Mkuu umesema vyema kabisa...mtu anapopatwa na shida au kukumbana na jambo la kumchanganya, huingiwa na hofu na kuanza kutafuta majibu kokote, iwe kwenye nyumba za ibada au kwa waganga. Akikosa majibu husema ni kazi ya Mungu...kaangalie ile filamu ya God must be crazy...bushman anaokota chupa ya cocacola then anasema Mungu kaidondosha, simply bcoz hajawahi kuiona.Dhambi zetu ndiyo chanzo cha laana zote sasa Mwenyezi Mungu kosa lake lipi? Wamlaumu kwa makosa ya wenye viburi na tamaa zisizosikia sheria!
Suala la imani ya uwepo wa Mungu/Miungu linahusiana sana na upungufu wa maarifa kwa binadamu juu ya maisha na kila kilichopo duniani. Pale ambapo binadamu maarifa yalimpungukia na akakosa majibu ya baadhi ya mambo aliamini kuwa kuna kitu mahali kinaweza kuwa na majibu. Zaman hata kupatwa kwa jua au mwezi kulihusishwa na Mungu kwa kuwa hakukuwa na maelezo kutokana na maarifa kuwa finyu. Kadri maarifa na ujuzi unavyopanuka suala hili linapungua nguvu. Maana saiz watu hata wana uwezo wa kufahamu Jua (kama mojawapo ya nyota ndogo tu ndani ya Milky way galaxy) linatoa wapi mwanga na joto lake na kwamba nuclear fusion hiyo inaweza kukoma lini, n.k. Na mifano ya kutengeneza nuclear fusion kama inayotokea juani imeshaonekana hapa duniani bila suala la Mungu au likiumbe likubwa linalokaa sehemu flani kuhusika. Kwahiyo mtoa mada amekuwa mwanafalsafa kiasi ingawa baadhi walioamini na hawapendi kuhoji (kama wewe) watamshambulia.
Magu alisema wale walioimba 'wana imani na nani sijui' angewatimua wote siku hiyo hiyo... Mimi nasema kama ningelikuwa Mungu pindi tu kidole chako kinabonyeza kitufe cha kupost hapo hapo ningekugeuza senene!!
Unafanya dhihaka kama hizi na bado uko hai! Aisee Mungu ana uvumilivu wa hali ya juu sana... Mwacheni Mungu aitwe Mungu!!
Like anazo 15.Na akapata 5 LIKES
Maneno ya mkosaji hayo. Kwanini ulete vitisho badala ya hoja? Au ndio kukubali kwamba huyu mungu ni mshindwaNaamini kwa kufuru hizi Chamiton unahitaji kutubu kwa Mungu ama sivyo siku zako si nyingi hautakuwepo duniani ,naapa kwa Mungu kwa jina la Yesu kwa hili umekosa kitu cha kudhihaki.
Jamaa yeye kauliza maswali tu na anataka ajibiwe ili imani yake izidi kuimarika zaidi.Naamini kwa kufuru hizi Chamiton unahitaji kutubu kwa Mungu ama sivyo siku zako si nyingi hautakuwepo duniani ,naapa kwa Mungu kwa jina la Yesu kwa hili umekosa kitu cha kudhihaki.
Nani alikuambia Adam na Eva walikuwa weupe?Nakuunga mkono! Kama Mungu aliumba Adam na Eva wawili tu weupe wakazaana. Uzao wao ukawa mweupe, sasa sisi waafrika weusi tulitoka wapi? Ukiuliza unaambiwa unakufuru!
Hakuna anayeijua biblia, tunajifunza kila kukicha.Hamna sense hapo lete mada nyingine hiyo noooooooooo! Tatizo hijui biblia umegusa gusa vitu kidogo bila kutafuta majibu You know nothing.
Mungu anatupenda na ndio maana ametupa utashi wa kutambua baya na jema, amekupa uwezo wa kuchagua kipi chema kwako na kipi si chema.Wanasema
Mungu anatupenda sana kwa moyo wote but km kweli anatupenda kwann kamleta shetan??
Wanasema pia mungu n powerful kuliko kitu chochote....ila pamoja na nguvu zake kashindwa mwondosha shetan na bado wanasema anaupendo
Vilivile wanasema ana huruma..hv kama ana huruma ,upendo na nguvu..katuletea shetan wanini??
Inatia wacwac kwakweli
Mm nasema kama mungu hapenzwi kwa jinsi navyo ishi yeye ndio aje kuniambia mm sio hawa waarabu na wazungu.na vitabu vyao vya kusadikika hata siwaelewi
Kuuliza si ujinga ni kutaka kujua. Kuna wenye elimu ya theolojia na Sana elimu ya haya mambo na wanaweza kumjibu vyema. Kama huna majibu usikimbilie kuchukua nafasi ya Mungu kuhukumu kuwa anamdhihaki MunguKushiba ni kubaya sana!!!......Wewe kijana unamdhihaki Mungu kisa unakula na kushiba vizuri na una afya njema ya kuingia kwenye mitandao ya kijamii????
Hapa huenda ukawa na hoja na kwa sababu umefikiia mawazo haya baada ya kuwaza, kufikiri na kutafakari, ni wazi ukiendelea kufanya hivyo uaweza kufikia mawazo makubwa zaidi.Mbona unaimba Ngonjera? Kwaiyo walio na kansa, wanaojinyea na walioko mahospitali ndio tuseme kuna mungu muweza au mungu dhaifu?
Wewe kijana unaabudu uoga!
Narudia tena kwamba hakuwezekani kuwe na Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo, muweza wa yote, muumbaji wa vyote.
Kama atakuwepo mungu wa hivo atakuwa sio mungu bali ni mshindwa wa mwisho.
Fikiri kijana acha kukalia akili zako
HAKUWEZEKANI KUWE NA MUNGU MSHENZI NAMNA HIYO.
Watu wanateseka hovyo, watu wanakufa, watu wanadhulumiana, watu wanaibiana, watu wanateseka na njaa hadi kufa alafu uje uniambie kuna mshenzi kajikalia eti ndio aliyeumba vyote na anaweza yote na ana upendo.
Huo utakuwa ni ulimbukeni wa Mungu
Suala la Mungu halina dini. Jamaa amehitaji kuoewa elimu. Ni vyema akaelimishwa, kutokuwa na majibu kwako kusikufanye kuchukuwa nafasi ya Mungu kuhukumu kuwa anadhihakiwa. Muachie mungu nafasi yake . Mwanzilishi wa thread ajibiwe tusirahisishe. Wanatheolojia watujibu coz wana majibu kama huna unapotezea tuUSIMDHIHAKI MUNGU HATA KIDOGO, huwezi kufanya conclusion ya kuwa hakuna Mungu kwa kufanya reference ya kitabu kimoja cha DINI, wakati duniani Kuna DINI nyingi sana, UISLAM, BAHAYI, HINDI, nk na bado huwezi kusema Mungu hayupo wakati kunasayari nyingi sana ULIMWENGUNI,vipi kuhusu viumbe wanaoishi sayari nyingine wanamuabudu Nani ? Inamaana wewe unaakili nyingi sana kuliko watu wote wanaomuabudu MUNGU ALIYE HAI, TANZANIA, AFRICA, DUNIANI na SAYARI ZINGINE. Embu achana na hii habari ya MUNGU BABA, ongea kitu kingine.