Makonda anapitia kipindi kigumu

Hawezi kuitegemea SERIKALI kwa ulinzi...alikwisha waumbua akina SIRO....!!

Hawezi kuwategemea RAIA katika AMANI, UPENDO, UMOJA na USALAMA....kwa sababu kesha wavuruga..!

Hana marafiki ENZI na hatarajii kupata marafiki wapya wa UKWELI....sababu wengi hawamuamini tena..!!

Ndugu wa DAMU wamemuona amevimba kichwa na hashauriki toka alipopata MADARAKA makubwa..!!

Ni wazi sasa anapita katika DARAJA ambalo pengine halitoshi yeye kuweka miguu yake miwili na kuweza KUVUKA ama pengine anapita katika DARAJA ambalo haoni KULIA kwake, KUSHOTONI wala MWISHO wake....!!

Kwa hali kama hii atatamani MKUU wake amtumbue walau aweze ISHI kama awali....

Kweli kijana anapitia KIPINDI kigumu...!!
 
Sizonje ndio nani?
12049637_1009615249090473_3662877625504063905_n.jpg
12049637_1009615249090473_3662877625504063905_n.jpg



huyu mwenye tsht ya njano
 
Mungu wa Darisalama.

Amedhalilisha watumishi wa serikali acha laana imtafune.

ea45e74b58729a30c44621b22f2d1df0.jpg
1a8f8e410dd894a5da9a999f87b2fa96.jpg



Hii Haina ubishi ukimuona Mtu anamtafuta sana Mungu kuliko kawaida yake ujue anasababu za kufanya hivyo inawezekana kuwa amegundua ukweli kwamba ametenda dhambi hivyo ameamua kutubu, lakini hii mtu anakaa kwenye dini moja tu, either anapitia kipindi ambacho ni kigumu yeye mwenyewe kwa uwezo wake hawezi,

Kutokana na maneno yaliyowekwa kwenye picha hizi na mambo yanayoendelea bila shaka muheshimiwa anapitia kwenye kipindi kigumu,

Mshahara wa dhambi ni mauti
 
Paul Makonda Aeleza Kilichomfanya Kutaja Majina ya Watuhumiwa wa Madawa ya Kulevya
Paul Makonda, Siasa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa uamuzi wa kuwataja hadharani majina ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya ni kutokana na maombi ya Watanzania waliyayotoa wakati wa serikali ya awamu ya nne.

Makonda alisema kuwa licha ya watu wengi kupaza sauti zao wakitaka watuhumiwa wa dawa za kulevya watajwe hadharani, lakini Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete yeye hakuwataja huku akiacha vyombo husika vifanyekazi zao kwa usiri.

Lakini kwa upande wa serikali ya awamu ya tano, waliamua kuwataja watuhumiwa hao ikiwa ni kujibu maombi ya kile watanzania walichokitaka tangu kipindi cha nyuma, alisema Makonda jana akiwa kwenye semina ya Walimu Wanaosomesha Quran Tanzania (JUWAQUTA).

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam.

“Mzee Jakaya mlimpigia kelele taja, taja, taja, taja, sasa tulipoingia sisi tukaona wacha tufanye kama alivyokuwa mnataka” alisema RC Makonda.
Aidha, RC Makonda amewakosoa wote walioibuka na kumdhihaki sababu alitaja majina hayo akisema kuwa giza haliwezi kuondolewa kwa giza bali ni kuwaleta waliopo gizani kwenye nuru.

“Uliona wapi giza linaondolewa kwa kutumia giza? Aliyefanya mafichoni anawekwa hadharani na harudii tena,” alisema Makonda.
Katika awamu ya tatu ya vita dhidi ya dawa za kulevya, RC Makonda hakutangaza majina hadharani kama alivyofanya katika awamu mbili zilizopita ambapo alimkabidhi majina 97, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Sianga ili ayashughulikie.
 
Wasiwasi wangu ni kuwa hii series inaweza kukatishwa mapema kabla stelingi hajafa kwenye majani, kama ile ya faru John.
Hapana hii movie bado Tamu Maana manji bado hajaonyesha hasira zake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom