Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,030
- 59,682
- Thread starter
- #141
Na atapata kweli..huko hotelini atapata atakacho
Na atapata kweli..huko hotelini atapata atakacho
Safi sana,eti huyo ndio mkuu wa mkoa,hii ni laana tena ya kiwango kikubwa kabisa,au laana imempata baada ya KUMPIGA MAKOFI Mzee WARIOBA,kazi ya mkuu wa mkoa sio kupambana na MASHOGA,hiyo haipo kabisa katika utendaji wake,anatakiwa kufanya jitihada katika majukumu nyeti ambayo yamedorora tangia awamu nne zilizopita ili kuhakikisha hadhi na maendeleo ya mkoa wa Dar yanakuwepo kwa kiwango kinachotakiwa sio kufuatilia mashoga mahotelini,huo ndio uongozi wa kukurupuka.Mkuu wa mkoa wa dsm kasema kuwa atapambana na mashoga popote walipo ataenda hadi mahotelini.. Source Magazetini
My take: kuwafuata mashoga mahotelini ni hatari. Ila nampa support yangu. Hii hulka ya ushoga ni mbaya sana
=======
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza operesheni ya kuwasaka mashoga jijini humo.
Makonda amesema vitendo hivyo vimeanza kuongezeka jijini humo na lengo lake ni kuwaokoa watoto wasiige mambo hayo yanayoonekana kukua kwa kasi.
Bosi huyo wa mkoa amesema, “hili ni tatizo linalokua kwa kasi sitaruhusu liendelee katika mkoa wangu, nitawasaka popote walipo”.
“Hata hapa bandari wanaweza kuwapo mashoga wafichueni, mkiona mtu ana tabia za ajabu ajabu mfichueni, tutashughulika nao”.
Chanzo: Mwananchi
Hii ni Tanzania bana sio marekani
USA baby!Teh! Teh! Teh! Naona mnamchokoza MMAREKANI.
ofisi gani hiyo wanayohitaji interview za kijeshi!Maofisini wengi sana hawa...kazi itakua kubwa kuwakamata.
Mkuu wa mkoa wa dsm kasema kuwa atapambana na mashoga popote walipo ataenda hadi mahotelini.. Source Magazetini
My take: kuwafuata mashoga mahotelini ni hatari. Ila nampa support yangu. Hii hulka ya ushoga ni mbaya sana
=======
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza operesheni ya kuwasaka mashoga jijini humo.
Makonda amesema vitendo hivyo vimeanza kuongezeka jijini humo na lengo lake ni kuwaokoa watoto wasiige mambo hayo yanayoonekana kukua kwa kasi.
Bosi huyo wa mkoa amesema, “hili ni tatizo linalokua kwa kasi sitaruhusu liendelee katika mkoa wangu, nitawasaka popote walipo”.
“Hata hapa bandari wanaweza kuwapo mashoga wafichueni, mkiona mtu ana tabia za ajabu ajabu mfichueni, tutashughulika nao”.
Chanzo: Mwananchi
Wananchi wa Dsm wana shida nyingi sana za kijamii na za kiuchumi kuliko kadhia ya uwepo wa mashoga! Nini vipaumbele vyetu? Pia yeye hawezi kukamata, hivyo atahitaji polisi ambao kwa sasa hawatoshi wala kulinda watu wa Dsm na mali zao! Kwenda kuwatumia polisi hao kwenye operation zake sio matumizi mabaya ya nguvu kazi ya Taifa? Pia operation hizo zitahitaji bajeti ya utekelezaji, hapo sio matumizi mabaya ya kodi za wananchi?
Hivi ni States zote Marekani zinaruhusu ushoga?Marekani wameruhusu ushoga hadi jeshini... Makonda hajui anachotaka kukifanya.. Kwenye hili marekani watakuwa very serious na harshy.. Msishangae misaada yote kufutwa
Mimi sijaelewa kiundani hii issue, kwani kuna sheria yoyote juu ya ushoga?
Na hao mashoga wanawasumbuaje watu kiasi kwamba waendesha nchi wawasake mjini dar, huku wezi na majambazi wanaosumbua wananchi wapo wamekaa mkao bila kusumbuliwa na wengi wanajulikana na hao wengine?
Sasa tunasubiri kusikia kavamia nyumba za majambazi na wezi waliokubuu wa jijini kwake maana hata kutembelea Dar, tunaogopa siku hizi. Bora zaidi mkoani kwangu.