Makongoro amfungia safari Leticia Nyerere


Mama Zuma aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini enzi ya Mbeki anaendelea kutumia jina la mumewe ingawa waliachana miongo mingi tu iliyopita!! Huo ni utamaduni wa kiafrika mara mwanamke anapokuwa na watoto na mume wake walioachana!! Makongolo kwahilo kafulia!!
 
Huyu mtu kapata wapi huo ujasiri wa kumuamulia mtu mzima mwingine jina la kutumia wakati ni jina halali? Yaani imepita miaka kumi na mbili ndio anakumbuka kuwa Leticia bado anatumia jina la Nyerere? Na watoto wa Leticia wanaruhusiwa kutumia jina la "babu yao maarufu"?
 




Namfahamu vizuri Makongoro, sekondari alichapwa viboko alipo jibu swali la nani rais wa Tanzania naye akajibu "Babangu" Wakina nyerere mbona wapo kila mahali Tanzania???????????? Umaarufu wa Baba wa taifa mbona ulileta wa kina nyerere nchi nzima??? kwa mila nyingi za kiafrica watu wengi huweka kumbukumbu zao kutokana na jambo kuu (remarkable ) lilokuwapo kipindi hicho, Leo tangu nyerere kutawazwa ni miaka karibu 50 je ? walioitwa wakina Nyerere leo hawana watoto wenye ubin wa jina hilo????!! je sheria inawazuia kutumia jina??????? ACHENI HIZO.
 
Huyu naye aache kuchemka.

Mbona Tina Turner anatumia jina la Mumwe hadi leo na walishaachana zamani saana na mumewe kufariki.

Mbona Vivian Ndour anatumia jina la NDOUR ingawa walishaachana na mdogo wake Youssour Ndour?

Mifano ipo mingi saaana.

Hapa nawawekea kibao alichotesa watu roho akiwa na Phillip Monteiro:

Chini mwenye nguvu anaweza kuangalia wakati Bibie akiimba kwa jina la Viviane Chidid yaani hapo alikuwa hata bado hajaolewa. Ila pamoja na kuachana, waweza kuona Clip walizoimba pamoja tena na Youssour Ndour na hii imefanya watu wengi wafikiri ni mtu na dada yake wakati ukweli ni kuwa ni mtu na Ex-Shemeji yake. Youssour alikuwa bado Yanki ile mbaaaya yake.

YouTube - Youssou Ndour & Viviane Chidid Seven Second Live
 
Last edited by a moderator:
Hapa makongoro kanoa step; kama ni kweli mama huyu alikuwa ameolewa na mtoto wa Nyerere na katika kipindi cha ndoa yao akawa amebadili jina na kuitwa Leticia Nyerere. bado ana haki ya kutumia jina hilo hata kama wameshatalikiana lasbda kama yeye mwenyewe atataka kubadili tena. Ndiyo maana hata mama yake mzazi Maria Nyerere anaendelea kuitwa hivyo ingawa kwa sasa hivi siyo mke wa Nyerere tena

Kosa ni kama ataendelea kujitambulisha kama mke wa Madaraka, ila kama anajitambulisha kama mtariki wa Madaraka ni haki kabisa.
 
Ex-husband wa Leticia, Madaraka, HAJALALAMIKA. Nini kiherehere cha Makongoro? Mzee, kama umeishiwa hoja, kaa kimya! Angerudi Mwalimu angekuchapa bakora hapo ulipo!
 
Mbona Mama Maria anaitwa Maria Nyerere wakati Ndoa yake na Nyerere haipo tena ( Tena Imetenganishwa na Mungu). Graca Machel pamoja na kuolewa na mandela lakini bado anaendelea kutumia jina hilo hilo! Hapa Mkulu makongoro kweli umetokota
 
Huyu aliwahi kukimbia kulipa bili ya bia pale Fourways ya zamani kule masaki....tukamlipia kwa heshima ya babaye na kwa kuwa alikuwa Anakunywa SAFARI...

Ka vile ulikuwa unanisoma. Na kwa kupenda bia za bure huyooooooooo! basi zake ni pale kaunta. Njaa kali wako wengi huko CCM.
 
Makongoro akimpinga huyu Leticia,that is just as it should be,kwa sababu huyu ni mpinzani wake wa kisiasa. Isipokuwa, as far as the Nyerere Family is concerned,mimi napinga hili jambo. Kama Leticia anataka kuwa Mbunge,wa wapi kule,Serengeti?,sisi,Familia ya Nyerere hatuwezi kuwa na sababu ya kupinga au kusema kwamba akichaguliwa itakuwa ni jambo baya kwetu. Yuko mtu mmoja nilisema kuchaguliwa kwake hakuwezi kuifurahisha Familia ya Nyerere. Na huyo mtu hakuwa Leticia. Huyo mtu sasa hivi siwezi kumtaja sasa ,kwa sababu conditions zimekuwa difficult.
No,hata kama timu ya mpira,kwa mfano Young Africans,wakimfukuza mchezaji. Yule mchezaji akiondoka Yanga akienda kwenye timu ya Simba,sidhani kama Yanga watasema,''Msimuajiri huyo.''
Kwa hiyo sisi Familia ya Nyerere hatupingi Leticia kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Serengeti. In fact,sisi Familia ya Nyerere,ni lazima,lazima,lazima tuwe non-partisan,tuwe watu ambao hatujali nani anachaguliwa Rais,nani anachaguliwa Mbunge au nani anachaguliwa diwani.
Again,nasema sipingi Makongoro kumpinga Leticia. In fact,namuunga mkono Makongoro kumpinga Leticia,lakini kama Familia,wa are non-partisan.
 
Huyu Makongoro kweli kichaa mimi sikutaka kuamini siku zote toka zamani tukikutana. Yaani hii inaonyesha wazi jinsi mtu huyu anavyowatazama wanawake kama chombo cha kutumiwa na kubwagwa anapotaka. Yeye nani kuamua nani anatakiwa kutumia jina la Nyerere na nani hatakiwi?.. Hata kama hakuolewa na Madaraka bado mtu yeyote anaweza badilisha jina lake na kujiita Nyerere maadam amepitia sheria za kubadilisha jina acha mbali huyu mke alozaa watoto wenye kutumia jina la Nyerere kama babu yao.

Ukisha oa na mke akachukua ubini wa jina lako hapo kisheria tayari ni jina lake yeye mhusika ambaye pekee ndiye anaweza kuamua kutolitua tena..
 

Mkuu Mbona unajichanganya katika maneno yako?
 
Tena kwa mila na desturi za KIZANAKI ndoa huwa hazivunjiki. Kama Leticia kaendelea kuzaa hata baada ya kutengana na Madaraka watoto ni wa Madaraka!

Kuna madai kutoka baadhi ya Wazanaki wanaoijua familia kwamba hata Nyerere mwenyewe si mtoto wa Chifu Burito Nyerere, alipata "uNyerere" kwa style hiyo hiyo, baada ya mama yake kutoka kwa Chifu Burito, lakini kwa mujibu wa mila hii ikabidi aukwae uNyerere tu. Hamna mwanahistoria anayeweza kuchunguza hili Tanzania.

Funny things. Bitter politics. Family dirty laundry tossed open in the air for political expediency.

Haya ndiyo matokeo ya kuwafanya watu waamini kwamba jina la Nyerere lina upako fulani wa kitakatifu.

Watu wameona Nyenyere, nini Nyerere.
 
Siasa za Tanzania hizo.
Nyerere ana Makongoro
Mwinyi ana Hussein
Malima ana Adam
Kikwete ana Riz One
Makamba ana January

All are rubbish

Mhe. Mmakonde,

Umesahau kwamba Kawawa ana Vita
Nnauye ana Nape
Sijaona ana,???......jazia hapo
 

Wakina mama wa tz mko wapi katika hili? wanawake mlio wanaharakati bila kujali vyama vyenu hamuoni huu ni unyanyashaji wa kijinsia? hamuoni kuwa anatengeneza mkakati wa kuwadhalilisha kwa kutumia majina ya waume zenu. Huyu makongoro ana bahati sana amelisema hili akiwa tz ambako wanasisiem hawaguswi kwa maovu wanayowafanyia wananchi wengine!! vinginevyo kama angekuwa yuko afrika ya kusini ,angepigwa mbooko hadharani na kutobolewa macho!!!!
 
FROIDA nikusahihishe kidogo aliyechakachuliwa akili ni Makongoro na si Madaraka kama ulivyoeleza, Madaraka mwenye mke yupo kimya wala ajazungumzia mkewe kugombea ubunge wala kutumia jina la Nyerere hila vuvuzela Makongoro ndio yupo hewani. Wala haelewi kumdhalilisha shemejie ni kuzalilisha watoto wao na nduguye Madaraka. Kweli njaa mbaya na kufulia usiombe Makongoro unadai hadi jina.
 
Katika ukoo wa Nyerere wapo watu wengi mno lakini aliyelibeba jina ni Julius Kambarage Nyerere na kwa mbali mdogo wake Joseph Nyerere lakini tukumbuke hata jina la JULIUS sio la kizanaki bali mwalimu alilichagua wakati anabatizwa. Je waje wenye asili ya jina la Julius walidai maana sio la kiafrika? Pili Makongoro wakati akiwa mbunge wa Arusha Mjini kupitia NCCR MAGEUZI kuna mwanaCCM mashuhuri hivi aliwahi kusema Makongoro sio mtoto wa mwalimu kutokana na mambo yake na kuasi chama, Mwanasiasa huyo alishambuliwa sana ili kulinda heshima ya mama Maria kuwa hana mtoto wa nje ya ndoa, pamoja na matusi na udhalilishwaji huo kichwa maji huyo wa mwalimu akarudi CCM, baada ya wakina MKONO NIMROD kumuhakikishia kumpatia uenyekiti wa CCM mkoa. Makongoro inabidi aelewe kuwa NYERERE ni jina kama MADENGE, NIPASHE, KOMBA, NGURUWE, MCHAMBAWIMA nk. Jina NYERERE limepata umaarufu sababu ya JULIUS KAMBARAGE kuwa kiongozi muadilifu na mfano hadi waTZ tukakubali kumuita baba wa TAIFA. Lakini akumbuke waafrika wanautamaduni wa kuenzi viongozi wanao wapenda kwa kuwapa watoto wao majina ya viongozi hao mf kuna watanzania wengi wanaitwa SAMORA , MANDELA, MUGABE, OSAMA nk. Kimsingi wenye majina hayo wala hawana nasaba na koo husika. hivyo jina ni jina tu. mtu anaweza kuitwa FISI na bado akawa kiongozi mzuri kuliko mtu anayeitwa NYERERE mfano mzuri ni wewe mwenyewe Makongoro ulichemsha katika ubunge Arusha japokuwa ulitumia jina la NYERERE. Wanachi watamchagua au kumkataa LETICIA kwa kupitia sera za chama chake na uwezo wake nasi kwa jina la NYERERE. kama jina la NYERERE ni mtaji basi wewe gombea urais 2015 uone kama utashinda? Tena kumbuka kuweka majina yote muhimu MAKONGORO JULIUS KAMBARAGE BURITO NYERERE wa KIJIJI CHA BUTIHAMA mtoto wa MARIA NYERERE.Acha mambo ya kizamani yakila mtu kujidai anatoka ukoo wa kichifu, au kila baba yeye alikuwa wa kwanza darasani, kumbuka umaarufu wa ukoo wa NYERERE unabebwa na JULIUS KAMBARAGE na si kila mwana Ukoo. Akili, BUSARA na uadilifu ni wa JULIUS KAMBARAGE nasi wakila mwana Ukoo wa Nyerere mbona wewe dk tano mbele na bado ni Nyerere tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…