Makapuku Forum

Afrika katika ubora wake wa hali ya juu ya ujinga.

Mkuu ahsante sana kwa 10 bora.
 
33% ya Watanzania ni mambumbumbu pure
Idadi yao kubwa wanapatikana huko vijijini
Hawa ndio CCM mbele kwa mbele....

........
This too myopic Madenge!

Huwa nawashangaa sana nyie "wasomi" ambao huwa mnakimbilia kuwadhihaki na kuwadharau hawa watu wa vijijini. Pengine kweli ni "mambumbumbu pure" kwa vile hawajui kusoma na kuandika, lakini ukikaa,na kuongea nao watakushangaza. Hata katika masuala ya kisiasa wana welewa mpana na vitu wanavyovitaka vina mantiki kubwa sana. Kuna tasnifu moja na uzamivu (PhD) imeandikwa na mwanafunzi wa Political Science kutoka chuo kikuu cha Leiden (kama sijakosea) ina mambo mengi sana ya kujifunza kuhusu attitude hizi kuhusu watu wa vijijini si katika siasa tu bali katika masuala ya maendeleo na mengineyo.

CCM kupendwa na watu hawa "mambumbumbu pure" haishangazi kwa sababu Mwl. Nyerere aliwekeza sana huko na CCM ilijiimarisha mno kuanzia mashinani na kuendelea. Shida ya upinzani ni attitude hii hii ya huu usomi huu uliojaa dharau. Badala ya kwenda huko vijijini kuwafuata hawa "mambumbumbu pure" na kuwaelimisha kuhusu sera zao, upinzani umewekeza zaidi mijini. Na hili ni tatizo.

Kubadili attitude ya watu inahitaji muda na vyama vya upinzani kama vina akili ni lazima viwekeze sana huku vijijini. Hawa "mbumbumbu pure" wana mengi sana ya kuwafunda kuhusu siasa, usomi, mahusiano ya watu, gia za angani; na mengineyo.
 
All the time God is good
Aren't you overusing this phrase? I know it is an irrefutable fact that God is good all the time (assuming that someone is not an atheist and ignoring the philosophical + logical conundrums), copying somebody's unrelated post only to say "All the time God is good" is kind of weird and overreaching!
 

Ila yule kiongozi wao wa zamani (Sankara) hata yeye nafikiri hakuwa na elimu kubwa lakini ni miongoni mwa viongozi maarufu Afrika kuwahi kutokea
.......
Umaarufu wake unatokana na nini? Tunaupimaje umaarufu wa viongozi hawa? Na ni nani anayeamua kiongozi fulani awe maarufu? I am just curious kwa sababu mtu unaweza kujikuta unasema fulani ni kiongozi maarufu kwa sababu tu umesikia hivyo kwa marafiki na watu wanaokuzunguka.

Anyway, rafiki yake wa chanda na pete Compaore hakumtendea haki huyu kijana kwa kumuua kinyama na kumzika katika kifusi tena kwa kutumia greda la Halmashauri!
 
Umefafanua vizuri
Sio kwamba nawadharau bali ni umbumbumbu wa kutojua kusoma na kuandika tu
Mimi napenda sana maisha ya kijijini
Ni kweli tatizo CCM ina mashina mengi huko wala haipingiki

Tukutane asubuhi
.........
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…