.
Sielewi kwanini kauli hiyo hajatakiwa kuifafanua kama si kufungwa jela.

Hiyo kauli ingekuwa imesemwa na mtu wa CCM pasingetosha magazetini.

Yaani Tanzania ya leo wapinzani wana nguvu za shetani. Wanakubalika kirahisi kama ambavyo binadamu hupenda kufanya mabaya kuliko mema.
I wish I could be Magufuli!Thanks God kwamba bado ni kijana!
 
Wewe ni nani ?? hata uwe na maamuzi juu ya Tundu kwa niaba yetu. who are you by the way???

Hayo unayoona ni makosa ni kwa mtazamo wako na siyo mtazamo wa kila mtu, na wewe ni mmoja kati ya wa TZ mil 50, sio lazima wala haituhusu kuona kile wewe unaoa kwa interest zako, kila mmoja anajicho lake kwa wakati na nafasi yake kuona mambo
Usitusemee
 
Niliwahi kumpigia chapuo Ndugu Tundu lisu kuwa ni mmoja wa wanasiasa waliotakiwa kushika Uongozi waTaifa hili mwaka 2015 kama kijana na kama mtu mwenye msimamo ulio thabiti..sikukosea bali yeye mwenyewe ameshindwa kujitambua na kujipanga na hatimaye kuipoteza sifa hiyo adimu kwa sababu zifuatazo na ambazo zitaendelea kujitanabaisha kadri muda unavyojiri.

1-Tundu lissu hajawahi kumkubali Mwalimu Nyerere...na mbaya zaidi amewahi kumtusi hayati mwalimu Nyerere.

2-Tundu lissu haamini katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar na huu ni uvunjifu mkubwa wa katiba.

3-Tundu lissu alikosea sana kukubali kuwa mmoja wa wanachadema waliompokea mtuhumiwa mkuu wa ufisadi lowassa na hatimaye kugeuka kuwa mtetezi wake...leo hii lowassa hii lowassa amempinga kuhusu swala la hatua za Rais dhidi ya makanikia.

4-Tundu lissu amekosea tena kutokana na hulka yake ya jazba na arrogance kwa kukinzana na swala la kitaifa la juhudi za Magufuli katika kuliondoa Taifa kutoka mikono ya wizi wa mabepari.

5-Tundu lissu ameshindwa kuwa na msimamo thabiti na wa kiadilifu dhidi ya viongozi wa chama chake mfano Mbowe ambao ametuhumiwa kwenye ukwepaji kodi,madawa ya kulevya na uzinzi.

Kwa hayo machache nasikitika kumuona Tundu lissu akipoteza talanta na fursa adhimu ya kuwa Rais wa nchi hii.

Pengine Tundu lissu angekuwa ndani ya CCM ingewezekana kufichwa kama hazina ili asiingie kwenye makosa ya kijinga ambayo yamemgharimu.

Iam sorry my broda TL but these are bitter medicines and we all have to swallow!


Niliwahi kuandika juu ya Tundu lissu....mwaka 2015 kabla ya gia za angani....Tofauti yangu mimi na yeye kwa sasa imekuja kwenye msimamo aliouchukua dhidi ya fisadi mkuu kwani naamini ndicho kilichombadilisha Tundu Lissu na ambacho kimembadilisha forever and ever!

Again sikukosea kutokana na muda niliokuwa nikiandika thread ile lakini pia kutokana na aina ya wagombea waliokuwa wakipigiwa upatu ndani ya CCM(Ukimuondoa Magufuli) na ndani ya Ukawa Original.

Ni Tundu Lissu pekee(Sababu moja sifa kumi)
Bahati mbaya ulimpigia upatu kwa kutomuelewa.tangu wakati ule alikuwa hafai
 
hiyo namba 3 ujue Lowasa hakuwa fisadi bali ccm wabaya walitengeneza propaganda za kumchafua wakawapelekea wapinzani wakaamini lakini Lowasa alipohamia chadema alianika Ukweli wote na kusema kuwa mmiliki wa Richmond ni Kikwete, usiendelee kukariri ya zamani angalia ya sasa,
Alianikia chumbani mbona mpaka leo hatujasikia hoja za lowasa ama wewe ni nyumbu kwelikweli
 
TL ktk kizazi hiki namuona kma mandera, maana amekuwa muwazi sana, sema watz wengi tumekuwa bendera fata upepo, ni wangap wanaothubutu kumukosoa rais bila kuvunja sheria za nchi?
 
TL ktk kizazi hiki namuona kma mandera, maana amekuwa muwazi sana, sema watz wengi tumekuwa bendera fata upepo, ni wangap wanaothubutu kumukosoa rais bila kuvunja sheria za nchi?

Keshavunja sana sheria za nchi na alitakiwa awe jela siku nyingi. Hiyo serikali inasita tu kwa kuogopa itaonekana inafunga wapinzani.
Halafu acha ujinga. Unamfananisha Lissu na Mandela. Unajua alichokuwa akipigania Mandela?
 
El sio kiongozi wa serilali lakini aliwahi kuwa kiongozi wa serikali.EL alituhumiwa sana na Chadema kuwa ni fisadi na ilikuwa ni hoja iliyoikuza Chadema.kumkubali fisadi kwa gia za anga ni kosa kubwa sana...na kuendelea kumtetea ndi kosa zaidi.

Mwenyekiti Mbowe anapotuhumiwa ni lazima ahojiwe au kuulizwa au kuandamwa kama ulivyo utamaduni wa enzi wa Chadema dhidi ya watuhumiwa wa CCM.
Tatizo ni kwamba anatuhumiwa na ccm na sio wanachama wake sasa obvious hizo zinaonekana tu ni hila za kisiasa
 
Yani jamaa anamfananisha mzee wa kiraracha na Tundu Antipas Lissu, hahahahaha uwezo wa Lissu ni mara mia ya babu Mrema hata yeye anajua ukichanganya na senile dementia aliyonayo basi hakuna kitu tena! Tuache mlinganisha lissu na takataka za lumumba.
NI KWELI.UWEZO WA LISSU NI MALA MIA KW MREMA.LKN UZALENDO JEE.NANI YUPO JUU??!! MREMA NI MZALENDO ZAIDI KULIKO TUNDU LISSU.
Shida ya hili li Lissu ni kutaka sifa ya kufikia kuwapiku hata viongozi wake wa chadema, anataka aonekane anajua kila kitu na wenzake ni maamuma tu.
 
NI KWELI.UWEZO WA LISSU NI MALA MIA KW MREMA.LKN UZALENDO JEE.NANI YUPO JUU??!! MREMA NI MZALENDO ZAIDI KULIKO TUNDU LISSU.
Labda definition yako ya uzalendo ni ya tofauti
Sijaona Mzalendo TZ kama Tundu Lisu
Nikikumbuka harakati zake za kupigania haki za wanaoishi maeneo ya migodini
Harakati zake za kupinga Mikataba ya kupitishwa kwa hati za dharura
Harakati zake za kupigania Bunge lisimame kama mkosoaji na mshauri wa serikali na sio mshangiliaji.
Tundu Lisu ni mzalendo wa kweli.
 
Halafu wajidai kuwa wazalendo.Magufuli ajifunze kushukuru vijana jasiri kama TL aliyepuliza kipyenga tangu 1998 kuhusu utaratibu mbovu wa mikataba ya madini. Pia kijana mwingine anayepaswa kushukuriwa ni ZZK kwa kushikilia kidete hoja ya uwazi katika mikataba ya nadini.baada ya kumshukuru hapo hapo wamuombe msamaha kwa kumfukuza bungeni 2007 wakati akikaza nati za hoja Yake juu ya mikataba ya madini.Poor JMP na wenzake wa Chama Cha Makanikia (CCM) waliokalili kuwa kila wasemacho wapinzani hakina msingi.
Imewachukua wana ccm takriban miaka 20 kumwelewa Lissu!!!!!!!!!!!!!….... definitely they are slow Learners, alafu ndo wanashika u incharge wa taifa!!!!...... twafwaaaaa.
 
Back
Top Bottom