Makonda: Mashoga wanataka kuniangamiza

Makonda: Mashoga wanataka kuniangamiza

sasa kama alibaini mashoga zaidi ya 150 walikaa kikao kwanini asiende kuwakamata??hii nchi inamatatizo mengi sana aachane na hiyo ya mashoga
haya ni maajabu 150 yeye anakamata nane tu hapo si lazima wajidai, na katika wale kama hayupo KAOGE au Kademu shoga wa Musoma shoga la kisukuma basi hapo hakuna intelegensia
 
Apambane na umasiki unaogusa kila jamii nchini... hizo issue za mtu mmoja mmoja aachane nazo. Ingawa siusapoti ushenzi huo ila angeachana nao tu. Ni sawa na kufatilia issue za madawa ya kulevya!
 
Anatafuta kiki tuu huyu hana lolote, akasafishe mitaro ya jiji sio kuleta vita vya kutupotezea muda
 
Jamaa anapambana na kivuli cha mashoga,siku akiwatekenya utasikia Tanzania kuna magaidi,hakuna utawala wa sheria na haki za binadamu....itaambatana na vikwazo vya kiuchumi,mkiwa wabishi mnaundiwa zengwe mnapigwa.Hii vita ni kubwa mno Makonda sio saizi yake.
 
Mh. Makonda pambana na hawa mashoga na machangudoa tafadhali sana. Ni lazima tujenge jamii inayojiheshimu kwa mila na desturi. Hasa hasa hawa mashoga ni aibu sana kwa taifa letu. Kama wanataka wahame nchi waende kwa akina Cameroon na Obama.
 
Tunahawa vijana mkoani kwako wanahangaika kutafuta ajira....tafuta mpango tuone unawaokoa wawe wajarisilimali wajenge nchi.

Hawa hawapo mechi ya mpira..wako interview kuomba nafsi 20 za immigration
Hebu tuoneshe ubunifu kidogo....mimi nikiwa hio nafasi yako ndani ya miezi sita hili jeshi lisilo kazi nalipa nyenzo na litajiajiri....

ImageUploadedByJamiiForums1469201676.224311.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1469201695.589757.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1469201706.393066.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1469201718.323180.jpg
 
..mashoga ni hatari..maana hayana aibu kabisa....usiombe shoga lipate namba yako ya simu....yanasumbua ile mbaya....sasa kama yameanza vita na makonda basi kazi anayo...maana yanawashwa ile mbaya.....duniani kote vita na mashoga imekwama....kwingine yameruhusiwa hata kuoana...
 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema tangu alipotangaza kuanza kukamatwa kwa mashoga, amebaini kuna mkakati unawaohusisha watu hao zaidi ya 150 kutaka kumwangamiza.

Kauli hiyo aliitoa jana Dar es Salaam baada ya kumaliza mahojiano katika kituo cha redio Clouds FM, ambako alikuwa akifafanua hoja na changamoto mbalimbali za mkoa wake.

Alisema kuwa baada ya kubainika kwa mipango hiyo, mashoga wanane wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi.

“Lazima watu wajue jitihada na harakati za kusimamia katiba na usawa hapa nchini. Hakuna anayezipenda, vita inakuwa kubwa… Nimebaini kuwa mashoga zaidi ya 150 waliketi katika baa moja Kinondoni wakipanga njama za kunimaliza kwa namna moja ama nyingine, lakini kutokana na taarifa za kiintelijensia, watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni mashoga wameshakamatwa,” alisema Makonda.

Katika hatua nyingine, Makonda aliwatolea uvivu watu wanaosambaza ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii, ikiwamo kutengeneza akaunti feki.

“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina akaunti ambayo inaanza na cheo changu, hivyo akaunti zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda si vinginevyo, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo,” alisema Makonda.

Aliweka wazi kuwa kuna agizo batili lililowekwa katika mitandao ya kijamii, akidaiwa kusema kuwa watu wasiokuwa na kazi watakwenda jela, lakini ukweli ni kwamba ameagiza wenyeviti wa Serikali za mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa maeneo wanayoishi.

Aidha Makonda alisisitiza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo, kamwe Hatoacha kupambana na mafisadi katika halmashauri zote tatu za mkoa wake, pamoja na wauza unga, wafanyabiashara wa shisha na mashoga.

Chanzo: Mpekuzi


===========

My take:

Sema chochote kwa Mkuu wa Mkoa

Kwa hii tabia yake ya " kupayuka payuka " hovyo na kuwa kama " mswahili " nadhani kabakiza tu 5% za kuheshimika na wanaojitambua na 95% zote zilizobaki anaonekana " kituko ". Binafsi AMENISIKITISHA mno kwani badala ya kufanya Kazi Dar iende yeye kutwa tu ni kuzunguka zunguka katika Media ambazo sasa zimeshamfanya yeye ni MTAJI wao na kile akisemacho ( PERSONALITY + CONTENT MARKETABILITY ). Kuna kitu fulani sasa very technical ambacho Media hiyo anayoipenda inakitumia dhidi yake ila siwezi nikakisema hapa kwani nitaharibu " ulaji " wa Watu.

Wanachokifanya ni KUTEKENYA huku kisha WANAMJAZA " Jamaa " na yeye bila kujua kuwa " anajazwa " anaingia katika mtego wao na WANAMUME wanapiga madili yao. Siku atakayokuja kushtuka atagundua kuwa kapoteza muda wake mwingi sana na nimalizie tu kwa kumshauri atafute haraka COMMUNICATION STRATEGIST hapo Ofisini kwake ili aweze kusawazisha haya mambo mengine otherwise kwa hii trend anayokwenda nayo niseme tu kuwa ANAPOTEA vibaya sana.
 
Hii vita ilisha wasumbua watu wengi....kwa kifupi.....
1.Bondia maarufu duniani manny pacquiao...
2.Muimbaji maarufu wa reggae Alpha Blondy
Unajua kwa nini haya yanatokea...Sababu kubwa hawa mashoga nyuma yao kuna watu wakubwa ...Hebu fikiri mwanamuziki Elton John ni shoga lakini malkia wa Uingereza alimpa heshima ya Knight Bachelor...na kuwa Sir Elton John....Hivyo basi RC kupambana na watu kama hawa ni dhahiri anapambana na watu asiowajua.
Kwa sasa shetani ndio yuko kazini.DEVILS AT WORK.
USHOGA TUUKATAE KWA NGUVU ZOTE NA KWA GHARAMA YEYOTE.
Na ana moto vby mnoo(devil)......... Ila akaze
 
Back
Top Bottom