Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Makonda angejiongeza tu.Asingeenda kuuza sura.
Ana Kabwe kaweka maslahi ya familia kwanza.Big up.
 
kwani marehemu aliwahi kufanya ubinadamu? nikumbushe...alikosea angejiunga CHADEMA mgemsafisha fasta.
Wewe umewahi kufanya ubinadamu? Kwani hukusikia hotuba ya mnafiki ambaye hajawahi kufanya ubinadamu? Kwani watumbuaji wao hawajawahi kufanya ubinadamu? Kwani madhaifu ya kibinadamu hufanywa na wanyama?

Kama hata wewe hujawahi kufanya ubinadamu basi umekuwa ukifanya kinyume chake.

Pole sana kwa maswahibu yaliyokusibu!
 
Binafsi mimi ningemwagia maji,yaani kumsema hadharani mbaba wa watu ,tena im sure Makonda alijuwa kabisa kuwa Kabwe alikuwa ni mgonjwa,Binti wa Kabwe safi sana
Thank u victorie,issue Si makosa ya Kabwe..,, Hatakama mtu wangu WA karibu angefanya alofanya Kabwe,afu Makonda Akaja kwenye msiba,,hisia za chuki zingekuwa pale pale! Ndg Ni ndg tuu, haijalishi. Kibinadam Makonda asingeenda! Full stop
 
Usitafute kivuli cha kujificha kwa hoja yako mfu! Ilikua ni Busara Tu kwa mkuu wa mkoa, kumwagiza hata mkuu wa wilaya akamwakilishe! Serikali ingewakilishwa! Huyo binti Kama angeweza kufanya chochote zaidi ya kile kuonyesha hisia zake angefanya!
 
View attachment 350809

Anna Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amegoma kumpa mkondo Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Tukio hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa pole kwa familia ya Kabwe.

Wakati Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.

Kitendo hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili 19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini mikataba iliyoikosesha mapato serikali.

Kabwe alifariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauli yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto watano; wanne wa kiume na mmoja wa kike.

Hajatumia Busara huyo Binti
 
Usitafute kivuli cha kujificha kwa hoja yako mfu! Ilikua ni Busara Tu kwa mkuu wa mkoa, kumwagiza hata mkuu wa wilaya akamwakilishe! Serikali ingewakilishwa! Huyo binti Kama angeweza kufanya chochote zaidi ya kile kuonyesha hisia zake angefanya!

Wewe na huyo Binti ni typical binadamu na bado hamjatoka hapo na hamjui maana ya maisha na ndiyo maana mmejaa chuki na visasi visivyo na msingi, maisha ni zaidi hivyo, kama ulikuwa na akili wewe na huyo binti mngejua kwamba Makonda hakwenda kwenye huwo msiba kama Makonda bali amekwenda kama Mkuu wa Mkoa ambaye ni muwakilishi wa Raisi JMTZ na Serikali kwa ujumla, sasa unapomdharau namna hiyo ina maana umemdhrau Raisi JMTZ na Watz kwa ujumla!
Kuna namna nyingi ambavyo unaweza kuonyesha protest yako lkn siyo hivyo!
 
Human nature inam_support huyo dada...I,e anybody with BOLD mind could do the same.
Ni wanafki na viherehere pekee ndio watampinga huyo dada alichofanya.

Anyway_na support kutumbuliwa kwa marehemu ila the how_ndio inaleta shida....hope mheshimiwa sana atakuwa kajifunza kitu kwenye hili.
 
Sasa mkuu..alichofanya huyo dada na wewe kuoa vinauhusiano gani? Nifafanulie tafadhali
 
Na mara nyingi mabinti waliolelewa na Wababa "smart" hupata shida sana katika ndoa zao,maana hutaka kuwalinganisha waume zao na tabia za baba zao
Binti anakumbuka jinsi Mama alivyokuwa "well treated" na baba yake,anaona mbona huyu wangu hafanyi kama baba alivyokuwa anafanya kwa Mama??

Ndio maana unakuta kutwa kucha binti anasema "Aaa yani baba alikuwa anamfanyia Mama hivi na vile"
Ukizingatia Baba kama Kabwe,alikuwa anawalea watoto wake kwa maisha safi,shule unaenda kwa amani,hela ya matumizi,hupati shida uwapo shule au chuo nk

Lazima aumie,asononeke na hasa akiona baba anasemwa hadharani na "mtoto" kama Makonda.Maana Mzee anapokuwa anapiga madili hasemi kuwa hizi ni hela za madili.

Damu nzito kuliko maji,niliwahi kukaa na jamaa baba yake ni mlevi sana,lkn alikuwa hakosi kuwalea watoto wake vizuri,kuna siku tunapita sehemu tukakuta watu wanapiga kelele eneo la Bar,ikabidi tupite kutazama,kufika pale tukakuta baba wa jamaa amelewa chakari,kajikojolea na amelala fofofo
Barmaid anamvuta kumuamsha Mzee wafunge Bar...huku akitoa maneno makali na kumzaba makofi.Damu nzito kuliko maji,Jamaa alitembeza kichapo kwa bar maid na waliokuwa wanamgasi Mzee,akamchukua mzee kwenye Tax hadi home

Japo kiukweli mzee alichokuwa kafanya hakikuwa sahihi,lkn mtoto alipatwa na "damu nzito" akamsaidia.Binti yupo sahihi
Una akili nyingi.thank uu
 
yeuwii jamani ....dadys girl, muhurumieni huyo kidada jamani anamaumivu makali mno...tuwaombee amani wafiwa hasa mjane wake..jamani
 
Jamani hivi huyo binti anajua maana ya serikali-yaani kwa shutuma zile alitaka makonda akae kimya ama kweli taifa litajengwa na wenye moyo
 
Kupeana mkono ni ishara ya mawasiliano ya ndani. Mara nyingi kupeana mikono ni ishara ya upendo au hata kuomba msamaha. Kuukataa mkono wa mtu ni ishara ya vita au kuonyesha kuwa vita iliyopo bado haijaisha.

Lakini kupeana mkono kwa kukejeli hiyo ni mbaya zaidi. The sky is the limit. RIP Kabwe
 
View attachment 350809

Anna Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amegoma kumpa mkondo Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Tukio hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa pole kwa familia ya Kabwe.

Wakati Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.

Kitendo hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili 19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini mikataba iliyoikosesha mapato serikali.

Kabwe alifariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauli yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto watano; wanne wa kiume na mmoja wa kike.
MHESHIMIWA MAKONDA NAYE ASEMA HAYA
 
Wewe na huyo Binti ni typical binadamu na bado hamjatoka hapo na hamjui maana ya maisha na ndiyo maana mmejaa chuki na visasi visivyo na msingi, maisha ni zaidi hivyo, kama ulikuwa na akili wewe na huyo binti mngejua kwamba Makonda hakwenda kwenye huwo msiba kama Makonda bali amekwenda kama Mkuu wa Mkoa ambaye ni muwakilishi wa Raisi JMTZ na Serikali kwa ujumla, sasa unapomdharau namna hiyo ina maana umemdhrau Raisi JMTZ na Watz kwa ujumla!
Kuna namna nyingi ambavyo unaweza kuonyesha protest yako lkn siyo hivyo!
Hata angeenda Mkuu wa Wilaya angemuwakilisha Rais vilevile! Na ingeepusha yote hayo! Unataka watu wote wawaze Kama wewe? Who are you by the way???
 
Back
Top Bottom