Makosa 10 aliyotenda Mungu

Makosa 10 aliyotenda Mungu

1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
Kwanza mkuu mi naona hujakosea kuhoji hata kidogo...mungu ametupa maaarifa hayo kwa sababu hii unayoifanya, maana bila kuhoji hakuna elimu wala maarifa.

Ila fikiria kama tungelikua kama wanyama wengine kama hao bacteria....kazi yao ni moja tu tangu kuzaliwa kwao; kutengeneza chakula ili wazaliane, baada ya muda fulani wafe. Kwa maana hiyo hapa duniani chochote kingine zaidi ya hilo ni kawaida tu, kwao hakuna kitu "kibaya" wala "kizuri", vyote ni sawa. Kifupi wameumbwa kwa majukumu fulani tu. Sisi tumepewa utashi, kujua mema na mabaya kama Mungu mwenyewe ndio maana upo hapa unahoji.Lakini jiulize, kama kila kitu kingekua unavyotaka wewe kiwe "perfect", je dhumuni la kuishi lingekuwepo wapi?,..je ungeweza kutambua ukuu wa mungu?..je ungeweza kua na maarifa?..kama ungekua sawa na viumbe wengine, basi ningesema wewe kazi yako hapa duniani ni kuzaliana na kufa baadae, vingine havikuhusu na havipo ktk mpango wako...
 
Kwani Mkuu vitu haviwezi kuwa 'perfect' na bado maana ya maisha ikabaki pale pale?

Kwani Mungu hawezi kufanya mambo yakawa 'perfect' na ukuu wake ukawepo palepale?
 
Kwa sababu "perfection" ni point ya mwisho kabisa na baada ya hapo hakuna kitu (vacuum)...jaribu tu ku-imagine perfection unayoitaka wewe alafu angalia kweli kama vitu vya duniani hapa vitaenda...mfano perfection kwa swala ni siku ambayo atakula majani bila kuliwa na simba, so kwa kifupi simba wafe....hata ukisema wale majani, pefection ya majani ni siku ila ambayo yatachanua bila kuliwa..so wanyama wala majani wote wafe.....ukiangalia utagundua mwisho wa siku kutakua hakuna kitu hai zaidi ya mungu mwenyewe kama siku ya kwanza alivyoumba vitu

Mimi binafsi naamini kwamba, maisha "life" ni lazima yawe pande mbili ili kuleta maana ya maisha...infact nahisi shetani angetokea tu at some point, otherwise hakukua na haja ya sisi kuwa na utashi tulionao..Kumbuka biblia kwa mfano inasema jinsi Mungu alivyotuumba ila haisemi kwa nini....nahisi mfumo huu wa maisha ulipangwa tupitie.
 
Kwani pangekuwepo na matatizo/mapungufu yapi kama dunia isingekuwa na majanga asilia?
 
Kusingekuwepo na dunia kabisa...hakuna chochote ambacho ni "perfect" hapa duniani mpaka sasa.Hata wenye kusali sana wanajua hawana garantii ya kwamba changamoto za dunia hazitawapata.
 
Kwahiyo tukubaliane kwamba Mungu hajawahi kuumba kitu perfect?

Je ni kweli hakuna kitu perfect?

Mungu ana/hana uwezo wa kuumba kitu perfect? kama ana huo uwezo, leta ushahidi....tofauti na hapo hana huo uwezo.
 
Upo shahahidi wa kwambamungu aliumba vitu "perfect" lakini labda sio katika "perfection" unayoitaka wewe...anyway
Biblia inasema kwamba vitu vyote vilivyoumbwa hapo mwanzo vilikua perfect mpaka pale shetani alipotokea. Kosa la mwanadamu kudanganywa moja kwa moja lilipelekea na vitu vingine viende vibaya kwa sababu yeye alikua msimamizi wa vitu vyote,..Huu ni ushahidi wa kimaandiko.Kwa hiyo kabla ya hapo kila kitu kilikua perfect katika hali zote

Ushahidi mwingine ni uwepo wa "hesabu" na theory zake. Tunajua kwamba, uwezo wa kutengeneza "formula" ambayo inaweza kueleza matukio ya dunia, au hata ku-predict matukio hayo kihesabu ni "perfection"...sasa kwa mfano, Fibonacci Sequence ni moja ya mfumo wa hesabu ambao umeweza kutoa ushahidi kwamba, uwepo wa viungo fulani kwa viumbe hai, visivyo hai n.k unafuata pattern fulani ya ulimwengu na unaweza ku-predict nini kitafuata.Lakini pia, mathermatically, kuna "perfection" fulani katika namba hizo
fibonacci-spiral.gif

Kwa ufupi, pale vitabu vya dini viliposema Mungu ametuumba kwa mfano wake na "perfect" ilikua na maana ya kuwa na viungo vinavyotupasa kutumia, kuwa na utashi, akili n.k...sio moral issues kama unazozungumzia. Kwa hiyo yes, sisi tupo "perfect" katika hali fulani. Angalia mfano wa nyota za angani, ni ngumu kusema kama ni "perfect au sio" kwa sababu haziku-athiri kwa vyo vyote vile, hiyo ndio maana yangu ya kwamba "perfection" yako ni tofauti na ile ya vitabu vya dini.
Lakini pale utakapo kuja kujua kwamba jua(nyota) ni mlipuko wa volkano ambayo inaweza kuangamiza maisha yako, hapo utasema jua sio "perfect".

Kwa hiyo Mungu hana makosa, kila kitu kipo kwenye mpango.
 
Upo shahahidi wa kwambamungu aliumba vitu "perfect" lakini labda sio katika "perfection" unayoitaka wewe...anyway
Biblia inasema kwamba vitu vyote vilivyoumbwa hapo mwanzo vilikua perfect mpaka pale shetani alipotokea. Kosa la mwanadamu kudanganywa moja kwa moja lilipelekea na vitu vingine viende vibaya kwa sababu yeye alikua msimamizi wa vitu vyote,..Huu ni ushahidi wa kimaandiko.Kwa hiyo kabla ya hapo kila kitu kilikua perfect katika hali zote

Ushahidi mwingine ni uwepo wa "hesabu" na theory zake. Tunajua kwamba, uwezo wa kutengeneza "formula" ambayo inaweza kueleza matukio ya dunia, au hata ku-predict matukio hayo kihesabu ni "perfection"...sasa kwa mfano, Fibonacci Sequence ni moja ya mfumo wa hesabu ambao umeweza kutoa ushahidi kwamba, uwepo wa viungo fulani kwa viumbe hai, visivyo hai n.k unafuata pattern fulani ya ulimwengu na unaweza ku-predict nini kitafuata.Lakini pia, mathermatically, kuna "perfection" fulani katika namba hizoView attachment 431189

Kwa ufupi, pale vitabu vya dini viliposema Mungu ametuumba kwa mfano wake na "perfect" ilikua na maana ya kuwa na viungo vinavyotupasa kutumia, kuwa na utashi, akili n.k...sio moral issues kama unazozungumzia. Kwa hiyo yes, sisi tupo "perfect" katika hali fulani. Angalia mfano wa nyota za angani, ni ngumu kusema kama ni "perfect au sio" kwa sababu haziku-athiri kwa vyo vyote vile, hiyo ndio maana yangu ya kwamba "perfection" yako ni tofauti na ile ya vitabu vya dini.
Lakini pale utakapo kuja kujua kwamba jua(nyota) ni mlipuko wa volkano ambayo inaweza kuangamiza maisha yako, hapo utasema jua sio "perfect".

Kwa hiyo Mungu hana makosa, kila kitu kipo kwenye mpango.
Mara useme hakuna kilicho perfect, mara useme kila kitu kiliumbwa perfect,....sasa nikueleweje?

Kusema kila kitu kiliumbwa perfect ila baada ya Shetani kuasi aliharibu ile perfection, inadhihirisha kwamba vitu viliumbwa bila perfection.Maana kama vingekuwa perfect, Shetani asingeweza kuviharibu.
 
Kwahiyo tukubaliane kwamba Mungu hajawahi kuumba kitu perfect?

Je ni kweli hakuna kitu perfect?

Mungu ana/hana uwezo wa kuumba kitu perfect? kama ana huo uwezo, leta ushahidi....tofauti na hapo hana huo uwezo.
"Perfection is determined by your desire "
Unataka kitu kiwe hivi lakini kiko vile ,kwa hiyo hakiko perfect.
Ulitaka uishi milele ,lakini kwa vile unakufa uhahi siyo "perfect".
Macho ulitaka yawe na nusu kipenyo(radius) kama shilling I ,lakini kwa vile yapo " oval generally "hayako "perfect".
Kwa hiyo basi:- kama mambo yalivyo ndiyo ilikuwa Desire ya mungu ,alikuwa ,ni na ni perfect forever!
Shetani unayemzungumzia ni "malware"kwenye operating system ya Bin Adam na ali " install " yeye mwenyewe !sababu ?rudi baadaye
 
Maelezo yako ni kwa mujibu wa nani/nini?

Hanajibu hoja ipi?
 
Nasikia aliyeandika hii thread ni marehemu,
Imani ni tiba
 
Kwahiyo tukubaliane kwamba Mungu hajawahi kuumba kitu perfect?

Je ni kweli hakuna kitu perfect?

Mungu ana/hana uwezo wa kuumba kitu perfect? kama ana huo uwezo, leta ushahidi....tofauti na hapo hana huo uwezo.
Uwezo anao...yeye kafanya hvo ili kuleta maana halisi ya maisha. ili tuishi kwa kutegemeana. ndo maana kuna maskin na tajiri..mlemavu na mzima ili hawa watu wasaidiane. mungu hajaumba kitu perfect ndo maana kuna hii kauli kuwa hakuna aliyekamilika isipokuwa yeye tu Mungu.Sisi tukiwa perfect na yeye atakuwa nani sasa. tumepewa maarifa tu ya kutambua jema na baya.
Na ndo maana kwenye bible kuna mistari inasema wapo walioumbwa kwa ajili ya wakati wa ubaya na wapo walioumbwa kwa ajili ya wakati wa mema ili neno lake lipate kutimia. upaswi kureason sana unaweza ukakufuru. kuwa na iman iliyoshiba tu kama utachagua upande wa mungu au wa shetani ni maamuzi yako.
 
Kama Mungu aliumba imperfections, basi avumilie madhara ya hizo imperfections.
Kitu kingine, kungekuwepo ubaya gani kama watu wote wangekuwa 'perfect'

Je Mungu ni mkamilifu au lah!.....weka ushahidi wa jibu lako.
 
Back
Top Bottom