Hapa tukubali rafiki yangu Makongoro kachemsha. Hata nitakapoongea naye nitamwambia hivyo hivyo. Dalili ninayoiona hapa ni kwamba CCM hawataki kukumbushwa jina la Nyerere kwa sababu hata katika ilani zao hawamkumbuki huyu mwanzilishi wa taifa letu. Sasa inawastua kuwa Leticia, aliyekuwa mkwe wa Nyerere, ambaye amemzalia wajukuu, anaendelea kuwakumbusha watu kuwa Nyerere alikuwepo na hii inawashtua sana CCM. Hakuna mahali Dr Slaa katumia jina la Nyerere au Leticia kujipatia umaarufu lakini naona mgombea wa CCM hajiamini kiasi cha kuomba msaada kutoka mwenyekiti wa CCM wa Musoma ambaye hagombei kiti chochote katika jimbo la Kwimba.