Achana na ng'ombe..... Ubora wa ma barobaro wa Ajax upo zaidi katika kucheza kama team (team work) na ni mara chache sana wamekuwa wakionyesha ubora wao ule ule wakati team work inapofeli, pamoja na kuwa na vijana wenye uwezo Mkubwa lakini bado wamekuwa wakifanya kazi na utamaduni wa Ajax wa kucheza kama timu mwanzo mwisho kuanzia katika academy zao.
Manchester united mara nyingi katika michuano hii wamekuwa wakiamua matokeo yao kwa njia mbinu na team work lakini pia individual performance imekuwa ikitumika zaidi kuwafikisha hapa walipofika...... Namna wachezaji wa Manchester united walivyopewa uhuru katika kucheza kama timu ila pia namna wanavyokuwa huru katika kutumia mbinu na uwezo binafsi katika kutafuta matokeo ndio moja ya vitu vinavyowafanya kufika fainali.
Ajax kama watakubali kuruhusu goli la mapema ndivyo watakavyojitoa mchezoni.... Lakini pia umakini mkubwa zaidi unahitajika katika eneo la difference ya Ajax kutokana na aina ya washambuliaji wanaokutana nao na ile kasi yao ikiongozwa na Rashford. Hapa ndipo Sanchez anatakiwa kusimama imara na kumlinda Onana.
Kama united watakubali kuruhusu goli jioni kuanzia dk ya 80 basi mchezo kwao utakuwa mgumu kuliko kawaida.... Na hii imetokana na muda ambao united wamekuwa wakishindwa kupindua matokeo kuanzia dk ya 75 mpaka kipenga cha mwisho.
Kama Ajax atakubali kwenda katika dk 120 basi wanaweza kuruhusu goli nyingi katika dk30 zile za kuongeza..... Hii inatokana na aina ya kikosi cha vijana walichonacho na uzoefu wa kikosi cha united katika hatua kama hizi.
Nje ya hapo mchezo utakuwa mzuri na fainal tamu kabisa katika kipindi hichi ligi zimefika tamati.
Muda saa 9:45pm usiku.
Ajax fc vs Manchester United