Kama ilivyokuwa awamu ya 5, ndivyo imekuwa awamu ya 6. Makonda ndio Mwanasiasa anayeogopwa zaidi baada ya Rais. Nini siri yake?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,110
49,825
Awamu ya 5,ukimtoa marehemu Rais Magufuli,hakuna mtu mwingine aliweza kumgusa Makonda.Alikiwa anaogopwa kushinda VP na PM.

Awamu ya 6, Ukimtoa Rais Samia, hakuna Kiongozi mwingine anaogopwa kama Mwenezi Makonda, hakuna Cha VP Wala PM au NPM.

Kwa siasa za Tanzania zinavyokwenda,msije kushangaa baada ya Samia akawa Makonda ingawa Kwa jambo hili Mimi siliungi mkono Kwa sababu tutarudi kule kule tulikotoka.

Makonda anafaa kuwa kwenye nafasi ambayo anadhibitika,Makosa yakiyofanyika Kwa Magufuli hayatakiwi kurudiwa ila Kwa kuwa kitu muhimu Kwa ccm ni madaraka,msije kushangaa Makonda kuwa mgombea Urais ,itategemea na Haki ya upepo wa siasa wa kipindi hicho.Magufuli aliwekwa kuokoa jahadi na huyu anaweza kuja kuwekwa kuokoa jahazi.

View: https://twitter.com/millardayo/status/1754806236451652058?t=E2eW4Bt6kT6MLqTyjqOJEw&s=19

Swali.
Nini Siri ya Makonda kuaminiwa na Ma Rais? Je ana kitu Cha ziada? Muda utaongea.

View: https://www.instagram.com/reel/C3AfThPK91l/?igsh=ZXJuYWxlbWY0dXpv
 
Wanamwita Magufuli mdogo 😂

Uimara wa hawa Akina bwana mdogo unatokana na nani alikuwa Mlezi wake kichama ama baba yake wa kisiasa

Nikupe mifano michache

Mbowe kalelewa na Mwalimu Nyerere kisiasa Ndio unaona kawa Mwamba

Dr Emmanuel amelelewa na Mzee Lowasa Ndio unamwona Hayumbagi kimsimamo

Makonda na Zitto kisiasa wamekuzwa na Mzee Sitta Ndio unawaona Wana Ngozi ngumu na siyo Waoga

Hawa Watafika mbali Sana kisiasa kwa sababu ya Misingi waliyosimamia

Mungu wa Mbinguni awabariki Sana 😂
 
Awamu ya 5,ukimtoa marehemu Rais Magufuli,hakuna mtu mwingine aliweza kumgusa Makonda.Alikiwa anaogopwa kushinda VP na PM.

Awamu ya 6,Ukimtoa Rais Samia,hakuna Kiongozi mwingine anaogopwa kama Mwenezi Makonda ,hakuna Cha VP Wala PM au NPM.

Kwa siasa za Tanzania zinavyokwenda,msije kushangaa baada ya Samia akawa Makonda ingawa Kwa jambo hili Mimi siliungi mkono Kwa sababu tutarudi kule kule tulikotoka.

Makonda anafaa kuwa kwenye nafasi ambayo anadhibitika,Makosa yakiyofanyika Kwa Magufuli hayatakiwi kurudiwa ila Kwa kuwa kitu muhimu Kwa ccm ni madaraka,msije kushangaa Makonda kuwa mgombea Urais ,itategemea na Haki ya upepo wa siasa wa kipindi hicho.Magufuli aliwekwa kuokoa jahadi na huyu anaweza kuja kuwekwa kuokoa jahazi.

Swali.
Nini Siri ya Makonda kuaminiwa na Ma Rais? Je ana kitu Cha ziada? Muda utaongea.
1. Mlokole.
2. Systeam
3. Back Up toka Mtaa wa magogo.
4. Kundi kubwa la SUKUMA GANG linalomzunguka.
5. Mdomo wake usiojali utu wa mtu.
 
Back
Top Bottom