Safina ya Nuhu

Los santos

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
961
2,037
daa nimeikuta sehem hili bandiko

Nina maswali machache juu ya hii safina naomba watu wajuzi wajibu..

Swali la kwanza ni kuhusu gharika. Hivi dunia nzima ilipewa taarifa juu ya ujio wa gharika?

Je, alioleta taarifa ya ujio wa gharika huku kijijini kwetu ni nani?

Je, Nuhu alizunguka dunia nzima kutia taarifa au aliishia maeneo yake tu na gharika ilitokea maeneo yake tu?

Swali lingine ni kuhusu wanyama na viumbe alio waweka nuhu kwenye safina, je aliwaweka wanyama wote has tunao waona duniani?

Je, aliwezaje kuwapata wanyama wanyama na viumbe hai wanao ishi sehemu tofauti tofauti hapa duniani?

Hivi aliwaweka wapi samaki wakubwa kama papa na nyangumi au kulikua na bwawa kwenye Safina ambalo aliweka samaki wa aina zote?

Je, Nuhu alichukua pia aina ya miti na nyasi zote duniani?

Nimekuuliza kwasababu kulingana na kitabu cha mkoloni mzungu (Biblia) inasema MWANZO 7:21-24 inasema kila kiumbe kilicho hao kwenye juu ya nchi kilikufa, hivyo hata mimea si ni viumbe hai pia na walio baki ni wa kwenye Safina tu?

Swali la mwisho ni kwamba ikiwa kila kiumbe kilicho nje ya Safina ya nuhu kilikufa je shetani alikua wapi wakati wa mafuriko?

Tunaambiwa kuwa shetani na mapepo wachafu wote tunaishi nao hapa duniani baada ya kufukuzwa huko mbinguni Sasa je walikua wapi wakati wa mafuriko na wao ni viumbe hai?

Je, nuhu ali waingiza kwenye Safina shetani na mapepo wachafu wakanusulika kifo ndomana wapo hai mpka leo?

Au shetani majini na mapepo walikufa lakini mungu aka waumba wengine na kutuletea tena?

Au shetani na majini na mapepo sio viumbe hai?

FB_IMG_1705910984968.jpg
 
duniani kinachokufa ni mwili na sio roho, mapepo na shetani ni roho hivyo hawawezi kufa kimwili kama viumbe wengine...
zama za Nuhu, dunia ilikua na watu wachache, na hawakua wamsambaa kama dunia ya leo, kwenye geografia kuna theory zinazosema dunia ya zaman mabara yote yalikua pamoja/karibu sio kama sasa.....
na zaidi vitabu vinasema alijenga safina kwa muda mrefu, miaka 40.... sasa kwa injili hyohyo kuhubiriwa miaka 40 mfululizo kuna uwezekano kila mtu alisikia neno, miaka 40 ni mingi, kwahyo kila mtu aliskia, na ukifatilia historia utaona mataifa yalianzia kwenye uzao wa Nuhu, kuna moja ya wanawe ndio baba wa wa africa na wengine maeneo mengine.
kuhusu samples za kila species ikiwemo mimea, Nuhu alikuwa anatekeleza magizo ya Mungu, wapo wanyama waliokuja wenyewe safinani vipo viumbe alivyopewa maelekezo jins ya kuvichukua.
 
daa nimeikuta sehem hili bandiko

Nina maswali machache juu ya hii safina naomba watu wajuzi wajibu..

Swali la kwanza ni kuhusu gharika. Hivi dunia nzima ilipewa taarifa juu ya ujio wa gharika?
Yes dunia nzima ilipewa na taarifa
Je, alioleta taarifa ya ujio wa gharika huku kijijini kwetu ni nani?
una uhakika kijiji chenu kilikuwepo?
Je, Nuhu alizunguka dunia nzima kutia taarifa au aliishia maeneo yake tu na gharika ilitokea maeneo yake tu?
dunia yote
Swali lingine ni kuhusu wanyama na viumbe alio waweka nuhu kwenye safina, je aliwaweka wanyama wote has tunao waona
Ndio. hakuwaweka yeye, alishangaa tu wameanza kuingia mdogomdogo
duniani?

Je, aliwezaje kuwapata wanyama wanyama na viumbe hai wanao ishi sehemu tofauti tofauti hapa duniani?
kwa uweza wa Mungu
Hivi aliwaweka wapi samaki wakubwa kama papa na nyangumi au kulikua na bwawa kwenye Safina ambalo aliweka samaki wa aina zote?
kwani Samaki na nyangumi wanaadhiriwa na maji
Je, Nuhu alichukua pia aina ya miti na nyasi zote duniani?
miti iliota baadae
Nimekuuliza kwasababu kulingana na kitabu cha mkoloni mzungu (Biblia) inasema MWANZO 7:21-24 inasema kila kiumbe kilicho hao kwenye juu ya nchi kilikufa, hivyo hata mimea si ni viumbe hai pia na walio baki ni wa kwenye Safina tu?

Swali la mwisho ni kwamba ikiwa kila kiumbe kilicho nje ya Safina ya nuhu kilikufa je shetani alikua wapi wakati wa mafuriko?
shetani ni liroho
Tunaambiwa kuwa shetani na mapepo wachafu wote tunaishi nao hapa duniani baada ya kufukuzwa huko mbinguni Sasa je walikua wapi wakati wa mafuriko na wao ni viumbe hai?

Je, nuhu ali waingiza kwenye Safina shetani na mapepo wachafu wakanusulika kifo ndomana wapo hai mpka leo?

Au shetani majini na mapepo walikufa lakini mungu aka waumba wengine na kutuletea tena?

Au shetani na majini na mapepo sio viumbe hai?

View attachment 2879378
una maswali ya kitoto sana na ya kijinga
 
Yes dunia nzima ilipewa na taarifa

una uhakika kijiji chenu kilikuwepo?

dunia yote

Ndio. hakuwaweka yeye, alishangaa tu wameanza kuingia mdogomdogo

kwa uweza wa Mungu

kwani Samaki na nyangumi wanaadhiriwa na maji

miti iliota baadae

shetani ni liroho

una maswali ya kitoto sana na ya kijinga
Hilo andiko nimelikuta sehem ,ila majibu yako umemjibu vizuri sana

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom