Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

maajabuya Mungu kumucha shetani duniani na kuwatesa bianadamu kwa takriban miaka zaidi ya elfu mbili.
Maajabu ya Mungu aliumba ulimwengu wote bila kutumia chochote lakini akahitaji ubavu wa mwanaume ili aweze kumuumba mwanamke.
 
Usisome vitu juu juu ukaleta taarifa za uongo humu yote ulioorodhesha hapo juu ukisoma kwa undani utagundua chanzo ni uasi wa mwanadamu dhidi ya Mungu kwaio hayamuhusu Mungu...


Ukiambiwa usishuke moto utaungua then ukashika ukaungua unadhani hapo nani mwenye kosa...ni yeye aliekuonya au wewe ulieshikaa???


Inaezekana Mungu akatumia nguvu kukuzuia lakini Mungu wetu sio dictator maamuz na uchaguzi upo juu ya mwandamu.....


Ila asante kwa darasa lako zuri litafumbua wengi akili...

Karbuni wana JF kwa hoja zaid...........
Kama Mungu siyo dikteta na anatupa uwezo wa kuchagua, basi angetupa uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe, kama tuzaliwe je na wazazi wapi? nchi ipi? na wakati gani.

Pia angetupa uhuru wa kuchagua kutembea au kupaa.
 
Maajabu ya Mungu aliumba ulimwengu wote bila kutumia chochote lakini akahitaji ubavu wa mwanaume ili aweze kumuumba mwanamke.
maajabu ya mungu kuwatuma nyoka kuwauma wana wa israeli jangwani na badae kutengeneza sanamu ya nyoka ili wapone.!! sa ndo nin!!
 
maajabu ya mungu kuwatuma nyoka kuwauma wana wa israeli jangwani na badae kutengeneza sanamu ya nyoka ili wapone.!! sa ndo nin!!
Maajabu ya Mungu aliyeandika kitabu kinacho anza na nyoka anayeongea, halafu bikira aliyepata mimba bila kuwa na mume na mwishowe Dragon mwenye vichwa vinne.
 
Kama Mungu siyo dikteta na anatupa uwezo wa kuchagua, basi angetupa uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe, kama tuzaliwe je na wazazi wapi? nchi ipi? na wakati gani.

Pia angetupa uhuru wa kuchagua kutembea au kupaa.
Kwani Mungu kazui mtu kupaa? ina maana kama mtu ana uwezo wa kupaa hatoweza kufanya hivyo kwa sababu Mungu kazuia?
 
Hana huruma? Nafikiri angekuwa hana huruma wala rehema saa hizi uzi wako usingesomeka, Siku moja atakujibu, ndio utafahamu tofauti ya Mungu na binadamu mdhaifu mwenye uelewa mdogo. Lakini akishakujibu usisahau kuleta mrejesho ili siku nyingine mwingine asilete uzi kama huu.
 
Alikuwa mkristo huyo,mnashindwa hata kundua kwa jinsi wanavyojenga hoja zao?
kujenga hoja si tatizo mkuu, mimi nilifikiri huyu jamaa ni FREEMASON fulani ambae anatafuta wafuasi kwa kuharibu imani za watu kupitia maneno yake ambayo ukiyasoma vizuri utagundua sio kwamba huyu jamaa ana akili bali ana mapungufu makubwa ya kiimani ambayo naamini hata nicomment maneno ya aina gani hatayasadiki.
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.
Kwanza lazima ujue historia ilikuaje kuhusu uyo shetwani. Kabla ya kuumbwa mwanadamu walikuwa hao Malaika na Majini kama viumbe vyake Mungu alivoviumba. Mungu Akawaambia malaika kuwa anataka kuumba kiumbe kilicho bora ili akiweke duniani, malaika wakamuuliza kwanini aumbe kiumbe chengine mwisho wa siku waje waichafue dunia si angewaachia wao wakaishi tu, kwa sababu wanamuabudu Mungu kila wakati na hawajawahi kumuudhi? Mungu akawaambia mtajua kwanini. Kumbuka wakati huo majini na malaika wote walikuwa wanamuabudu mungu. Hakukuwa na kiumbe shetani. Baada ya kuumbwa binaadamu, ambae ni Adam, Mungu akamfundisha Adam, kisha akawaita malaika na viumbe vyote, akawaonesha kalamu (kama ntakuwa sijakosea) akawauliza viumbe vyote hii nini? wakajibu hawajui, alipoulizwa Adam akawaambia jibu. Mungu akawaambia viumbe vyake hivo wamsujudie Adam (jua kuwa kusujudia huku sio kule kuweka komo kwenye ardhi, ni kama vile ku bow, unavomuamkia mzee wako), wote wakasujudu isipokuwa Iblis, iblis akagoma, na akasema yeye hawezi kumsujudia kiumbe alichoumbwa kwa udongo wakati yeye kaumbwa kwa moto. Hapo ndipo alipoasi na kulaaniwa. Iblis huyu akamuahidi Mungu kuwa atawapotosha viumbe vyake vyote wasimuabudu Mungu, nae Mungu akampa kama challenge, Ibliss aliomba asiadhibiwe na yeye awe wa mwisho kutoka roho, ombi lake likakubaliwa. Sasa Iblis ndio akatoka kuwa jini mwema na kuwa jini muovu ambae muovu ni shetani. Binaadam tumepewa freewill....

2.KUISHI MAFICHONI:

Upande wetu wa kiislam tunasema Mungu ana kibri, kibri chake ndio kinatuzuia kumuona yeye, akionekana manake hana kibri, na yeye atakuwa kiumbe tu kama viumbe tunavoviona kila siku, lakini yeye sio kiumbe. Mussa alimwambia anataka kumuona, matokeo yake alipotaka kujionesha wote walizimia na milima kuangamia na hakuna aliemuona. Hajajificha kabisa, macho yetu hayamfikii.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Swali jepesi sana, we ulitoka wapi? ulishushwa mbinguni tu? Aliuwa watu wengi bila huruma? mi naona wala hakuwa na hasira apo alipowaangamiza, kwa sababu adhabu za mungu ukisikia si mchezo. Ndio mafuriko yalikuwa Suluhisho kwa Umma wa wakati, yesu na mitume wengine walikuja kwa ajili Nyumma nyengine, vizazi vya baadae Ibrahim, au Judas msaliti alikuwepo wakati wa Ibrahim?

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:

Sijui story ya upandde wa pili (wakristo), lakini, we jiulize tujaalie waliambiwa wawavamie hao watu, je kama hao watu ndio walikuwa wamevamia ardhi ya watu? anyways Upande wa waislam kama sikosei, waliahidiwa ardhi lakni kwa vile walimuudhi Mungu, basi Mungu nae aliwaacha mkono waendelee kuhangaika.

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:

Have you heard about metaphors? Anyways who has ever sat down and count the numbers of the stars? Who has ever known the population back in the days? DO you know by the time when the earth dissapears how many people would have lived in?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Maradhi hayakuumbwa kumuadhibu mtu, au allergy ya mtu sio adhabu kutoka kwa mungu, that is the beauty of the creator, anaweza kufanya vitu in different ways. Kwani wenye allergy hawali chakula? hawanywi?

7.MAJANGA ASILIA:
Majanga mengine tunajitakia wenyewe na tunayatengezea mazingira yenyewe. Mfano katika quran tunafundishwa kuwa milima ni kama pillars zenye kustabilise dunia, saivi watu wanakwenda wanachimba milima na kukata kata ili kupata dhahabu na mengineyo. Sasa kama pale Jangwani ikinyesha mvua panatokea mafuriko, afu mtu waende kueka kijumba chako, ukifika utamsingizia mungu kakuua au umejiua mwenyewe? Everything that tasted life shall go, hio ndio principle. kwaio natural disasters pia can be a way to clear the land for new beings.

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kama nlivosema hapo juu, umeonja maisha basi ikifika mda lazima urudi kwake. Na maradhi ni majaribio katika maisha, ukiumwa hio ni neema kutoka kwa Mungu, sasa unatizamwa imani yako, watu kama wewe ndio mnakimbilia kwa mganga kuchinja ng'ombe wa manjano. Dunia hakuifanya kuwa sehemu ya kuishi milele.

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Naam, jehannamu ni kwa ajili ya waovu, kama ilivo wewe mwanao wa kike akitiwa mimba uko nje ukitambua unatamani usingemzaa. Sasa jehannam wanakwenda wale waliofanya maovu kisha hawakutubia, duniani umepewa mda wa kufanya mema wewe umechagua maovu, basi hustahili kuishi pale wanapokaa watu ambao duniani wamehangaika kufanya mema. Eti we mwenyeo unaona fair kwamba wewe duniani ulikuwa unahangaika sana na maisha, ukisali sana kumuomba mungu, afu kuna rafiki yako duniani alikua na mihela na mimali, akitumbua, hana cha mungu wala nini, akipita njiani alikuwa anakumwagia maji, vipi unaona ni sawa akiwa peponi na wewe? Au tutoe mfano mwengine, we umesota mashuleni na kutafuta mavyeti, unamaliza chuo ajira unakosa lakini mshkaji wako alikuwa hasomi kaekwa bosi wizara ya fedha? Is it FAIR?

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:

Mwili wa binaadamu una kasoro? We umeumba nini kwa kweli chenye uhai?
 
kujenga hoja si tatizo mkuu, mimi nilifikiri huyu jamaa ni FREEMASON fulani ambae anatafuta wafuasi kwa kuharibu imani za watu kupitia maneno yake ambayo ukiyasoma vizuri utagundua sio kwamba huyu jamaa ana akili bali ana mapungufu makubwa ya kiimani ambayo naamini hata nicomment maneno ya aina gani hatayasadiki.
Nachokushauri acha kucomment kwanza na upitia sana nyuzi za aina hii ndiyo utawaelewa vizuri maana hivi hivi watakusumbua.
 
Hana huruma? Nafikiri angekuwa hana huruma wala rehema saa hizi uzi wako usingesomeka, Siku moja atakujibu, ndio utafahamu tofauti ya Mungu na binadamu mdhaifu mwenye uelewa mdogo. Lakini akishakujibu usisahau kuleta mrejesho ili siku nyingine mwingine asilete uzi kama huu.
Tangu nikiwa na miaka 4-5 nimekuwa nikiambiwa na kusikia nonsenses kama hizi zako......hivi hamna single nyingine.
 
Dini zinanihusu nini ? Huwezi kufikiri nje ya uwepo wa dini?
unazungumzia kufikiri!!?? hivi unajua unatumia asilimia ngapi za ubongo wako kwenye kufikiri? embu nambie iyo asilimia inatosha nini wewe kufikiria vitu vya maana kama sio kufikiria ujinga tu ulouandika apo.
 
Back
Top Bottom