njiwa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 12,360
- 5,473
Na wewe una una nani?Siasa za Tanzania hizo.
Nyerere ana Makongoro
Mwinyi ana Hussein
Malima ana Adam
Kikwete ana Riz One
Makamba ana January
All are rubbish
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na wewe una una nani?Siasa za Tanzania hizo.
Nyerere ana Makongoro
Mwinyi ana Hussein
Malima ana Adam
Kikwete ana Riz One
Makamba ana January
All are rubbish
Madaraka amechakachuliwa akili yake mke wa ndugu yake aliyezaa naye watoto wa tatu anaenda kumnyanyasa kijinsia kwa aina hiyo mbele ya Umma ,anadhani watoto wa ndugu yake watakuwa na heshima naye kweli mtu anaenda kumdhalilisha mama yao mbele ya jamii kwa kuendelea kutumia jina mpaka leo,huu ni utamaduni uliobaki kwa wanawake wengi wa Tanzania ambao waliolewa na wakaachika na waume zao lakini pindi wakiwa wamezaa na hao wanaume wameendelea kutumia majina ya waume zao kwa sababu nyingi tu zikiwemo nyaraka za kikazi,passport na hata elimu huw wanaona taabu tena kwenda mahakamani kuapa na kuanza kugeuza kila kitu.
Kuna wengine maarufu hapa Afrika ambao bado wanatumia majina ya waume zao akiwemo Winnie Mandela na Graca Machelle ambaye ni rafiki wa familia ya Nyerere kwa hiyo Madaraka asimnyanyase huyo mama kisaikolojia na sidhani wananchi watamsikiliza kwa huo ujinga wake.
MWENYEKTI wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, amemtupia madongo mgombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, kupitia tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere, kuwa anatumia jina la Nyerere ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Makongoro pia amemtaka Leticia kuacha mara moja, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika harakati zake za kisiasa kwa kuzingatia kuwa ndoa kati yake na Madaraka Gedfrey Nyerere haipo tena.
Mwenyekiti huyo wa CCM na Madaraka ni watoto wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Leticia anagombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, akichuana na Shanif Hirani Mansoor, anayewania kwa tiketi ya CCM.
Hatua ya Makongoro kumtaka Leticia aache kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika shughuli za kisiasa, aliifanya juzi alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CCM, katika Jimbo la Kwimba.
Kampeni hizo zilizinduliwa katika mji mdogo wa Hungumalwa, wilayani Kwimba.
Katika uzinduzi huo, Makongoro alielezea kushangazwa kwake juu ya hatua ya viongozi wa Chadema na Leticia, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika kujinadi kwa wapiga kura.
Alisema hata hivyo kitendo hicho kinacholenga katika kumwezesha mgombea huyo wa Chadema kuchaguliwa, hakitasaidia hata kidogo kushinda katika uchaguzi huo.
Alisisitiza kuwa ni makosa kwa mgombea huyo kutumia jina la ukoo wa Nyerere kujinadi, hasa ikizingatiwa kuwa ndoa baina yake na mdogo wake (Madaraka) haipo tena.
Kwa mujibu wa Makongoro, wanandoa hao walitengana miaka 12 iliyopita baada ya kutofautiana.
"Huyu anayejiita Leticia Nyerere hasemeshani na Madaraka, achilia mbali hata kusalimiana, sasa anatumiaji jina la ukoo wetu. Angalau mimi naweza kuzungumza naye, ni kweli alikuwa mke wa mdogo wangu na alibahatika kuzaa naye watoto watatu lakini mambo ya ndoa wengi mnayajua, sasa siyo mke wake tena," alifafanua.
Alisema ingawa hataki kuingia kwa undani kuzungumzia mgogoro kuhusu ndoa hiyo, alisema yeye na mkewe Jaji Aisha Nyerere, ndio walikuwa wasimamizi.
Alisema katika ndoa hiyo, hayati Mwalimu Nyerere, alitoa ng'ombe 30.
"Huo ni uongo, ninawaomba wananchi wa Jimbo la Kwimba muuachana naye na kumchagua mgombea wa CCM Shanif Mansoor," alieleza makongoro Nyerere.
Makongoro alidai kuwa wakati wa harusi, yeye alikuwa ofisa wa jeshi na mke wake alikuwa hakimu.
Pia alisema mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, amekuwa akimtumia Leticia kama mtaji wa kisiasa katika kuomba kura.
Katika hotuba yake, Makongoro pia alisema Dk Slaa naye anapoteza muda mwingi kuzungumzia ufisadi, wakati jambo hilo limeshashughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Nne.
Alisema serikali imeshughulikia jambo hilo, kwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa.
"Ufisadi ni sawa na kibaka, fisadi anaweza kuwa upande wowote, mbona hata kwao wana mafisadi kibao,ufisadi ni tabia ya mtu,CCM iko safi na ndio maana tumekuwa tukiendesha kampeni zetu kwa ustaarabu bila kutumia matusi. Wnanchi msidanganywe na hoja ya ufisadi mwacheni Dk Slaa aendelee kupiga kelele kuhusu ufisadi,",alisema.
Kwa upande wake, Mansoor alisema akichaguliwa kuwa mbunge, atamaliza matatizo ya maji, huduma za afya na upungufu wa walimu katika shule za jimbo hilo.
Huyu aliwahi kukimbia kulipa bili ya bia pale Fourways ya zamani kule masaki....tukamlipia kwa heshima ya babaye na kwa kuwa alikuwa Anakunywa SAFARI...
Makongoro akimpinga huyu Leticia,that is just as it should be,kwa sababu huyu ni mpinzani wake wa kisiasa. Isipokuwa, as far as the Nyerere Family is concerned,mimi napinga hili jambo. Kama Leticia anataka kuwa Mbunge,wa wapi kule,Serengeti?,sisi,Familia ya Nyerere hatuwezi kuwa na sababu ya kupinga au kusema kwamba akichaguliwa itakuwa ni jambo baya kwetu. Yuko mtu mmoja nilisema kuchaguliwa kwake hakuwezi kuifurahisha Familia ya Nyerere. Na huyo mtu hakuwa Leticia. Huyo mtu sasa hivi siwezi kumtaja sasa ,kwa sababu conditions zimekuwa difficult.
No,hata kama timu ya mpira,kwa mfano Young Africans,wakimfukuza mchezaji. Yule mchezaji akiondoka Yanga akienda kwenye timu ya Simba,sidhani kama Yanga watasema,''Msimuajiri huyo.''
Kwa hiyo sisi Familia ya Nyerere hatupingi Leticia kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Serengeti. In fact,sisi Familia ya Nyerere,ni lazima,lazima,lazima tuwe non-partisan,tuwe watu ambao hatujali nani anachaguliwa Rais,nani anachaguliwa Mbunge au nani anachaguliwa diwani.
Again,nasema sipingi Makongoro kumpinga Leticia. In fact,namuunga mkono Makongoro kumpinga Leticia,lakini kama Familia,wa are non-partisan.
Tena kwa mila na desturi za KIZANAKI ndoa huwa hazivunjiki. Kama Leticia kaendelea kuzaa hata baada ya kutengana na Madaraka watoto ni wa Madaraka!
Unyerere huu wana taabu sana!Mkuu Mbona unajichanganya katika maneno yako?
Siasa za Tanzania hizo.
Nyerere ana Makongoro
Mwinyi ana Hussein
Malima ana Adam
Kikwete ana Riz One
Makamba ana January
All are rubbish
Yaliyofanywa na Makongoro ni unyanyasaji mkubwa kijinsia. Leticia anazo haki zote za kutumia jina la Nyerere kwa sababu alifunga ndoa takatifu katika kanisa Katoliki. Kuingiza mambo ya ndoa ya mtu kwenye mambo ya siasa ni dalili za kufilisika. Mwacheni Leticia ahukumiwe na achaguliwe na wananchi kwa uwezo wake binafsi. Naamini kabisa Mzee Kambarage Nyerere angelikuwa hai wala Makongoro asingethubutu kunyanyua mguu wake kwenda kumchafua shemejiye. Makongoro amejiaibisha sana!
FROIDA nikusahihishe kidogo aliyechakachuliwa akili ni Makongoro na si Madaraka kama ulivyoeleza, Madaraka mwenye mke yupo kimya wala ajazungumzia mkewe kugombea ubunge wala kutumia jina la Nyerere hila vuvuzela Makongoro ndio yupo hewani. Wala haelewi kumdhalilisha shemejie ni kuzalilisha watoto wao na nduguye Madaraka. Kweli njaa mbaya na kufulia usiombe Makongoro unadai hadi jina.Madaraka amechakachuliwa akili yake mke wa ndugu yake aliyezaa naye watoto wa tatu anaenda kumnyanyasa kijinsia kwa aina hiyo mbele ya Umma ,anadhani watoto wa ndugu yake watakuwa na heshima naye kweli mtu anaenda kumdhalilisha mama yao mbele ya jamii kwa kuendelea kutumia jina mpaka leo,huu ni utamaduni uliobaki kwa wanawake wengi wa Tanzania ambao waliolewa na wakaachika na waume zao lakini pindi wakiwa wamezaa na hao wanaume wameendelea kutumia majina ya waume zao kwa sababu nyingi tu zikiwemo nyaraka za kikazi,passport na hata elimu huw wanaona taabu tena kwenda mahakamani kuapa na kuanza kugeuza kila kitu.
Kuna wengine maarufu hapa Afrika ambao bado wanatumia majina ya waume zao akiwemo Winnie Mandela na Graca Machelle ambaye ni rafiki wa familia ya Nyerere kwa hiyo Madaraka asimnyanyase huyo mama kisaikolojia na sidhani wananchi watamsikiliza kwa huo ujinga wake.