Makosa 10 aliyotenda Mungu

Ibilisi, Shetani, Malaika, Mungu, Malaika yote ni majina ya hadithi tu.

Si majina ya vilivyopo kiuhalisia.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha hata kimoja kati ya hayo majina kipo kwa uhalisia.
Na mimi naunga mkono hizo ni ID fake kama za Jf

Lakini nyuma wapo the real 'Anunaki' mpende msipende
 
Hakuna kitabu cha Mungu.

Kwa sababu Mungu hayupo.

Mungu angekuwepo na angetaka tumjue, angetupa habari zake zote kwenye DNA na kwenye ubongo tumjue bila kitabu.

Kwa namna hiyo, Wadigo wasingelalamika kwamba hawajui Kiarabu na hivyo hawawwzi kusoma Quran.

Wewe huoni Mungu aliyeshusha yabari zake kwa Waarabu kawapunja Wadigo?

Huoni kwamba ni upumbavu kwa Wadigo kuacha kuelekea kwao, inakuwa wakisali wanaelekea Mecca?

Huoni kwamba huu ni ukoloni wa kidini na kushikiwa akili?
Ulishawahi kujaribu kutafuta majibu ya maswali yako kupitia hivyo vitabu?
 
1.KUMUUMBA SHETANI:
Hili lilikuwa kosa kubwa sana. Makosa yate yamechepuka kutoka hapa. Shetani anawasababishia watu maovu, then Mungu anawahukumu watu dhaifu. Hapa Mungu inambidi amkamate shetani na kumtokomeza ili maovu yaishe, kama wote wanatoshana nguvu basi wasuluhishe ugomvi wao na kupatana ili maisha yawe ya amani.

2.KUISHI MAFICHONI:
Toka enzi na enzi, Mungu amekuwa akiishi mafichoni, kwanini asijitokeze na kujionesha kwa viumbe vyake? Anaishi mafichoni kwani yeye ni Joseph Kony? Hili limepelekea watu wake kudanganywa na manabii wa uongo na kutapeliwa bure. God come from your hidings and reveal yourself to your people.

3.MAFURIKO YA WAKATI WA NUHU:
Mungu alisababisha mafuriko ili kuangamiza watu waovu na kubakiza watu wema, Yes he did, sasa waovu wa leo wametoka wapi? mbona aliuwa watu wengi bila huruma? Kama mafuriko yalikuwa ni suluhisho la maovu, Yesu na mitume walijia nini? It seems he fought effects instead of causes.

4.SAFARI YA WANA WA ISRAELI:
Mungu aliwatoa wana wa Israel kutoka Misri kwa madai ya kuwapa nchi ya ahadi, matokeo yake aliwaamuru wafanye uvamizi wa nchi za watu(mf. waamori, wamoabu na wakanani). Kwanini asingebadilisha jangwa na kuwatengenezea waisraeli nchi yao? mbona Gadaffi aliweza? Imagine waje wapuuzi hapa TZ wachukue nyumba na ardhi kwa madai kwamba wameagizwa na Mungu, ungereact vipi? WE HAVE TO BE FAIR!

5.KUTOTIMIZA AHADI YAKE KWA ABRAHAM:
Mungu alimwambia Abraham kuwa atampatia uzao wa wana wengi kama nyota za angani au mchanga wa pwani. Sasa hivi ukichanganya walio wa Abrahamu na wasiyo wa kwake bado watu hawawezi kuwa sawa na nyota au mchanga wa pwani. Ata ukijumlisha na waliokufa back to Adam. Atatimiza lini hi ahadi? je kuna muda wa kutosha? mbona watumishi wake wanasema Yesu yuu karibu kuja ili kutamatisha nyakati?

6.KUWEPO KWA MZIO(ALLERGY):
Kwanini watu wengi ambao ni wema wana allergy na vitu alivyoumba Mungu? mbona maandiko yanasema kila alichoumba Mungu ni chema? Kwanini aumbe mimea na wanyama wenye sumu kwa watu wake awapendao? au hakujua?

7.MAJANGA ASILIA:
Kama Mungu aliumba dunia ili iwe sehemu ya amani kwa watu wake na wamwabudu yeye, kwanini kuna matetemeko ya nchi, vimbunga na mafuriko. Kwanini anawauwa watu kikatili hivi? au haya nayo tumsingizie shetani?

8.KUUMBA VIUMBE HATARISHI:
Kwanini Mungu aumbe bacteria, virusi, fangasi na viumbe wengine wanaosababisha magonjwa na kifo? Kwanini hawa viumbe wasingefia kwenye yale mafuriko ya Nuhu ili watu wema alio wabakiza waishi kwa amani? Je hawa viumbe hatari Mungu alimwamuru Nuhu awaingize wawili wawili kwenye safina?

9.JEHANAMU NA MOTO WAKE:
Kwanini Mungu aumbe jehanamu kuteketeza waovu? Kwani hajui kusamehe? Kwanini huruma yake ina kikomo kwa shetani? Kama wewe ni mzazi, mwanao akikukosea na hajaomba msamaha, itabadilisha uhalisia kuwa yule sii mwanao? SHETANI PAMOJA NA WAOVU NI KAZI YA MIKONO YAKE, PRODUCTS OF HIS OWN MIND BEFORE CREATED THEM. So aache kuweka vinyongo na kutamani kulipiza kisasi juu ya kazi yake.

10.KASORO KWENYE MWILI WA BINADAMU:
Kwanini pawepo na mabadiliko hasi kwenye jeni za binadamu(mutation)? kwani hakujua hicho ni chanzo cha viwete??? Kidole tumbo(appendix) ni cha kazi gani? mbona hajatoa maelezo namna ya kukitumia? Na chuchu za mwanaume ni za kazi gani?

TO THE RIGHT WING OR THE LEFT WING WE ARE NEITHER, NOT EVEN AT THE MIDDLE....R.I.P MOBUTU!

===================
Nonsense
 
Kubishana na mtu kuhusu imani yako ambayo yeye haikubali au kuiamini ni kupoteza muda na haiwezekani kukubaliana. Lakini kupinga imani ya mtu mwingine ambayo wewe huiamini ni upumbavu.

Tafsiri ya neno IMANI ni nini?
Kwa tafsiri rahisi, imani ni kuamani jambo, habari, tukio au uwepo au kutokuwepo kwa kitu au jambo ambalo wewe huwezi kutumia milango yako ya fahamu kuthibitisha ukweli au uhalisia wake. Huwezi kuona, kusikia, kugusa, kuonja au kunusa kitu hicho, ila unaamini kuwa kipo, au kiliwahi kuwepo au kitakuwepo baadae. Tofauti na hivyo hiyo sio imani ni uhalisia.

Sasa suala la uwepo au kutokuwepo kwa Mungu ni la kiiamani. Sio linalothibitishika kimaumbile katika hali ya kutumia milango ya fahamu. Ndio sababu katika kubishana kote nashangaa kwanini hamjauliza ROHO ni nini katika uhai wa binadamu?

Na je, BODY, MIND and SPIRIT vina uhusiano wowote katika uhai au afya ya mtu?

Kitu cha kujua ni kuwa, wewe kutoamini anachoamini mwingine hakufanyi kitu au imani hiyo kuwa ya uongo, ikiwa utadhani hivyo lazima uwe mpumbavu, maana, unawezaje kupinga kitu usichoamini wewe kwa kusema sio kweli? Hii ni sawa na kusikia watu wansongea lugha usiyoielewa kisha ukawaambia wanakosea, wakati lugha hiyo huielewi, utakuwa mzima wewe?

Asiyeamini uwepo wa Mungu atambue hiyo pia ni imani. Sio sayansi. Maana kama ni sayansi basi athibitishe kuwa hayupo. Na ili athibitishe lazima awe na majibu tayari (hypotheses) kuwa ili Mungu asiwepo inatakiwa iwe hivi au vile. Sasa unawezaje kutaka kuthibitisha kuwa kitu fulani hakipo wakati hujui ili kisiwepo inatakiwa kiweje?

Anayeamini Mungu yupo hiyo pia ni imani. Anaweza kuithibitisha kiimani hivyo hivyo ila kwa mtu mwingine anayemiani pia. Hawezi kuthibitisha kwa mtu asiyeamini maana hizo ni lugha mbili tofauti zisizotafsirika moja kwa nyingine.

Nakumbusha tu, kupinga imani usiyoiamini wewe ni upambavu. Mtu anayeamini mlima acha aamini mlima. Ndio imani yake. Ukija wewe kumwambia huo mlima sio kweli, yeye pia anaweza kukwambia huyo anayemuamini sio kweli.

Sayansi na imani ni vitu viwili tofauti. Kujaribu kuvifaya kimoja kithibitishe kingine ni zaidi ya upumbavu.
 
THE REAL GT
 
Quran imetungwa na watu tu, tena ngumbaru kamaulivyosema wasiojua kusoma.

Ndiyo maana imejaa contradiction.

Hapa unaambiwa Allah ana rehema zote na ni Mungu wa haki.

Pale unaambiwa kuna watu Allah anawafunga mioyo, macho na masikio, wasimjue. Kisha anawahukumu kwa adhabu kubwa sana, kwa sababu hawakumjua.

Sasa mtu hujiulizi, huyu Allah mwenye rehema kubwa sana, mwenye upendo mkubwa sana, mwenye haki kuu, kwa nini anawafunga macho, masikio na mioyo viumbe wake?

Allah akiwafunga macho, masikio na mioyo viumbe hao, maana yake hata wajitahidi vipi kumjua Allah, hawatamjua.

Sasa anawafunga macho, masikio na mioyo, wasimjue. Halafu, wasipomjua, anawaadhibu kwa kutomjua.

Huyo Allah ni Mungu au kichaa?

Yupo kweli? Au hadithi za kutungwa na watu tu?

Unapaswa uelewe tunajadili nini,hapo kwenye red ndio suala tunaojadili hapa kwamba Qur'an imetungwa tu na watu tena Ngumbaru wasiojua hata kusoma.

Ndio maana nikakuwekea maelezo ya wanasayansi wakielezea Qur'an kwa mambo yenye kuhusu sayansi,Qur'an ambayo wewe unasema wamejitungia tu mangumbaru. Ila ajabu unalipotezea hili na kukimbilia contradictions.

Hoja ya msingi ni kwamba Watu tu Mangumbaru wamewezaje kutunga masuala kama hayo ya kisayansi?
 
Watu ambao wamewahi kuathiriwa na mambo ambayo umeyataja mfano allergy, natural disasters, n.k. na wamekata tamaa ndio huwa wanaandika nyuzi za hivi. Am guessing your one of them
 
Unapaswa uelewe tunajadili nini,hapo kwenye red ndio suala tunaojadili hapa kwamba Qur'an imetungwa tu na watu tena Ngumbaru wasiojua hata kusoma.

Ndio maana nikakuwekea maelezo ya wanasayansi wakielezea Qur'an kwa mambo yenye kuhusu sayansi,Qur'an ambayo wewe unasema wamejitungia tu mangumbaru. Ila ajabu unalipotezea hili na kukimbilia contradictions.

Hoja ya msingi ni kwamba Watu tu Mangumbaru wamewezaje kutunga masuala kama hayo ya kisayansi?
Kwani ngumbaru asiyejua kusoma hawezi kujua sayansi?

Mbona kuna ngumbaru wasiojua kusoma ni herbalists wanatibu watu kwa mitishamba, lakini bado ni ngumnaru wasiojua kusoma.

What is your point?

Kitabu cha Mungu kinakuwaje na contradiction? Mbona suala la contradiction hulijibu?

Unaelewa kitabu kikiwa na kila kitu sawa, kikawa na kosa moja tu, tayari kimeingia doa na hakiwezi kusemwa sawa kwamba ni cha Mungu?

Huyo Mungu alishindwa kufanya Quran ikose contradiction?
 
Kubishana na mtu kuhusu imani yako ambayo yeye haikubali au kuiamini ni kupoteza muda na haiwezekani kukubaliana. Lakini kupinga imani ya mtu mwingine ambayo wewe huiamini ni upumbavu.

Tafsiri ya neno IMANI ni nini?
Kwa tafsiri rahisi, imani ni kuamani jambo, habari, tukio au uwepo au kutokuwepo kwa kitu au jambo ambalo wewe huwezi kutumia milango yako ya fahamu kuthibitisha ukweli au uhalisia wake. Huwezi kuona, kusikia, kugusa, kuonja au kunusa kitu hicho, ila unaamini kuwa kipo, au kiliwahi kuwepo au kitakuwepo baadae. Tofauti na hivyo hiyo sio imani ni uhalisia.

Sasa suala la uwepo au kutokuwepo kwa Mungu ni la kiiamani. Sio linalothibitishika kimaumbile katika hali ya kutumia milango ya fahamu. Ndio sababu katika kubishana kote nashangaa kwanini hamjauliza ROHO ni nini katika uhai wa binadamu?

Na je, BODY, MIND and SPIRIT vina uhusiano wowote katika uhai au afya ya mtu?

Kitu cha kujua ni kuwa, wewe kutoamini anachoamini mwingine hakufanyi kitu au imani hiyo kuwa ya uongo, ikiwa utadhani hivyo lazima uwe mpumbavu, maana, unawezaje kupinga kitu usichoamini wewe kwa kusema sio kweli? Hii ni sawa na kusikia watu wansongea lugha usiyoielewa kisha ukawaambia wanakosea, wakati lugha hiyo huielewi, utakuwa mzima wewe?

Asiyeamini uwepo wa Mungu atambue hiyo pia ni imani. Sio sayansi. Maana kama ni sayansi basi athibitishe kuwa hayupo. Na ili athibitishe lazima awe na majibu tayari (hypotheses) kuwa ili Mungu asiwepo inatakiwa iwe hivi au vile. Sasa unawezaje kutaka kuthibitisha kuwa kitu fulani hakipo wakati hujui ili kisiwepo inatakiwa kiweje?

Anayeamini Mungu yupo hiyo pia ni imani. Anaweza kuithibitisha kiimani hivyo hivyo ila kwa mtu mwingine anayemiani pia. Hawezi kuthibitisha kwa mtu asiyeamini maana hizo ni lugha mbili tofauti zisizotafsirika moja kwa nyingine.

Nakumbusha tu, kupinga imani usiyoiamini wewe ni upambavu. Mtu anayeamini mlima acha aamini mlima. Ndio imani yake. Ukija wewe kumwambia huo mlima sio kweli, yeye pia anaweza kukwambia huyo anayemuamini sio kweli.

Sayansi na imani ni vitu viwili tofauti. Kujaribu kuvifaya kimoja kithibitishe kingine ni zaidi ya upumbavu.
Mimi sibishani kuhusu imani. Najadili fact.

Imani kila mtu ana haki ya kuamini anavyotaka.

Imeruhusiwa kikatiba.

Kimataifa inatetewa na International Declaration of Human Rights tangu December 10 1948.

Kistaarabu si tabia nzuri kujibizana kuhusu imani.

Kiutamaduni wa kiungwana imani ni suala la faragha.

Lakini, mtu akileta habari za dini kwa mjadala wa kitafuta ukweli hapa, sijadili imani. Najadili fact.

Aliyeleta mjadala anakuwa kaondoa habari za faragha, huu ni ukumbi wazi wa jamii..

Najadili fact. Si imani.

Sijui kama unaeleea tofauti.
 
Sasa basi ungesema _'nina wivu na waarabu kwanini Wao na si wamatumbi'

Hapo ungeeleweka

Na wapo wengi tu humu wenye imani na kitabu chao wangekusaidia
Hujajibu niliyouliza.

Bujajibu contradiction inayoonesha mapengo katika ubongo wako yanayofanya fikra zako ziwe na kilema cha kudumu.
 
Ndio maana Kiranga nikimuuliza maswali yangu hajibu. Sasa kujadiliana na mtu mjinga asie jua chochote katika Qur'an ni kupoteza muda.

Angekuwa mtu wa kusoma mtu wa elimu,juzi kati hapa nilimuuliza swali hili :

Unajua kwanini Allah alie juu anawaziba watu masikio,macho na mioyo ? Ukweli hajui,badala ya kujibu swali nililo muuliza yeye alivyokuwa mtovu wa adabu za kielimu akawa anataka mimi nimjibu hilo swali,nikamwambia wazi silijibu swalo hilo kwa kujidai yeye mjuaji.

Nina uhakika Kiranga hajui hata kuisoma Qur'an bali nukuu zake zote anazitoa google,sasa watu wa elimu hawafanyi mambo kwa mtindo huo,watu wa elimu wanasoma hasa.

Mimi kazi yangu kwa Kiranga nimeimaliza,na hata hoja isipokuwa upuuzi mtupu.

Nataka akija tena aje na maswali yangu yote niliyomuuliza. Kisha tujadili mada mpya. Ila kwa maada hii kazi nimemaliza.
Wewe hata swali unalijua ni lipi na jibu ni lipi?

Utaanzaje kulijua hili swali na hili jibu kama unaamini Mungu mwenye contradiction?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom