Makonda: Mashoga wanataka kuniangamiza

Makonda: Mashoga wanataka kuniangamiza

Suala la kupinga ushoga linahitaji sheria kali na sio kutoa matamko tu,washughulikie tu mashoga wala hawana nguvu kiviile mpaka utetemeke wakikutishia,ingekuwa madawa ya kulevya ningekuhurumia.
 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema tangu alipotangaza kuanza kukamatwa kwa mashoga, amebaini kuna mkakati unawaohusisha watu hao zaidi ya 150 kutaka kumwangamiza.

Kauli hiyo aliitoa jana Dar es Salaam baada ya kumaliza mahojiano katika kituo cha redio Clouds FM, ambako alikuwa akifafanua hoja na changamoto mbalimbali za mkoa wake.

Alisema kuwa baada ya kubainika kwa mipango hiyo, mashoga wanane wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi.

“Lazima watu wajue jitihada na harakati za kusimamia katiba na usawa hapa nchini. Hakuna anayezipenda, vita inakuwa kubwa… Nimebaini kuwa mashoga zaidi ya 150 waliketi katika baa moja Kinondoni wakipanga njama za kunimaliza kwa namna moja ama nyingine, lakini kutokana na taarifa za kiintelijensia, watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni mashoga wameshakamatwa,” alisema Makonda.

Katika hatua nyingine, Makonda aliwatolea uvivu watu wanaosambaza ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii, ikiwamo kutengeneza akaunti feki.

“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina akaunti ambayo inaanza na cheo changu, hivyo akaunti zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda si vinginevyo, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo,” alisema Makonda.

Aliweka wazi kuwa kuna agizo batili lililowekwa katika mitandao ya kijamii, akidaiwa kusema kuwa watu wasiokuwa na kazi watakwenda jela, lakini ukweli ni kwamba ameagiza wenyeviti wa Serikali za mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa maeneo wanayoishi.

Aidha Makonda alisisitiza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo, kamwe Hatoacha kupambana na mafisadi katika halmashauri zote tatu za mkoa wake, pamoja na wauza unga, wafanyabiashara wa shisha na mashoga.

Chanzo: Mpekuzi

===========

My take:

Sema chochote kwa Mkuu wa Mkoa
Kwanza ushukuliwe kwa kutuletea huu ujumbe pili makonda awache kukimbia kivuli chake
 
Hii vita ilisha wasumbua watu wengi....kwa kifupi.....
1.Bondia maarufu duniani manny pacquiao...
2.Muimbaji maarufu wa reggae Alpha Blondy
Unajua kwa nini haya yanatokea...Sababu kubwa hawa mashoga nyuma yao kuna watu wakubwa ...Hebu fikiri mwanamuziki Elton John ni shoga lakini malkia wa Uingereza alimpa heshima ya Knight Bachelor...na kuwa Sir Elton John....Hivyo basi RC kupambana na watu kama hawa ni dhahiri anapambana na watu asiowajua.
Kwa sasa shetani ndio yuko kazini.DEVILS AT WORK.
USHOGA TUUKATAE KWA NGUVU ZOTE NA KWA GHARAMA YEYOTE.
Mkuu unaweza ukadadavua kidogo kuhusu Manny Pacquiao?
 
sasa kama alibaini mashoga zaidi ya 150 walikaa kikao kwanini asiende kuwakamata??hii nchi inamatatizo mengi sana aachane na hiyo ya mashoga
Hajui kuwa watanzania wa karne hii hatudanganyiki kama anasema kulikuwa na mashoga 150 kwenye kikao na yeye anasema anawasaka mashoga sasa alishindwa nini kwenda kuwakamata? Awache kutudanganya
 
Intelijensia ilibaini mashoga 150 wamekaa kikao cha kutaka kumdhuru, ila vyombo vya usalama vimekamata baadhi yao tu, kha! hao walioachwa wameachwa ili waendelee kutoa huduma au? Makonda kuchokoza mashoga ni sawa na kukimbizana na mwendawazimu jalalani, hawa wtu akili zao haziko sawa ujue, umetoa tamko nyamaza acha vyombo vya dola viwakamate kama kuna sheria ya kuwatia hatiani wataenda jela. Dar bado chafu sanaaaa, bora uende kusafisha mitaroni huko kama huna kazi ya kufanya ofisini.
Hiyo sonema ya usafi naona imeanza kupoteza mvuto maana wabongo hatuna muda wa kumsikiliza makonda
 
Kuna mambo meng muhimu ya kufanya Makonda achana na hayo ya ushoga!

Huo mda alio utumia hapo clouds angeutumia kuutangaza mlima Kilimanjaro angalau, kuliko kuogea mambo ya starehe za watu
Kwanza ndio kwanza anaongeza hiyo tv station kupoteza watazamaji kabisa
 
Ni kwasababu ushetani huu umeachiwa muda mrefu.

Na wanaotetea lazima kuna siri nyuma ya panzia.
Haki ipi? zaidi ya uhayawani!kila kitu mungu kaumba kwa makusudio maalum sasa hawakomi ila madhara wanayapata sana kwa muungwana yoyote hawezi kusimama na kulitetea hili pana wengine husema kama makalio ni yake tabu gani? Hivi leo mtu asikie au mzazi wake wa kiume ajitangaze kuwa anatafunwa atajisikiaje?
 
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema tangu alipotangaza kuanza kukamatwa kwa mashoga, amebaini kuna mkakati unawaohusisha watu hao zaidi ya 150 kutaka kumwangamiza.

Kauli hiyo aliitoa jana Dar es Salaam baada ya kumaliza mahojiano katika kituo cha redio Clouds FM, ambako alikuwa akifafanua hoja na changamoto mbalimbali za mkoa wake.

Alisema kuwa baada ya kubainika kwa mipango hiyo, mashoga wanane wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi.

“Lazima watu wajue jitihada na harakati za kusimamia katiba na usawa hapa nchini. Hakuna anayezipenda, vita inakuwa kubwa… Nimebaini kuwa mashoga zaidi ya 150 waliketi katika baa moja Kinondoni wakipanga njama za kunimaliza kwa namna moja ama nyingine, lakini kutokana na taarifa za kiintelijensia, watu kadhaa, wengi wao wakiwa ni mashoga wameshakamatwa,” alisema Makonda.

Katika hatua nyingine, Makonda aliwatolea uvivu watu wanaosambaza ujumbe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii, ikiwamo kutengeneza akaunti feki.

“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina akaunti ambayo inaanza na cheo changu, hivyo akaunti zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda si vinginevyo, hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo,” alisema Makonda.

Aliweka wazi kuwa kuna agizo batili lililowekwa katika mitandao ya kijamii, akidaiwa kusema kuwa watu wasiokuwa na kazi watakwenda jela, lakini ukweli ni kwamba ameagiza wenyeviti wa Serikali za mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa maeneo wanayoishi.

Aidha Makonda alisisitiza kuwa kutokana na matatizo yaliyopo, kamwe Hatoacha kupambana na mafisadi katika halmashauri zote tatu za mkoa wake, pamoja na wauza unga, wafanyabiashara wa shisha na mashoga.

Chanzo: Mpekuzi

===========

My take:

Sema chochote kwa Mkuu wa Mkoa

Hivi, uwepo wa mashoga na bomba langu la maji safi kutotoa maji, kuna uhusiano gani. Sikatai wala hainiathiri kukamatwa au kutokamatwa kwa mashoga, Cha msingi hapa ni kwamba Jiji la Dar linakabiliwa na changamoto nyingi sana ambazo hukwaza wakazi wake kwa ujumla wao. Namshauri Bw. Makonda asikurupuke bali akae chini na viongozi wake wajipangie priorities na wazifanyie kazi systematically badala ya kukurupuka na sensationalism. Kamwe hatutamuona hafanyi kazi kama atakwama kwenye mambo ya msingi ambayo yatalifanya Jiji lionekane kama jiji. After all, Rome was not built in a day. Mkuu wa Mkoa get your priorities on track. Sensations will fail you in a bi way. waelimishe watu ili ufanye nao kazi. Wewe sio Mkuu wa Mkoa wa kwanza, wapo waliokutangulia, jiulize walikuwa wanakosea wapi?
WanaDSM tupo tayari kukusaidia. Remember an old adage: "brawn cannot beat the brain". Goodnight.
 
PM, MOLA mwenyewe atashuka kukulinda... usiwajali hao wanashindana na MWENYE ENZI MUNGU! mwisho wao hao mashoga ni mbaya sana!
 
Nathema hivi kwenye mkoa wang thitak kuthikia mambo ya mathoga na omba omba fhulu thistop
 
Back
Top Bottom