Makapuku Forum

MITHALI 3

24.Ulalapo hutaona hofu;Naam, utalala usingizi wako utakuwa mtamu

TUOMBE

Asante Baba kwa ulinzi wako mchana kutwa,tunaomba toba kwa yote tuliyokosea,asante kwa kuwaponya wagonjwa wetu,kuwapa faraja wafiwa na mayatima,tunakuomba endelea kukaa nasi Baba peke yetu hatuwezi.
Walinde wasafiri ,bariki ndoa na wote wanaotarajia kuingia kwenye ndoa,wasaidie wanaotafuta wenza wapate wa kufanana nao.
Baba tunaomba utukumbatie kama kuku anavyokumbatia vifaranga vyake.
Tunaenda kinyume na pepo wabaya na nguvu zote za giza damu yako ya thamani inene mema usiku wa leo.
Asante Baba kwa sababu utatenda sawa na mapenzi yako.
Tunaomba na kushukuru katika jina la Yesu Amen

MLALE SALAMA
 
Shukrani sana Shimba WA BUYENZE nashukuru nimemaliza masomo yangu salama huko Tel Aviv nchini Israel, nafurahi sana kwa sapoti yenu sababu hamkuniacha peke yangu hadi wakati huu wasasa ambao nimerejea tena hapa.

Nafurahi kuona mambo yote yanaenda vizuri na hakuna chochote kilichokwama...


Pia nichukue nafasi hii kuwatumia salamu zangu za pongezi wote ambao mlikuwa hapa kuhakikisha kuwa hakiribiki kitu.

Nawapenda wote
 
Usiku mwema watu wa Mungu View attachment 510782
Why should I change my life? Turn down for what?

Ushauri wa maisha bwana siku hizi kila kona mtandaoni. Zamani mambo haya ilibidi mpaka ukalishwe chini na wazee "hashikome" usiku kijijini Kolomije. Natumaini kizazi hiki kitakuwa powa balaa
 
Hongera kwa kumaliza masomo yako na karibu tena nyumbani
 
Amen
 
Huwa nafurahi kila nikiona post yako humu maana huishi kumchokoza Shedebe
 
NUKUU YA LEO

If you want something New, you have to stop doing something old


Kama unataka kitu kipya, unapaswa kuacha kufanya kitu cha zamani

Haya maneno yaliwahi kutamkwa na mkufunzi, mwalimu na mwandishi wa mambo ya utawala na uongozi Bw. Peter Fernand Drucker.

Peter Drucker alizaliwa November 19 1909 nchini Austria na kufariki November 11 2005 ktk jiji la carlifonia nchini marekani.

Peter Drucker ni mkufunzi na mbobezi wa masuala ya uongozi na utawala..Amefanya kazi nyingi katka muda wa miaka 95 aliyoishi dunia

Peter Drucker ndio Father of modern management.

Back to Jf and kapukuz..

Ukitaka mambo mapya acha kufanya mambo ya zamani..

Maisha ni yako, uamuzi ni wako, hatua ni zako wewe mwenyewe.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…