Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Haiwezekani mtoto usijue nyendo za mzazi wako. Cha msingi watu wengi huwalinda wa kwao hata kama ni waharifu na hilo ni kosa. Tusiwe na mazoea ya kula tu na kutohoji unavyokula vinatoka wapi?
Sio kila mtoto anayejua nyendo za mzazi wake na wengi wanaojua hawana uwezo wa kudhibiti nyendo hizo.
 
Kabwe ni home father lakini sisapoti hiki kitendo alichofanya huyu mwanamke. Kwa kipare huu ni ukosefu wa adabu uliopitiliza. Hata kama mkubwa amekosea namna alivyomuadabisha Baba yake still mbele ya umma wa watanzania hakupaswa kufanya hivi. Mbona kaka zake walikuwa na busara au unadhani wao hawakuumizwa na ile style ya asulubiwe asisulubiweee? Lakini waliamua kuwa wakomavu.Alichofanya huyu dada hakina tofautu na style ya makonda aliyotumia kumshitaki kabwe. mwanamke wa hivi hata ukioa atakuwa jipu tu.
 
Mkuu, ni rahisi kutoa na mawazo ya namna yako but vaa viatu vyake vya ukuu wa mkoa halafu upime uone kama angefanya hivyo angefikiriwaje na jamii!
Nikivaa viatu vyake common sense ingenituma nisiende msibani kwanza kakiri mwenyewe watu wengi walimshauri asihudhurie akawapuuza.
 
Lingine kweli mbele ya jeneza la baba yako mzazi unakuwa na uwezo wa kuWa busy na simu? au ndio Misiba ya kisasa?
Quinine huwa sina muda wa kujibuzana na mtu aliyeishiwa hoja. All I said ndio ukweli wenyewe. Siko hapa kufurahisha mtu.
 
Mpuuzi tu..sasa kwa kumchunia inasaidia nini?baba yake hakuwa muadilifu,hilo halina ubishi.kote alikopita alikuwa analaumiwa.angekuwa muungwana angemwambia baba yake aache ubadhilifu..mjinga tu.kwanza hata makonda amefanya ubinadamu tu kwenda msibani.
Mbn wapinzani walivyokuwa wanapiga kelele khs kabwe ccm waliweka pamba masikioni? Ubaya wake amekuja kuona makonda juzi. ccm acheni unafq
 
View attachment 350809

Anna Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amegoma kumpa mkondo Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Tukio hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa pole kwa familia ya Kabwe.

Wakati Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.

Kitendo hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili 19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini mikataba iliyoikosesha mapato serikali.

Kabwe alifariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauli yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto watano; wanne wa kiume na mmoja wa kike.
Shkamoo mtoto wa Kipare
 
lakini kuwepo kwake pale kunaongeza maumivu ya familia......hasa kwa mambo aliyoyafanya hivi karibuni...kwani ilimshinda nini kumwacha mkuu wa wilaya aende akamwakilishe?
Ila Mtoto wa kabwe alishasema kuwa baba yake alikuwa anaumwa na hata alipofukuzwa alikuwa hayupo likizo..
Mimi naona ni coincidence tu imetokea..
Makonda is the man. Much respect to him
 
In short Kabwe alikuwa kama king Maker.. Huu mpunga wote unaweza kukuta hata ccm walikuwa wanautumia kwenye kampeni zao
Na Ndivyo ilivyokuwa haswaaa. baba wa watu alitumika tu. Jmn inauma sn hlf mkwere ht kutoa pole hakuonekana.
 
Back
Top Bottom