Mshinga
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 3,532
- 1,128
Kaka nashukuru kwa nondo kama hizi. Kiukweli sijafuatilia haya mambo kwa muda sasa ila uchambuzi wako nimeukubali japokuwa uko baised kiasi fulani.
Pale juu nimeandika "UWEZEKANO WA MAREKANI KUSHINDA NI MKUBWA" sikusema ni lazima Marekani ashinde kwa kuwa natambua vita ni zaidi ya uwezo wa kisilaha na fedha na ndio maana wavietnam japokuwa waliumia sana lakini walimsimamisha Mmarekani huyohuyo. Kimsingi pamoja na yote uliyoandika officially Marekani ndio taifa lenye nguvu kubwa zaidi za kijeshi duniani kuliko mataifa yote na ndio wenye bajeti kubwa zaidi ya kijeshi kiasi kwamba bajeti ya Marekani pekee ni kubwa kuliko mataifa 14 yanaiyofuatia yakijumuishwa kwa pamoja.
Hivyo basi pamoja na uwezo wa Russia ukweli unabaki palepale kuwa sababu inayofanya Marekani asipigane na Urusi ni gharama kubwa ya vita hiyo. Hawa wakipigana mwisho wa vita watakuwa masikini pengine kuliko taifa lolote duniani na hapo ndio watamuachia China na India usukani. Wao sio wajinga kiasi hicho ndio maana huwa wanapigana mikwara mbuzi tu lakini mwisho wa siku inabidi wakubaliane au wakubaliane kutokukubaliana. Sana sana huwa wanapimana nguvu kwa kutumia proxy wars kama Afghanistan, hapo Syria na hata North/South Korea conflict.
bro sijawa biased.
unaposema Marekani ina uwezekano mkubwa wa kushinda lazima uwe na sababu ambazo zinawapa nafasi kubwa.
mimi nilichofanya nikukuonyesha tu kuwa advantage hiyo haipo kwa sababu huwezi kutabiri hapa na sababu ni rahisi tu.
kuna muda wamarekani wanaipiku urusi kwa muda mfupi kwa jambo hata moja lakini warusi wana counter attack haraka sana, kuna muda urusi nayo inaipiku marekani na marekani inacounter attack haraka sana.
hiyo advantage unayoisema ya marekani mimi siioni.
na nilikupa tu historia fupi sana ya nani alikuwa anashindwa na ni wakati gani.
lakini historia inaonyesha marekani ndiye alishindwa mara nyingi kuliko yeye alivyoshinda.
na ukumbuke kwa muda mrefu marekani amekuwa akitumia mgongo wa NATO lakini Urusi ni Taifa moja tu linalopambana na mataifa lukuki na warusi wanaju salama yao Ni kuweka kwenye silaha.
Sir Eisten alisema"sifahamu vita ya tatu ya dunia itapigwanwa kwa kutumia silaha zipi, lakini nina uhakika vita ya nne ya dunia itapiganwa kwa kutumia fimbo na mawe"
tafakari sana huu usemi.
alafu kuhusu kujaribisha silaha kwenye vita za wengine.
haya mataifa huwa hayapeleki silaha zake hatari zaidi kwenye majaribio ya vita nyingine kwa sababu ya siri na ulinzi.
siri nyingi za siaha huwa zinakuja kusemwa baada ya muda mrefu kupita na wakati huo walishaenda level nyingine ya silaha.
HIVI UNAJUA KUNA SILAHA YA HALI YA HEWA.
hii silaha pia inasemakana mrusi inampa jeuri na huenda amefikia hatua nzuri ,lakini hata mmarekani amewahi kuifanyia utafiti silaha hii.
hii silaha japo inasemekana inawezakuzuiwa chini ya sheria za kuzuia silaha za maangamizi.
wanadai wanaweza kufanya volcano ilipuke sehemu yoyote na kusababisha mafuliko, ama kubadili hali ya hewa na kuleta vimbunga na kusababisha mafuliko makubwa.
yapo mengi sana lakini hawa jamaa si rahisi kusema nani atashidwa ama atashinda hiki ndicho nachojua mimi.
mathalani kuna watu wengi hawaelewe kuwa hata waanzilishi wa technolojia ya anga marekani baadae ikazaliwa NASA ni Warusi. na technolojia hii imeanzishwa na Ujerumani chini ya Hiltler na ikaenda Urusi na Urusi ndio wakaipeleka marekani.
na hata sasa marekani haina chombo cha kupeleka wanasayansi wake kwenye kituo cha utafiti kilichojengwa angani, kinajulikana kama Internationla Space Station(ISS) au International Space Center(ISC).
kwa sasa ili wafike huko hao marekani wanategemea chombo cha Urusi kiitwacho Soyuz lakini ni wangapi wanajua hili?
hiki ndicho chombo pekee kinachotumika sasa na mmarekani hana baada ya Space Challenger kustaafu baada ya kuzeeka.
hawa wanajuana izuri sana na wanaogopana kuliko sisi tunavyoweza kufikiria.
SIJAHARIRI MAANDISHI.
nina muda sana