Mshinga
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 3,532
- 1,128
Sitaki kuingia sana kwenye huu mjadala lakini suala la Marekani kutotaka sana kupigana na Urusi ni vile maslahi yao yanakuwa hayajaguswa sana lakini uwezo inao. Na kitu kingine kutokana na ukweli kwamba Urusi nayo ina nguvu kubwa ya kijeshi kuanzisha military confrontation kunaweza kuwa na gharama kubwa sana kwa Marekani. Hata Urusi hana interest ya kupigana na Marekani kwa sababu zilezile. Kwa kifupi hawa wakipigana uwezekano wa Mmarekani kushinda ni mkubwa lakini je gharama yake ni kiasi gani?? Je ni vyema kushinda vita halafu mwishowe unapoteza nguvu yote na kuiruhusu China kuwa super power? Pili kuna nyuklia, kwa mfano labda Marekani inaweza kushinda kwa bahati Urusi waamue kukubali matoke lakini vpi wakiamua kutumia nyuklia? Ni kweli hata Marekani ana nyuklia lakini ni nani anataka Mutual Assured Destruction aka MADness!!!
Kaka mziki wa U.S sio mdogo sema watu wanaangalia consequences!!
nimekuwa msomaji na mfatiliji mkubwa sana wa mataifa haya mawili URUSI na MAREKANI.
huwezi kunidhibitishia kuwa MAREKANI ina UWEZO wa kuishinda URUSI.
kwa kifupi sana nitakuelimisha juu ya hisoria ndefu ya haya mataifa.
vita baridi ilikuwa inahusu mambo mawili.
1.UCHUMI.(superiority of world economy or super power economy)
2.UWEZO WA KIJESHI.(superiority of world military capability or military super power)
historia ni ndefu sana lakini ilionekana theory rahisi ilikuwa kushinda kwanza nguvu ya uwezo wa kijeshi ili ushinde nguvu ya uchumi.
1988 marekani ilizidiwa katika uwezo wa kijeshi na ilisalimu Amri na waliamriwa kushusha makombora yao waliyokuwa wameweka Uturuki ili waishambulie Urusi, shariti hili ilikuwa litekelezwe kwanza ndio Urusi ikubali kushusha makombora yake iliyoyaweka Cuba ili kuishambulia marekani.
kwa kifupi Marekani ndio waziwazi imewahi kukiri kushindwa na Urusi katika vita ya Vifaa vya kijeshi.
baada ya hapo Marekani ndio ikabadili theory ya kuishinda Urusi na ikaja na mpango wa kuisambaratisha Urusi wa kuua Muungano wake.
hapa ndipo Marekani ilishinda na kufanikiwa. hapa hakukuwa na maswala ya uwezo wa vifaa vya kivita.
kutokana na URUSI KUSAMBARATIKA.
Marekani ilishinda vita ya ukuu wa uchumi Duniani na mpaka sasa inajulikana America is a Super power.
ukisikia super power ya Marekani sio kwenye silaha bali ni kwenye uchumi.
Toka 1991 Urusi iliposambaratika Marekani iliamini kuwa Urusi isingeedelea tena kutaka kupambana na Marekani kwenye ukuu wa silaha.
kukudhihirishia kuwa hii vita ya ukuu wa kijeshi haikuwahi kabisa kuisha na wala marekani haikuwahi kabisa kushinda.
tafuta kwenye mtandao ndege ya marekani ijulikanayo SR 71(blackbird)
hii ni ndege hatari zaidi iliyokuwa chini ya marekani na ilinonekana kuitesa Urusi.(taarifa za mashuhuda ambao ni malubani wa Marekani na wale wa Urusi ndizo zilikuja kudhidhirisha haya)
kwa kifupi sana, ndege hii ilikuwa na kasi kushinda kasi ya ndege zote za Urusi na ajabu zaidi ikashinda kasi zote za makombora ya Urusi. ilikuwa inatembea kwa kasi ya mita 1,023 kwa sekunde moja.
wakati Urusi ikiwa imeshasambaratika 1998 walifanikiwa kutengeneza ndege hatari ya Mig 31.
hii ndegeya URUSI ilisababisha ndege zote za SR 71 za marekani kusitaafishwa ghafla mwaka 1998 baada ya wamarekani kuipeleka SR 71 Urusi kama walivyozoea kuwa hakuna silaha wala kombora la kuifikia kwa kasi yake hata ilipolengwa na makombora ama kukimbizwa na ndege za urusi. wakati huu SR ilikutana na Mig 31 na ikadhibitiwa vilivyo na haikufua dafu na ilikuwa mshituko kwa marekani na mwaka huohuo wa 1998 marekani ikatangaza kuzistaafisha ndege zote za SR 71 na wakatangaza mpango wa kuunda ndege ya SR 72 ili waweze kupambana na ndegeya Mig 31.
hii Mig 31 ilikuwa na kasi zaidi ya SR 71.
huu ni mfano mmoja tu nimekupa kuhusu uhalisia kuwa marekani haikuwahi kushinda vita ya technolojia wala ya silaha.
ALAFU LAZIMA UJUE KITU KIMOJA MUHIMU SANA.
marekani inatangaza sana taarifa na propaganda zake tofauti na Urusi.
inawezekana propaganda za marekani zimekuaminisha kuwa ina nguvu sana kushinda Urusi.
ila wamarekani wenyewe wanajua ukweli kuhusu nguvu za Urusi na wana ushahidi wa kihistoria na kiujasusi wa kushidwa mara nyingi na urusi kimyakimya wakati wao huwa ni wa kwanza kutangaza alafu urusi huwa mara nyingi ni ya kwanza kufikia mafanikio.
nikupe mfano mmoja.
kuna kitabu kikubwa sana cha NASA kinachoelezea historia ya mambo ya anga miaka 1980 kikiandikwa .
ukisoma Mule ndio utajua Urusi ni nani, achana na propaganda, wale ni wazee wa kimyakimya.
kitabu kimechapwa miaka ya 1980s kwa kumbukumbu yangu na kilitungwa mahususi kwa ajili ya kumkumbuka mwanaanga mmoja huko marekani na shirkia la NASA jina simkumbuki maana siko nacho hapa ila nikikipata nitakwambia jina la kitabu hicho ili usome mwenyewe.
vita baridi ilikoleza zaidi mafanikio vita ya anga kwa urusi na marekani.
lakini kila marekani ilipotangaza kupeleka chombo chao angani urusi ilikuwa kimya, lakini kabla hajafanya hivyo Urusi ilirusha chombo chake kwa mafanikio makubwa,Marekani ilipotangaza kuipiku urusi kwa kupeleka chombo kwenye Orbit Urusi ilikuwa kimya lakini kabla ya marekani haijafanikiwa Urusi ilirusha chombo chake na kukifikisha kwenye orbit.
marekani ilipotangaza kupeleka chombo mwezini Urusi ilikuwa kimya, lakini kabla Marekani haijafanikiwa Urusi ilirusha chombo chake na kilitua salama mwezini na vifaa vya Uingereza vilithibitisha kuwa kweli hicho chombo kinaonekana kipo mwezini.
nimelazimika kukupa haya machache sana juu ya tabia ya Urusi na Tabia ya Marekani.
Urusi ni wazee wa kimyakimya lakini ni watu hatari sana na wamarekani wanalijua hili na ndio maana ukitafuta taarifa za urusi kuhusu silaha ni jambo lenye usiri mkubwa sana tofauti na marekani wazee wa kupayuka na kuropoka.
Kwa sasa marekani wana dege hatari sana lijulikanalo F22 hili dege ni balaa, achana na habari za B52 ama B2 ambazo ni nuclear capable. hili dege ni balaa.
mrusi alishajibu mapigo haya kwa dege lake lijulikanalo kama T50 .
hizi ndizo ndege hatari zaidi kwa karne ya sasa.
ndege pekee duniani yenye uwezo wa kuidhibiti F22 ni T50.
kwa sasa ndege za kivita zinaenda generation ya sita. huku ulaya wakiwa wameachwa mbali maana mpaka sasa hawajaweza kuyafikia mataifa haya mawili kutengeneza ndege ya generation ya 5 wakati Urusi na Marekani sasa wakiwa kwenye harakati za kutengeneza generation ya sita ya ma-drones.
pia URUSI na MAREKANI ndio mataifa pekee hayanunui slaha bali yanajitengenezea silaha.
nina mambo mengi ya kuchambua lakini niishie hapa.
wala swala la nuclear si tishio sana kwa mataifa haya kwa kuwa yana interceptors za kipekee kupangua hata hayo makombora.
mwisho kuna watu wanadhani drones(UAVs) ni technolojiia ya marekani pekee huku kumbe urusi wana drones zao japo ni wazee wa kimyakimya.