Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,147
- 28,740
Nimesoma nikiwa siamini macho yangu taarifa katika Gazeti la Mwananchi (online) kwamba,
Rais John Magufuli...alisisitiza kwamba elimu yake (Makonda) siyo kitu kwake na kwamba hata angekuwa hajui kusoma yeye ni bora kwake kwa sababu anafanya kazi nzuri ambayo hata baadhi ya waliosoma hawaifanyi"
Imeripotiwa kwamba Rais Magufuli aliyasema hayo leo Jumanne wakati akifungua mkutano mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) uliofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Kilichonishangaza ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, anayejisema kwamba yuko kuinyoosha Tanzania na kuepukana na kila aina ya ufisadi na udanganyifu, anakiri kwamba yuko tayari kumtumia mtu mwenye tuhuma za kosa la kijinai ili mradi tu ni mtenda kazi mzuri, na hatajali malalamiko yanaotolewa dhidi yake, hata kama ni ya kweli?
Nani aliyedai kwamba suala la Makonda ni kutokuwa mfanyakazi bidii? Hakuna. Hata mimi nakubali Makonda ni mchapakazi - lakini haihalalishi kitendo chake cha kufoji, kosa la jinai, kama ni kweli, na Raisi anapaswa aelewe hilo hata bila kuwa na PhD.
Raisi Magufuli anataka tukate shauri kwamba;

- Kufuata sheria za nchi ni jambo linalotakiwa kufanyika pale tu linapokuwa na manufaa binafsi kwake
- Suala la baadhi ya watendaji wa kamati za madini kutuhumiwa kwamba nao ni wachafu na raisi akawatetea inawezekana ilikuwa ni zuga tu
- Raisi anachagua nani wa kuchukuliwa hatua nani wa kuacha pale makosa yanapofanyika
- Kwa hiyo raisi wa Tanzania anavunja kimakusudi Katiba ya Tanzania inayotaka asimamie sheria za nchi bila kupendelea mtu