Makongoro amfungia safari Leticia Nyerere | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makongoro amfungia safari Leticia Nyerere

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bujibuji, Sep 17, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,399
  Trophy Points: 280
  MWENYEKTI wa CCM mkoani Mara, Makongoro Nyerere, amemtupia madongo mgombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, kupitia tiketi ya Chadema, Leticia Nyerere, kuwa anatumia jina la Nyerere ili kujipatia umaarufu wa kisiasa.
  Makongoro pia amemtaka Leticia kuacha mara moja, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika harakati zake za kisiasa kwa kuzingatia kuwa ndoa kati yake na Madaraka Gedfrey Nyerere haipo tena.

  Mwenyekiti huyo wa CCM na Madaraka ni watoto wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

  Leticia anagombea ubunge wa Jimbo la Kwimba, akichuana na Shanif Hirani Mansoor, anayewania kwa tiketi ya CCM.

  Hatua ya Makongoro kumtaka Leticia aache kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika shughuli za kisiasa, aliifanya juzi alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za CCM, katika Jimbo la Kwimba.

  Kampeni hizo zilizinduliwa katika mji mdogo wa Hungumalwa, wilayani Kwimba.

  Katika uzinduzi huo, Makongoro alielezea kushangazwa kwake juu ya hatua ya viongozi wa Chadema na Leticia, kutumia jina la ukoo wa Nyerere katika kujinadi kwa wapiga kura.

  Alisema hata hivyo kitendo hicho kinacholenga katika kumwezesha mgombea huyo wa Chadema kuchaguliwa, hakitasaidia hata kidogo kushinda katika uchaguzi huo.

  Alisisitiza kuwa ni makosa kwa mgombea huyo kutumia jina la ukoo wa Nyerere kujinadi, hasa ikizingatiwa kuwa ndoa baina yake na mdogo wake (Madaraka) haipo tena.

  Kwa mujibu wa Makongoro, wanandoa hao walitengana miaka 12 iliyopita baada ya kutofautiana.

  "Huyu anayejiita Leticia Nyerere hasemeshani na Madaraka, achilia mbali hata kusalimiana, sasa anatumiaji jina la ukoo wetu. Angalau mimi naweza kuzungumza naye, ni kweli alikuwa mke wa mdogo wangu na alibahatika kuzaa naye watoto watatu lakini mambo ya ndoa wengi mnayajua, sasa siyo mke wake tena," alifafanua.

  Alisema ingawa hataki kuingia kwa undani kuzungumzia mgogoro kuhusu ndoa hiyo, alisema yeye na mkewe Jaji Aisha Nyerere, ndio walikuwa wasimamizi.

  Alisema katika ndoa hiyo, hayati Mwalimu Nyerere, alitoa ng'ombe 30.

  "Huo ni uongo, ninawaomba wananchi wa Jimbo la Kwimba muuachana naye na kumchagua mgombea wa CCM Shanif Mansoor," alieleza makongoro Nyerere.

  Makongoro alidai kuwa wakati wa harusi, yeye alikuwa ofisa wa jeshi na mke wake alikuwa hakimu.

  Pia alisema mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, amekuwa akimtumia Leticia kama mtaji wa kisiasa katika kuomba kura.

  Katika hotuba yake, Makongoro pia alisema Dk Slaa naye anapoteza muda mwingi kuzungumzia ufisadi, wakati jambo hilo limeshashughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Nne.

  Alisema serikali imeshughulikia jambo hilo, kwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa.

  "Ufisadi ni sawa na kibaka, fisadi anaweza kuwa upande wowote, mbona hata kwao wana mafisadi kibao,ufisadi ni tabia ya mtu,CCM iko safi na ndio maana tumekuwa tukiendesha kampeni zetu kwa ustaarabu bila kutumia matusi. Wnanchi msidanganywe na hoja ya ufisadi mwacheni Dk Slaa aendelee kupiga kelele kuhusu ufisadi,",alisema.

  Kwa upande wake, Mansoor alisema akichaguliwa kuwa mbunge, atamaliza matatizo ya maji, huduma za afya na upungufu wa walimu katika shule za jimbo hilo.
   
 2. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu ni yule Makongoro aliyewahi kuwa mbunge kwa tiketi ya NCCR_mageuzi au siye??
  Kweli siasa inabidi uwe mnafiki kuongea mambo ambayo hata moyo wako unakiri ni uongo.
  Kwani si wametengana tu au wameachana?? kweli viongozi wa CCM ni balaa wao ni kumwaga upupu tu. Makongoro aende mahakamani kama hataki shemejie atumie jina hilo.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Tuliambiwa kwenye uchaguzi huu tutasikia mengi hewallah tunasikia sasa teh! teh! teh! teh!
   
 4. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Siasa za Tanzania hizo.
  Nyerere ana Makongoro
  Mwinyi ana Hussein
  Malima ana Adam
  Kikwete ana Riz One
  Makamba ana January

  All are rubbish
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tena kwa mila na desturi za KIZANAKI ndoa huwa hazivunjiki. Kama Leticia kaendelea kuzaa hata baada ya kutengana na Madaraka watoto ni wa Madaraka!
   
 6. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wee Makongoro mbona mwenye mke (Madaraka) kaa kimya halalalamika wewe kinachokuwasha nini ama ndio watafuta ukuu wa Mkoa!!
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,482
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Huyu aliwahi kukimbia kulipa bili ya bia pale Fourways ya zamani kule masaki....tukamlipia kwa heshima ya babaye na kwa kuwa alikuwa Anakunywa SAFARI...
   
 8. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  mpuuzi tu huyo kwani ana hati miliki ya Jina? Hata baba yake alishasema ccm siyo mama wala baba yake. Hivi leticia Nyerer angegombea kupitia ccm makaongoro angemwinukia kuwa anatumia jina lao kimakosa?
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Makongoro hana maana hata kidogo.WanaCCM Mara watakuwa vichaa kukubali kuongozwa na mhuni.Nakumbuka Mwl Nyerere mwaka 1995 alituita wapiga kura wa Arusha wahuni kwa kumchagua Makongoro mbunge wa Arusha mjini naanza kuamini Nyerere alikuwa sahihi kabisa.
   
 10. Beauty

  Beauty JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 540
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hapo sasa!
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,450
  Likes Received: 22,399
  Trophy Points: 280
  Makongoro, wakirudiana utaweka wapi sura yako?
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,983
  Likes Received: 690
  Trophy Points: 280
  Yale yale.CCM na siasa za ndani ya magauni na ndani ya suriali za watu!!
  BSH*T
   
 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,983
  Likes Received: 690
  Trophy Points: 280
  Kwanza unaweza kuta wanaendelea kuchakachuana......ila wamekubaliana kuwa kuishi pamoja hatuwezi!
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,482
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Shuka kwa Shuka......jamaa naingia mpaka kwenye shuka ya shemeji....hizi sera hizi
   
 15. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Achaneni na mlevi kwani kisha shikishwa kitu kidogo na CCM sasa analopoka hovyo, hata hivyo tunaomjua si jambo geni kwani hata Mama Maria naye anatia wasiwasi wa kushikishwa kitu kidogo kwani yupo karibu sana sana na upande wa mafisadi wanaojulikana
   
 16. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,511
  Likes Received: 1,232
  Trophy Points: 280
  sheria za mkoa wa mara katika ndoa huwa hakuna talaka hata kama mwanamke akizaa nje ya ndoa watoto wanatambulika kuwa ni wa mume aliyetoa mahari, kama makongoro anaona ni kero aende kortini kudai jina la baba yake
   
 17. p

  pierre JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Atuambie kwanza kilichomshinda Arusha kipindi kile na alivyokuwa akitueleza kuwa amekulia ikulu anajua uhuni wote wa CCM leo anawakumbatia.Kweli pesa .........................
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kile kiti alipewa na Nimrod Mkono. Anaishi na kupumua kisiasa kwa hisani ya fisadi Mkono.
   
 19. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2010
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  nyerere kama jina wala halina umaarufu, hata wewe makongoro nyerere ni hovyohovyo tuuuuuuuuuuu

  sisi tunamheshimu hayati julius nyerere.
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Madaraka amechakachuliwa akili yake mke wa ndugu yake aliyezaa naye watoto wa tatu anaenda kumnyanyasa kijinsia kwa aina hiyo mbele ya Umma ,anadhani watoto wa ndugu yake watakuwa na heshima naye kweli mtu anaenda kumdhalilisha mama yao mbele ya jamii kwa kuendelea kutumia jina mpaka leo,huu ni utamaduni uliobaki kwa wanawake wengi wa Tanzania ambao waliolewa na wakaachika na waume zao lakini pindi wakiwa wamezaa na hao wanaume wameendelea kutumia majina ya waume zao kwa sababu nyingi tu zikiwemo nyaraka za kikazi,passport na hata elimu huw wanaona taabu tena kwenda mahakamani kuapa na kuanza kugeuza kila kitu.
  Kuna wengine maarufu hapa Afrika ambao bado wanatumia majina ya waume zao akiwemo Winnie Mandela na Graca Machelle ambaye ni rafiki wa familia ya Nyerere kwa hiyo Madaraka asimnyanyase huyo mama kisaikolojia na sidhani wananchi watamsikiliza kwa huo ujinga wake.
   
Loading...