
ZABURI 91
1.Anayeka chini ya ulinzi wa Mungu Mkuu,anayeishi chini ya kivuli cha Mungu Mwenye Nguvu.
2.Ataweza kumwambia Mwenyezi-Mungu:"Wewe ni kimbilio langu na ngome yangu;Mungu wangu ninayekutumainia!"
3.Hakika Mungu atakuokoa katika mtego;atakukinga na maradhi mabaya .
4.Atakufunika na mabawa yake,utapata usalama kwake;mkono wake utakulinda na kukukinga.
5.Huna haja ya kuogopa vitisho vya usiku,wala shambulio la ghafla la mchana;
6.Huna haja ya kuogopa baa lizukalo usiku,wala maafa yanayotokea mchana
TUOMBE:
Mwenyezi Mungu Baba wa Mbinguni asante kwa jioni hii ya leo,umetulinda mchana kutwa na sasa ni usiku.
Tunaomba toba,tusamehe yote tuliyokukosea kwa mawazo ,maneno na matendo tunaomba uturehemu kwa kuwa tumetenda dhambi,tusaidie tuwasamehe wote waliotukosea walioomba msamaha na wasioomba msamaha Baba tupe nguvu ya kuendelea mbele.
Tunawaombea wote wagonjwa,wafiwa,wenye tabu na mateso mbalimbali huruma yako ikatende kazi ndani ya wote.
Tunawaombea wasafiri majini nchi kavu na angani wasafiri salama
Baba tunaenda kinyume n nguvu zote za giza usiku wa leo wachawi,mapepo yakashindwe katika jina la Yesu.
Malaika walinzi wakae nasi waweke vituo majumbani mwetu damu ya Yesu ya thamani inene mema kwetu tulale salama,tawala roho zetu,tawala akili zetu,tawala ndoa zote,tawala familia zote,navunja roho zote zilizo kinyume Baba hazina mamlaka juu yetu,tunaomba tulale kama watoto wachanga huku tukizingirwa na malaika walinzi
Asante baba maana utatenda sawa na mapenzi yako katika jina la Yesu Amani itawale
Marehemu wote wapumzike kwa amani amen
USIKU MWEMA MBARIKIWE