Naongea na mtu asiyejua anaongea nini??.
Hiyo kanuni Newton alianza nayo vipi??.
Alianza na "Hypothesis" baada ya lile tufaa kumuangukia kichwani alipokuwa ameketi chini ya mti wa mtofaa (apple tree), na hypothesis yake (prediction) akahisi kwamba lile tufaa lilivutwa na nguvu fulani kuelekea chini, kwa sababu alijiuliza kwanini lisingeenda juu au pembeni au kuelea ama vyovyote??!!, hakuishia hapo tu bali alijiuliza kwamba ni nguvu hizo hizo ndizo zinazoushikilia mwezi pale ulipo kutoka duniani na hiyo ndiyo inaitwa hypothesis au prediction na aka -conclude kuwa kati ya vitu viwili siku zote kunakuwepo na nguvu za uvutano na baada ya hapo akataka ku 'formulate" uhusiano kati ya nguvu ya uvutano uliopo kati ya vitu viwili na kanuni hiyo akaiita "the law of universal gravitation"
Katika ku formulate hiyo kanuni akaweka "assumption" moja inayoitwa "the inverse square law"
Force=constant /r², (where r = is the distance between the given bodies).
Baada ya hapo ndipo akaja na formular kamili:-
Force=GmM/r² , ambayo inasema:-
"The force between two bodies is direct proportional to product of their masses and inversely proportional to the square of their distance apart"
Sasa huyo Newton kwanza alianza na hypothesis (prediction/ ramli) baadaye akaweka "assumption" na hatimaye akakamilisha formular, sasa nani hapo ni mpiga ramli Qur'an au Newton??
Umeshikilia kuwa Qur'an ilitungwa na Nabii Muhammad (saw), (Mungu apishe mbali), inafahamika kabisa kuwa Mtukufu Mtume Muhammad (saw) hakujua kusoma wala kuandika bali Mungu alimfunulia Qur'an yote na waandishi wake wakaandika yale yote aliyofunuliwa na Mungu na ndiyo maana Mungu anatoa "challenge" katika Qur'an aliposema:- " Ikiwa mna mashaka juu ya yale tuliyomteremshika mja wetu (Muhammad) basi leteni sura moja mfano wa hii (Qur'an) na muwaite wasaidizi wenu kinyume na Allah ikiwa mu wakweli (2:23).
Chukua mfano mmoja, Qur'an inazungumzia juu ya "the expanding universe":-
و ا للسماء بنيناها بايد و انا لموسعون
Wa ssamaai banainaahaa biaidi wa inna lamuusiu'un. (51:47)
Yaani, " Na mbingu tumeziumba kwa uwezo (mikono) yetu na hakika tunaipanua (lamuusiu'un)."
👆🏻Ni Albert Einstein (d1955) na Edwin Hubble (d 1953) ndiyo waliokuwa ma pioneers wa "the expanding universe" hypothesises zao (RAMLI ZAO) walifanya katika karne ya 20 tu juu ya ulimwengu unaotanuka Allah aliliweka jambo hilo kupitia mtume Muhammad (saw) toka karne ya 14 wakati hata wana sayansi hao hawakufikiriwa kama wangezaliwa sembuse kuwa na mawazo ya kujua kwamba ulimwengu unatanuka!!, bila shaka hawa walisoma Qur'an kwa siri ndipo wakajua ukweli huo.
Kuna mifano kadhaa ya sayansi ndani yavQur'an ambayo wanasayansi wenye roho safi wanakiri hadhatani kuwe Qur'an isingeweza kutungwa na nabii Muhammad (saw) bali imetoka kwa yule mwenye elimu kubwa sana, sisi tunasema Qur'an imetoka kwa Yule aliyekuwa na elimu isiyo na kikomo yaani ALLAH (sw).