Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMG-20170530-WA0020.jpg
Tigo matatizo wameyataka wao
 
Kila jambo na wakati wake

MHUBIRI 3

1.Kwakila jambo kuna majira yake,Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2.Wakati wa kuzaliwa,na wakati wa kufa,wakati wa kupanda na wakati wa kung'oa yaliyopandwa.

3.Wakati wa kuua ,na wakati wa kupoza Wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga.

4.Wakati wakulia na wakati wa kucheka,wakati wa kuomboleza na wakati wa kucheza.

5.Wakati wa kutupa mawe nawakati wa kukusanya mawe,Wakati wa kukumbatia na wakati wa kutokumbatia.

6.Wakati wa kutafuta na wakati wa kupoteza,Wakati wa kuweka na wakati wa kutupa.

7.Wakati wa kurarua na wakati wa kushona;Wakati wa kunyamaza na wakati wa kunena.

8.Wakati wa kupenda na wakati wa kukuchukia;Wakati wa vita na wakati wa amani

9.Je!Mtendaji anayo faida gani katika yale anayojishughulisha nayo?

Hakika hiyo ndiyo kanuni ya maisha mkuu,tukiijua na kuifuata ,hatutapata shida.

Kila jambo na wakati wake na majira yake.
 
Mhubiri. Kitabu kimojawapo kizito sana katika Biblia. Mfalme Suleman mpaka anatisha aisee. Nadhani alikiandika uzeeni mwishoni mwa maisha yake. Baada ya kuwa Bill Gates wa dunia ya wakati ule, kuoa wanawake 700 na masuria 300; pamoja na kuponda raha za kila aina katika Mhubiri anahitimisha kuwa bila kumcha Bwana na kuzishika njia zake, yote haya ni UBATILI mtupu na kujilisha upepo. Hakukosea!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom