Makapuku Forum

ZABURI 71

8.Kinywa changu kitajazwa sifa zako, Na heshima yako mchana kutwa.

TUOMBE
Asante Baba kutuamsha salama.
Tunajikabidhi mikononi mwako,utulinde,utuongoze,utuponye.
Neema yako yatosha.


Amen

MBARIKIWE SIKU NJEMA
 
Hakika asante sana ubarikiwe
 
2005 - Liverpool yashinda taji la Ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya.

Ni baada ya kupigwa 3-0 wakati wa kipindi cha kwanza, kabla ya kurudi kipindi cha pili na kusawazisha goli zote.

Wakaenda kushinda kwa mikwaju ya penati chini ya uongozi wa Nahodha Steven Gerrard na kocha Rafa Benitez.

Ni moja kati ya fainali za kukumbukwa.
 
1961 - Apollo program: Rais wa Marekani John F. Kennedy anahutubia Congress na kuwaambia Mpango wa Serikali kupeleka binadamu wa kwanza Mwezini kabla ya kumalizika kwa Muongo.
Kisha kikatengenezwa kituo maalumu kilichoitwa NASA's Kennedy Space Center ambapo mnamo July 16 1969 safari ya kwanza kwenda mwezini ikazinduliwa ambapo Neil A. Armstrong,Michael Collins na Edwin Aldrin walipaa na chombo hicho kisha wakawa binadamu wa kwanza kufika mwezini
........
 
1953 - Daniel Passarella anazaliwa.

Alikuwa ni beki kisiki wa kati wa timu ya taifa ya Argentina.

Mmoja kati ya mabeki bora kuwahi kutokea.

Alifunga magoli 134 na kuwa beki wa pili katika orodha ya mabeki waliofunga magoli mengi zaidi nyuma ya Ronald Koeman ambaye kwasasa ni kocha wa Everton.

Ni mchezaji pekee wa Argentina kutwaa Kombe la Dunia mara mbili mwaka 1978 wakiwa nyumbani na 1986 pale Mexico.
 
1963 - Umoja wa Nchi huru za Afrika ( OAU ) waanzishwa huko Addis Ababa nchini Ethiopia.
Nkrumah na Nyerere walishiriki vilivyo uanzishwaji huo pamoja na Marais wengine wa nchi kadhaa km vile Libya,Senegal,Ethiopia,Togo n.k
Nyerere alienda kama rais wa Tanganyika ....Nchi zilizopata uhuru pekee ndo zulikuwa wanachama
.......
 
- Ni siku ya Watoto wanaopotea nchini Marekani.

Siku hii ilianzishwa na Rais Ronald Reagan baada ya kupotea kwa mtoto Etan Patz.

Mtoto Etan Patz , May 25 mwaka 1979 wakati anaenda kupanda basi la shule.

Hakuwahi kuonekana tena. Hivyo ile siku aliyopotea inaazimishwa kila mwaka.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…