Kwanza lazima ujue historia ilikuaje kuhusu uyo shetwani. Kabla ya kuumbwa mwanadamu walikuwa hao Malaika na Majini kama viumbe vyake Mungu alivoviumba. Mungu Akawaambia malaika kuwa anataka kuumba kiumbe kilicho bora ili akiweke duniani, malaika wakamuuliza kwanini aumbe kiumbe chengine mwisho wa siku waje waichafue dunia si angewaachia wao wakaishi tu, kwa sababu wanamuabudu Mungu kila wakati na hawajawahi kumuudhi? Mungu akawaambia mtajua kwanini. Kumbuka wakati huo majini na malaika wote walikuwa wanamuabudu mungu. Hakukuwa na kiumbe shetani. Baada ya kuumbwa binaadamu, ambae ni Adam, Mungu akamfundisha Adam, kisha akawaita malaika na viumbe vyote, akawaonesha kalamu (kama ntakuwa sijakosea) akawauliza viumbe vyote hii nini? wakajibu hawajui, alipoulizwa Adam akawaambia jibu. Mungu akawaambia viumbe vyake hivo wamsujudie Adam (jua kuwa kusujudia huku sio kule kuweka komo kwenye ardhi, ni kama vile ku bow, unavomuamkia mzee wako), wote wakasujudu isipokuwa Iblis, iblis akagoma, na akasema yeye hawezi kumsujudia kiumbe alichoumbwa kwa udongo wakati yeye kaumbwa kwa moto. Hapo ndipo alipoasi na kulaaniwa. Iblis huyu akamuahidi Mungu kuwa atawapotosha viumbe vyake vyote wasimuabudu Mungu, nae Mungu akampa kama challenge, Ibliss aliomba asiadhibiwe na yeye awe wa mwisho kutoka roho, ombi lake likakubaliwa. Sasa Iblis ndio akatoka kuwa jini mwema na kuwa jini muovu ambae muovu ni shetani. Binaadam tumepewa freewill....
Upande wetu wa kiislam tunasema Mungu ana kibri, kibri chake ndio kinatuzuia kumuona yeye, akionekana manake hana kibri, na yeye atakuwa kiumbe tu kama viumbe tunavoviona kila siku, lakini yeye sio kiumbe. Mussa alimwambia anataka kumuona, matokeo yake alipotaka kujionesha wote walizimia na milima kuangamia na hakuna aliemuona. Hajajificha kabisa, macho yetu hayamfikii.
Swali jepesi sana, we ulitoka wapi? ulishushwa mbinguni tu? Aliuwa watu wengi bila huruma? mi naona wala hakuwa na hasira apo alipowaangamiza, kwa sababu adhabu za mungu ukisikia si mchezo. Ndio mafuriko yalikuwa Suluhisho kwa Umma wa wakati, yesu na mitume wengine walikuja kwa ajili Nyumma nyengine, vizazi vya baadae Ibrahim, au Judas msaliti alikuwepo wakati wa Ibrahim?
Sijui story ya upandde wa pili (wakristo), lakini, we jiulize tujaalie waliambiwa wawavamie hao watu, je kama hao watu ndio walikuwa wamevamia ardhi ya watu? anyways Upande wa waislam kama sikosei, waliahidiwa ardhi lakni kwa vile walimuudhi Mungu, basi Mungu nae aliwaacha mkono waendelee kuhangaika.
Have you heard about metaphors? Anyways who has ever sat down and count the numbers of the stars? Who has ever known the population back in the days? DO you know by the time when the earth dissapears how many people would have lived in?
Maradhi hayakuumbwa kumuadhibu mtu, au allergy ya mtu sio adhabu kutoka kwa mungu, that is the beauty of the creator, anaweza kufanya vitu in different ways. Kwani wenye allergy hawali chakula? hawanywi?
Majanga mengine tunajitakia wenyewe na tunayatengezea mazingira yenyewe. Mfano katika quran tunafundishwa kuwa milima ni kama pillars zenye kustabilise dunia, saivi watu wanakwenda wanachimba milima na kukata kata ili kupata dhahabu na mengineyo. Sasa kama pale Jangwani ikinyesha mvua panatokea mafuriko, afu mtu waende kueka kijumba chako, ukifika utamsingizia mungu kakuua au umejiua mwenyewe? Everything that tasted life shall go, hio ndio principle. kwaio natural disasters pia can be a way to clear the land for new beings.
Kama nlivosema hapo juu, umeonja maisha basi ikifika mda lazima urudi kwake. Na maradhi ni majaribio katika maisha, ukiumwa hio ni neema kutoka kwa Mungu, sasa unatizamwa imani yako, watu kama wewe ndio mnakimbilia kwa mganga kuchinja ng'ombe wa manjano. Dunia hakuifanya kuwa sehemu ya kuishi milele.
Naam, jehannamu ni kwa ajili ya waovu, kama ilivo wewe mwanao wa kike akitiwa mimba uko nje ukitambua unatamani usingemzaa. Sasa jehannam wanakwenda wale waliofanya maovu kisha hawakutubia, duniani umepewa mda wa kufanya mema wewe umechagua maovu, basi hustahili kuishi pale wanapokaa watu ambao duniani wamehangaika kufanya mema. Eti we mwenyeo unaona fair kwamba wewe duniani ulikuwa unahangaika sana na maisha, ukisali sana kumuomba mungu, afu kuna rafiki yako duniani alikua na mihela na mimali, akitumbua, hana cha mungu wala nini, akipita njiani alikuwa anakumwagia maji, vipi unaona ni sawa akiwa peponi na wewe? Au tutoe mfano mwengine, we umesota mashuleni na kutafuta mavyeti, unamaliza chuo ajira unakosa lakini mshkaji wako alikuwa hasomi kaekwa bosi wizara ya fedha? Is it FAIR?
Mwili wa binaadamu una kasoro? We umeumba nini kwa kweli chenye uhai?