Ah ah ah ah ah, huyo ndio Mtono na wengine kama yeye ambao watu wa kawaida hawawajui au hawaelewi nini maana ya kuwa Commando (mwanajeshi). Watu wengi sana wameathirika na hizi filamu za kina commando John, Rambo n.k. Wanashindwa kutofautosha ukweli na maigizo.Huyu hata mie nilimsikia kuwa alichanganyikiwa kwenye mafunzo ya Kikomandoo huko Izrael. Ila wengi wanamkubali kuwa alikuwa na uwezo wa kumuona mtu kwa nusu sekunde na atakukumbuka.
Kuna vijana waliiba mahindi na kwenda kuchoma msituni. Wengine walikaa doria wakiangalia kama kuna mtu anakuja. Walipokuja kumuona huyo, wakapotea msituni na kumuacha peke yake. Aliitisha kambi nzima ya jeshi na kuwachoropoa mmoja mmoja. Ila mwisho akajisifu kuwa kama Wanajeshi basi kashatengeneza maana jinsi vijana waliyoondoka hapo na kwa mwendo wa chui na kupotelea vichakani, hadi alijisikia raha. Kwa sababu hiyo akawaachia huku akiwaambia kuwa wasirudie tena maana yeye siku zote yupo hatua moja mbele ya KURUTA/SERVICE MAN.
Acha dharau na kujifanya unajua kumbe hujui lolote...! Zile ni demo za kuonesha utimamu wa mwili..,
Hzo shotokan unazoongelea ni ushuzi tu kwa combinations za commando.., hawapigani aina moja ya martial art.., ila kwa ujinga wa baadhi ya watu wanafkiri kinachooneshwa pale ndo final.., style yako ya mapigano ndo ita-determine combination ya commando akupige vp...,
hakuna pigano la kiraia utaweza mpiga commando.., kama huamn jarb, na kama unajisifu una black belt ya karate utatandikwa ngumi moja iloshiba inayopiga push-up 500 daily, ikitua kwny koo utalia kama mtoto kanyimwa jojo, mamaee
tatizo la majina kuwa universal ndio hili....
mrisho ngassa na lionel messi wote ni WASHAMBULIAJI
vodacom premier ligue na barclays premier ligue zote ni LIGI KUU ZA SOKA
umoja wa afrika na jumuia ya ulaya zote ni REGIONAL INTEGRATION BLOC
............kweli?
sasa jijibu mwenyewe kama wa kwetu na wa kwao wapaswa wote kuitwa MAKOMANDOO
Jamani nyie acheni kuongea mambo ya historia , ndio jeshi letu limewahi kushiriki operesheni mbalimbali na vita nchi nyingine lakini ni zamani na mbinu zilizotumika kipindi hicho ni tofauti sana na sasa hivi kitekonologia na mambo mengine .
Kwenye historia hata rumi ilikuwa na jeshi bora zaidi liliweza kuteka eneo kubwa leo wapi rumi ? Miaka hiyo wamarekani walikuwa na uwezo wa kuipiga na kuikalia nchi yoyote lakini ona ndege yao ilivyoangushwa Iran Juzi hata uchina iliwahi kuangusha ndege zake za kijasusi .
Je sisi tunafanyiwa ujasusi mara ngapi na kupigwa picha mara ngapi kutokea Juu na sehemu zingine kama kwenye mitandao jamii na forums kama hizi ? tumejiandaaje maana hizi zote ni silaha za kivita .
Juzi hapa raisi wa zamani wa marekani amefika mawasiliano karibu yote hayakuwa vizuri mpaka leo hii baadhi ya huduma zinasumbua za mawasiliano je tumejiandaaje na hujuma au visa kama hivi ?
Komandoo haswa komando units kama zile zinazopambana kwenye uokoaji na shuguli nyingine zinahitaji teknologia za mawasiliano za hali ya juu ili ziweze kutekeleza kazi na wajibu wao vizuri , angalia ile Unit iliyomuuwa osama Bin laden iliandaliwa kwa kipindi fulani na kuwa maalumu kwa ajili ya operesheni hiyo tu na walikuwa wnafuatiliwa live toka ikulu ya marekani na idara nyingine za jeshi la nchi hiyo .
Juzi hapa akaunti ya twitter ya mke wa raisi iliingiliwa ikachukuwa zaidi ya masaa 10 kuweza kurekebisha lakini mchezaji mmoja wa Manchester united alipiga picha ikulu ya marekani na kuweka kwenye twiter yake ikaondolewa ndani ya Dakika kadhaa .
COMMANDO wa israel anaweza ruka toka kwenye ndege bila kutumia parachute,na huku akitumia breathing techniques za yin and yang anaweza float hewani for sometime bila parachute kabla aja hit the ground
Mimi nimeshuhudia komandoo wa kiisrael alizunguukwa na Makomandoo wa Hizbullah, alijigeuza kuku ili akwepe ! Hata hivyo walimkamata na kumfanya kitoweo!
Shy, nakubaliana na wewe. Haitoshi kuwa na makomandoo hodari na waliofunzika lakini kama hawana vitendea kazi bora vyenye kuendana na wakati kiteknolojia, mafunzo yao yanakuwa na manufaa kidogo sana. Wale wa jana wameonesha wako imara, wakakamavu na wana maarifa ya kutosha, lakini je, hiyo inatosha bila vifaa vya kisasa kama wale wa marekani na israeli? Kwa dunia ya leo vifaa vya kisasa vina nafasi kubwa sana katika kufanikisha kazi zao.Kuna mambo mengi ya kufanya zaidi haswa kwenye zama hizi za teknologia , msimamo wangu utabaki ule ule kuvunja mawe na matofali sio maonyesho si miaka yote wanafanya hivyo ? toka tumepata uhuru ? Kanda yetu inakabiliwa na tishio la ugaidi sasa hivi mbona hatujaona UNIT KOMANDO ya kupambana na ugaidi kwenye maonyesho hayo ? na hata awareness nyingine kwa watu walioenda kwenye maonyesho hayo ?
Hatujawahi pata inshu hapa bongo ya kuwatumia tuone kama kweli wako fii kama wenzao huko nje. But I know watakuwa fit coz kama ni training wanatapa kama hiyo ya kwa Obama. So let be assured wako fit.
Wakuu nimecheki clip kwa michuzi, kwenye ile segment ya kuvunja vitu, I rest my case.
Nimewakubali.
Ivi shimbo na mwamunyange nao ni makomandoo au?
Alikuwa anaitwa 'Tamim'Huna kumbukumbu, ulikua hujazaliwa au hufuatiliagi mambo yanavyokwebda.
Komandoo Hatib Ghandhi "Mac Ghee" aliekua akitafutwa kwa kosa la kutaka kupindua Serikali ya Nyerere alilazimika kukwepa risasi za akina Mabere Marando enzi hizo akiwa usalama wa Taifa kwa mtindo wa "Samasoti" akibenuka juu ya magari pale Kinondoni Mkwajuni!!
Uliza kwa wanaojua au hata tafuta simulizi au vitabu vya huo uhaini.
Although kina Rambo wamezidisha uongo mwingi kama wa makomandoo watano kupigana na Jeshi la zima la Wa-Vietnam, but kibongobongo hatuwezi kukosa wawili watatu.
Alikuwa anaitwa 'Tamim'
Hivi mfupa wako wa mkono ni mgumu kupita lile tofali ? Kwa teke lake moja kupitia mazoezi yale anaweza kuvunja mbavu zako ngapi? Hao wanaopigana kwa ndege ambazo hazina rubani bado wanahitaji kuingia uwanja wa mapambano. Ndege bila rubani haiteki eneo! Pia dawa ya ni suicide bombers na ma roadside bombs ! And it works, mpaka leo Afghan hakuna achievement yeyote.Hilo tofali limetengenezwa maalum kwa ajili ya hiyo event,
Pengine hata ni la mchanga tupu bila Cement!!!!
Na hizo mbao unajua aina yake.
Nakubaliana na mdau mmoja hapo juu kua siku hizi vita haipiganwi kwa kushikana shikana au kuonana ana kwa ana kama series za kina Jumong na Taesso!!
Watu wanatumia "auto pilot" ambazo zina sensa ya kugundua ujio wa kitu cha hatari kama "missile bomb" na kukikwepa
Tamim alikuwa Komandoo na aliasi kwa mujibu wa madai ya wabaya wake, usalama wa taifa. Alitoroka jeshi baada vita vya kagera na alikimbilia Kenya, alirudi kuungana na makampten waliopanga kufanya mapinduzi, akina Hans Pope, Maganga na Mac Ghee.Yeah nimekumbuka mkuu!!
But walikua kundi moja na Mac Ghee na mwanzao Kadeghe kama sikosei.
Ingawa si kwa kuwafananisha kwa kiwango cha uongo wa kina Schwarzenneger au War-Bus, but wale hawakua Makomandoo?
Hivi huwezi kupambanua tofauti ya muokoaji na mpiganaji ? Huwezi kuona tofauti ya Askari Magereza na Polisi? Soma soma humu upate ufahamu zaidi!Tumeshndwaje kuwatumia kwenye ajal ya meli ya NUNGWI?