Makonda anapitia kipindi kigumu

Makonda anapitia kipindi kigumu

Mungu siku zote uwashusha wanaojikweza,kujifananisha na Mungu ni kufuru kubwa sana Kwa mwanadamu, maisha ya kujipendekeza,kujikweza,kuwatakia mabaya wenzio huwa hayana mwisho mzuri,usirushe mawe hali unaishi nyumba ya vioo.Na hakuna siri chini ya jua, ukimwaga mafuta kwenye shimo la nyoka hakikisha unayo mafuta ya kutosha.
 
mnafki mmoja katika ubora wake,huyu jamaa atawasumbua kichwa sana,kampiga mtama mzee warioba,anasoma zaburi,kamfunga kamba riz1 anasoma zaburi,piga miti kajala anasoma zaburi,piga miti wema kesho wivu Wema kipupu anaachia hovyo,anasoma zaburi,manji anasoma zaburi,gwajima anasoma zaburi,freeman anasoma zaburi
 
Wanadamu bwana...mambo yakiwa magumu fasta anakimbilia dini,...akishaanza kupata ulaini hataki tena dini...yaani unafiki kiwango cha lami...

Ukishajitambua kua shida na raha zote ni za mwanadamu awaye yote,aombe asiombe lazima uzipate,tena shida ndio nyingi zaidi...dini haina maana.
 
Mithali 1;19-23
19 Ndivyo zilivyo njia za kila mwenye tamaa ya mali; Huuondoa uhai wao walio nayo.
20 Hekima hupaza sauti yake katika njia kuu, Hutoa sauti yake katika viwanja;
21 Hulia penye mikutano mikubwa ya watu, Mahali pa kuyaingilia malango, Ndani ya mji hutamka maneno yake.
22 Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
23 Geukeni kwa ajili ya maonyo yangu; Tazama, nitawamwagia roho yangu, Na kuwajulisheni maneno yangu.
24 Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, asiangalie mtu;
25 Bali mmebatilisha shauri langu, Wala hamkutaka maonyo yangu;
26 Mimi nami nitacheka siku ya msiba wenu, Nitadhihaki hofu yenu ifikapo;
27 Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.
28 Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione.
29 Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha Bwana.
30 Hawakukubali mashauri yangu, Wakayadharau maonyo yangu yote.
31 Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao, Watashiba mashauri yao wenyewe.
32 Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.
33 Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya
 
Sio mbaya, ni ishara ya kutambua udhaifu na unyonge wake, ni ishara ya kumtaka Mungu na nguvu sake.

Ni nani aliye mkamilifu mbele za Mungu? Nampongeza Makonda kwa kutambua kuwa pasipo msaada wa Mungu hataweza.

Imeandikwa, "Ni Heri kumkimbilia BWANA kuliko kuwatumainia wanadamu. Ni Heri kumkimbilia BWANA kuliko kuwatumainia wakuu". Zab.118: 8-9

Vv
Mungu anapenda Sala za mkono wa kulia umetoa wa kushoto usijue...

Sio hizi za maonesho.
 
Mpuuzi tu huyo anafikiri uongozi ni propaganda za ndani ya chama, wacha yamkute. Walikuwepo zaidi yake.
 
ea45e74b58729a30c44621b22f2d1df0.jpg
1a8f8e410dd894a5da9a999f87b2fa96.jpg



Hii Haina ubishi ukimuona Mtu anamtafuta sana Mungu kuliko kawaida yake ujue anasababu za kufanya hivyo inawezekana kuwa amegundua ukweli kwamba ametenda dhambi hivyo ameamua kutubu, lakini hii mtu anakaa kwenye dini moja tu, either anapitia kipindi ambacho ni kigumu yeye mwenyewe kwa uwezo wake hawezi,

Kutokana na maneno yaliyowekwa kwenye picha hizi na mambo yanayoendelea bila shaka muheshimiwa anapitia kwenye kipindi kigumu,

Mshahara wa dhambi ni mauti
Hivi hii picha ni ya kweli au ujanja ujanja? Maana Daah...
 
Nijuavyo mm kila mmoja ana imani yake, kama ni mkristo inamaana haamini uilam, kama ni muislam ina maana huamini juu ya ukristo ndiyo maana hata kwenye viap vya viongozi hutumia kitabu cha dini yake tu , kama msahafu ni msahafu tu na kama ni biblia ni bibli tu.
Kinachomgharimu Daudi Bashite ni unafiki wa kutaka maombi ya dini zote mbili wakati miungu wa dini hizi mbili haipatani.
 
Nijuavyo mm kila mmoja ana imani yake, kama ni mkristo inamaana haamini uilam, kama ni muislam ina maana huamini juu ya ukristo ndiyo maana hata kwenye viap vya viongozi hutumia kitabu cha dini yake tu , kama msahafu ni msahafu tu na kama ni biblia ni bibli tu.
Kinachomgharimu Daudi Bashite ni unafiki wa kutaka maombi ya dini zote mbili wakati miungu wa dini hizi mbili haipatani.
Hilo nalo ni tatizo
 
Back
Top Bottom