Makonda anawajibishwa kwa Makosa ya Magufuli why?

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Hakuna mtu mwenye ubavu wa kufanya jamba analochukia bosi wake na akabaki salama makosa yote yaliyotajwa na Marekani ni makosa yanayoungwa mkono na rais wetu so wakuwajibika hapa ni Makonda au Magufuli? tuache unafiki anayetakiwa kuwekewa vikwazo ni Magufuli.
 
Kwanini walimtungua general Kassim wakamuacha Ayatolah? Tuanzie hapo.

Lakini wamarekani navyowajuwa, huwa wanaanza na wale watu ambao ni influential.

Kubwa zaidi, hii ni kuhusu uchaguzi mkuu ujao.
 
Wameanza na huyo!Huko mbeleni tutegemee kuona hatua zaidi!
 
mkuu hizo ni mbinu za kivita , ili kumfikia mkuu wa kikosi cha kivita unamteka askari wake anaropoka kila kitu!! than unamalizia kama unaslide kwenye ganda la ndizi.

ka mfano kengine ni kumshika msafirisha madawa ni hatua kumfikia boss wake! lazma uwe na kidhibiti ( ushahidi) huyu ni mwingia front kwa kujifanya yeye mwamba sasa atavuna alichopanda
 

Mkuu makonda anawajibishwa kwa kosa moja tu ya kupinga hadharani Ushoga. Hayo mengine ya democrasia ni janja janja tu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu makonda anawajibishwa kwa kosa moja tu ya kupinga hadharani Ushoga. Hayo mengine ya democrasia ni janja janja tu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Yah right.... Utafikiri Makonda ndiye mtu wa kwanza kuupinga ushoga.

Zambia wamemfukuza mpaka Balozi wa US kwa ajili ya mashoga na hawakuadhibiwa kama Makonda au Tanzania.
 
Subiri wameanza na malaika wake. Atakapobaki mpweke watajitwalia tu.
 
Marekani ni wataalamu wa kucheza draft, ile kete waliyomsogezea mzee aile ni ya hatari sana. Mpaka sasa mzee anatafuta kete ya kusukuma lakini haioni, maana kila kete anayotaka kuigusa anaona kabisa kuwa anapigwa Super.
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha
 
Tatizo Magufuli kashajiwekea mwenyewe vikwazo vya kwenda Marekani.

Makonda wamempa ban kwa sababu alikuwa anapenda kwenda kuomba visa ubalozini, kila wakimkatalia anarudi.

Walimkatalia mwaka jana, akarudi tena kama wiki mbili zimepita, wamemkatalia tena.

Mwisho wakaona wampige ban asiwasumbue.

Sasa Magufuki kwenye hili hawampati, kwa sababu Marekani hata hataki kwenda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ile ni message sent kapigwa mbwa mwenye mbwa apate salamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…