Sawa sawa na hayo ndio yalikuwa madhumuni yangu mimi kuuliza hayo maswali na endapo kama ungesema haumani uwepo wa hivyo vyote viwili basi ningeaachana na wewe na kuamini kweli wewe ni pure atheist.
Lakini badala yake wewe umeonesha undumilakuwil na kunipa mashaka na huo msimamo wako, yaani unapinga uwepo wa Mungu wakati huo huo kuna vitu ambavyo chimbuko lake ni Mungu unakubaliana navyo.
Kama unakubali uwepo wa Freemasonry ambayo kihalisia ni dini/jamii ya kishetani, hauoni kwamba hapo tayari umeshakubaliana na uwepo wa Mungu?
Kwa sababu huyo shetani/ibilisi ambaye ndio mwenye hiyo dini ya Freemasonry chimbuko lake ni Mungu.
Kuamini kwamba kuna mtu anaamini kwamba kuna pembetatu duara ni kuamini kwamba kuna pembetatu duara?
Unafahamu kwamba kuna watu mpaka leo wanaamini kwamba dunia ni bapa na si tufe?
Ukikubali kwamba watu hawa wapo maana yake na wewe umeamini dunia si tufe ni bapa?
Unafahamu kwamba kuna watu hawaamini kwamba kuna HIV na UKIMWI?
Ukikubali kwamba hawa watu wapo maana yake unaamini hakuna HIV na UKIMWI?
Unafahamu kwamba kuna vibabu huko vijijini bado vinaamini Julius Kambarage Nyerere ni rais wa Tanzania?
Ukikubali kwamba watu hao wapo maana yake umekubali kwamba Julius Kambarage Nyerere ni rais wa Tanzania?
Unafahamu kwamba kuna Wamarekani wanaamini kwamba Tanzania ni kisiwa kilichopo pwani ya Australia?
Ukikubali kuwapo kwa watu hao hilo lina maana umekubali kwamba Tanzania ni kisiwa kilichopo pwani ya Australia?
Unafahamu kwamba kuna watu wanaamini mlima Kilimanjaro uko Kenya?
Ukikubali kwamba kuna watu wanaamini mlima Kilimanjaro upo Kenya hilo lina maana unaamini mlima Kilimanjaro upo Kenya?
Ukiwa unaamini mungu yupo na unaamini kwamba kuna watu wanaamini mungu hayupo, kuamini kwamba kuna watu hawaamini mungu yupo kunaondoa imani yakobya kuamini mungu yupo?
Kukubali kwamba watu wana imani fulani hakumaanishi kwamba umekubali kwamba imani hiyo ni sahihi.
Unaweza kukubali kwamba kuna watu wanaamini kula nyama ya mtu kunawaongezea nguvu za uchawi wakati wewe mwenyewe hukubalibkwamba imani hiyo ina msingi sahihi.
Hujaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo.
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao ubaya unawezekanika? Hususan kwa sababu aliweza kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekaniki na asipungukiwe chochote?