MAJIBU YA MASWALI YAKO MATATU YA MWANZO
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ogomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.
KATIKA SWALI LAKO HILI NAOMBA UTAMBUE YAFUATAYO:-
MISINGI YA FALME KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
Tangu milele hapakua na falme mbili zinazopingana bali ufalme wa Mungu baba peke yake muumba wa mbingu na nchi na vyote vinavyoonekana na visivyoonekana Mwa1:1. Visivyoonekana ni malaika watakatifu walio mbele zake wakimtumikia katka makundi tofauti tofauti kama ifuatavyo:-
Ø Malaika wakuu-kuna wenye uhai wanne ambao wako mbelle ya kiti cha enzi ufu 4:1-11
Ø Malaika walinzi-yakiogozwa a malaika Michael Dan 10:13
Ø Malaika wa uponyaji-likiongozwa na malaika Rafael Tob3:17
Ø Kundi linguine ni la malaika wajumbe wa Mungu linaloongozwa na malaika Gabriel Dan8:16 &9:21
Ø Kuna maserafi hawa pia wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu baba Isa 6:1-3.
CHANZO CHA UFALME WA UPINZANI AU SHETANI-Ni kutoka katika kundi la malaika wanaoitw makerubi, kudi hili liliogozwa na malaika aayeitwa lucifel, huyu alimhasi Mungu kutokana na uzuri wake alopewa na Mungu pia alikuwa kiongozi wa kikundi cha kusifu na kuabudu (praise and worship) hivyo baada ya kuasi/kunajisi akatimuliwa/akafukuzwa mbinguni pamoja na wale wote waliomtii. Na kwa kuwa alishanajisi, mahala pake pia kule mbinguni paliondoshwa pamoja naye na ule uweza wa kubadilikabadilika sura. (Ufunuo 21:27) Hakuna kilicho najisi kitakachoona/kugusa mbingu.
SIFA ZA MAKERUBI-Ni malaika wa kipekee wenye sura nne kama ifuatavyo:-
i. uso wa binadamu
ii. . Ng’ombe au mifugo ya aina mbalimbali(representing all domestic animals)
iii. . Kama tai ndege wa angani na
iv. .Simba representing all wild animals(ezek1:10)
Baada ya Lucifer kufukuzwa mbinguni alianzisha ufalme wake unaopinga kufanyika mapenzi ya Mungu na kuwazuia wale wanaomtii Mungu wasimtii wawe waasi kama yeye Mwa3:15 “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake. Huo utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino” Kutokana na maelekeo ya kutenda dhambi yaliyoko ndani ya mwanadamu, shetani anayatumia maelekeo hayo maelekeo ya kutenda dhambi yaliyoko ndani ya mwanadamu kuwafanya watu kuwa watumwa wa dhambi kwa kuwa imeandikwa “Yesu akawajibu Amini amini nawaamia kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi”(Yoh. 8:34). Kwa sababu hiyo kila mtu atambue ya kwamba yupo kwenye mapambano na shetani daima mpaka mwisho wa maisha yake hapa duniani. Shetani anawatumia mawakala wake kuwadanganya na kuwashawishi watu kumuasi Mungu na kumtii yeye na ia yake ni kuwatawala watu wote ulimwenguni na kuhakikisha anawapata wote ikiwezekana awaingize kwenye utawala wake wamtumikie hapa duniani na hatimaaye kwenye makao yake makuu ambako ni jehenamu. Vita hii ni kali sana kwa mwanadam anayempenda Mungu hakubali kutawaliwa na shetani, anapambana vikali ili amshinde shetani na kuipata ile ahadi ya uzima wa milele hivyo basi hali hiyo ya mapambao kati ya wanadamu na shetani ndiyo inaitwa VITA VYA KIROHO
Ndugu yangu tambua kwamba shetani hana lolote mbele ya muumba wake na anamwamini Mungu ila hashiki amri na maagizo yake kumbuka pale bustanin, shetani alichokifanya ni kugeuza maagizo ya Mungu. Mungu alisema MKILA MTAKUFA, shetani yeye akawambia HAKIKA HAMTAKUFA. Maandiko matakatifu yanatuonesha wazi kuwa shetani anamwamini Mungu ila kutii sharia na maagizo kama nilivyosema hataki (Yak. 2:19) “Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka”
HIVI NDIVYO LUCIFER ALIVYOKUA KABLA YA KUASI Ezekiel chapter 28
28:13 Thou hast been in Eden the garden of God; every precious stone was thy covering, the sardius, topaz, and the diamond, the beryl, the onyx, and the jasper, the sapphire, the emerald, and the carbuncle, and gold: the workmanship of thy tabrets and of thy pipes was prepared in thee in the day that thou wast created.
28:14 Thou art the anointed cherub that covereth; and I have set thee so: thou wast upon the holy mountain of God; thou hast walked up and down in the midst of the stones of fire.
28:15 Thou wast perfect in thy ways from the day that thou wast created, till iniquity was found in thee.
28:16 By the multitude of thy merchandise they have filled the midst of thee with violence, and thou hast sinned: therefore I will cast thee as profane out of the mountain of God: and I will destroy thee, O covering cherub, from the midst of the stones of fire.
28:17 Thine heart was lifted up because of thy beauty, thou hast corrupted thy wisdom by reason of thy brightness: I will cast thee to the ground, I will lay thee before kings, that they may behold thee.
28:18 Thou hast defiled thy sanctuaries by the multitude of thine iniquities, by the iniquity of thy traffick; therefore will I bring forth a fire from the midst of thee, it shall devour thee, and I will bring thee to ashes upon the earth in the sight of all them that behold thee.
28:19 All they that know thee among the people shall be astonished at thee: thou shalt be a terror, and never shalt thou be any more.
HAYA NDIYO MAPINDUZI ALIYOPANGA/ ALIYAKUSUDIA LUCIFER KUYAFANYA Isaya 14
14:13 Lucifer alisema moyoni mwake “nitapanda mpaka minguni,nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; nami nitaketi juu ya mlima wa makutano, katika pande za mwisho za kaskazini.
14:14 nitapaa kupita vimo vya mawingu, nitafanana na yeye Aliye juu”
ANGALIZO:
Mungu ni mwenye haki kwa viumbe wake wote ndo maana anaitwa Hakimu wa HAKI, kitu anachokifaya shetani anatumia sharia na kanuni za ulimwengu wa roho kututishia kwa kubweka kama mbwa asiyekua na meno kwenda kutushtakia ile hali hati ya mashtaka Kristo Yesu alishamg’aya shetani na ikatundikwa juu ya msalaba wake
NB: Nyoka alikubali kumpa shetani lifti (msaada wa kumfikia mwanamke) kwa kua alikua mwelevu saa lakini tazama mwisho wake leo ni kula vumbi tu.
2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.
Kufuatana na taratibu na kanuni ambazo Mungu ameziweka ni mwiko kwa mtu mwenye dhambi kutaka mashauri kwake bila kutubia dhambi alizonazo kwanza Mwa3:24 Basi Mungu akamfukuza huyo mtu akaweka upande Makerubi upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima. Lakini ukumbuke vizuri kabla ya kutenda dhambi mtu aliongea na alikua anamuona Mungu live akiwatembelea bustanini Mwa 3:8. Hivyo basi utakatifu wa Mungu hauruhusu yeyote mwenye dhambi amuone kabla ya toba.
Isa 59:1&2”Tazama mkono wa Mungu haukupunguka, hata asiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia. Lakini maovu yenu yamewafarakanisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia ”.
Kama unataka kuamiani hayuko mafichoni uamini na kumkiri Yesu kwa kinywa chako kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako, na kuamini moyoni mwako kuwa Mungu alimfufua katika wafu utaokoka (Rum10:9) uhalali wako wa kumilki na kutawala kama kusudi la Mungu kukuumba utarejeshewa na kumuona Mungu katika ulimwengu wa roho na atakuonesha yupi nabii wa ukweli na yupi nabii wa uongo
3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.
Kweli kabisa ndugu yangu after causes there’s effects hata wanafizikia wamesema “To every action there is an equal and opposite reaction” Uelewe kwamba unapokwenda kinyume na amri za Mungu na maagizo yake wewe ni muasi na umetenda dhambi, hivyo basi kizazi kile kiliteketea kwa gharika wakati wa mzee Nuhu badae wakati wa Ibrahim wakateketea kwa moto watu wa sodoma the same ata kizazi hiki kimewekwa akiba kwa moto. Haya yote yanafanyika kwa makusudi ili watu wajifunze taratibu na kuamua toka mioyoni mwao kipi cha kufuata kati ya Baraka na laana au uzima na mauti. Nyakati zote hizo walitumwa wajumbe wa Mungu (Manabii) ili kuonya, kukemea na kufundisha juu ya ufalme wa Mungu ambao ni wa Amani, haki na furaha (Rum14:17) “Maana ufalme wa Mungu si kula na kunywa bali ni haki na Amani na furaha katika Roho Mtakatifu”
WATU WAOVU WAMETOKA WAPI
Kama nilivyokuambia katika swali lako la kwanza kuna mapambano makuu au vita ya kiroho kati ya mwanadamu na shetani, ambapo wale wanaomtii shetani ndo hao walio waovu wa leo utawasikia wamewanajisi watoto wadogo, wako guest house wanaita show time na kupiga picha za uchi,wafiraji, watukanaji, waabudu sanamu, wachawi, washirikina n.k