Makapuku Forum

Makapuku Forum

ZABURI 55

16.Nami nitamwita Bwana naye ataniokoa

17.Jioni ,Asubuhi,na adhuhuri nitalalama na kuugua,Naye atasikia sauti yangu.

TUOMBE

Baba Mungu wa Mbinguni
Asante kwa ulinzi wako mchana kutwa,tunaomba toba kwavyote tuliyokosa kwa mawazo,maneno na matendo uturehemu.

Usiku huu Baba ,nyoosha mkono wako tufunike Baba kama kuku afunikavyo vifaranga

Naenda kinyume na pepo wa chafu,nguvu za giza uchawi usiwe na nafasi katika malango yetu usiku wa leo.

Tunamuombea SHIMBA YA BUYENZE BABA mponye jino Baba wa mbinguni,mtoe katika maumivu makali aliyonayo ukamtulize mwili na roho.

Baba wafariji wafiwa,wajane yatima ponya wagonjwa wote.

Tuna malaika wako watakatifu wazunguke vitanda vyetu na waweke vituo majumbani mwetu,Baba linda nyumba zetu damu Takatifu ikaponye nyumba zetu kwa hatari zote za kimwili na kiroho maana imeandikwa "...BWANA asipoulinda mji yeye aulindaye akesha bure..." ZABURI 127:1b Kesha nasi BWANA

Tunaombea ndoa,familia ,watoto na wote katika familia zetu ziwe familia takatifu kama ile ya Yesu,Maria na Yoseph

Mungu Baba tunakuomba utuamshe salama tukiwa na nguvu za kukutumikia,Roho Mtakatifu shuka utuongoze katika safari yetu ya mbinguni.

Tunaomba yote katika jina la Yesu mpatanishi na mwokozi wetu.

Amen

Tunawaombea marehemu wote wapumzike kwa amani

USIKU MWEMA WAPENDWA
Ameen mama mchuchu nimeisubili hii sala mpk nikalala bila sala
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom