Makapuku Forum

hahahahh
musukuma anataka kunipa kazi naanzaje kumuuliza mtu eti we mweupe ni kibonge

yeye amkubali tu kila kitu atajua mbele kwa mbele kwa atakavyokutana navyo huko
Haya basi nimebwaga manyanga. Ye yote tu atafaa ila mtafutie kwanza Shedede. Ukimalizana naye basi ndo uanze kumhangaikia Msukuma wako mbishi...
 
Ishi na watu kwa wema utafurahia muziki

Najua tumekuwa na wakti mzuri na tunapoenda kuimaliza Jumatano hii basi kama kawaida Makapuku nawakaribisha katika ka-kipengele haka ka ala za muziki na hasa tukijikita katika udonoaji na wadonoaji wa gitaa.

Kwa wapenzi wa muziki wa dansi miaka 20 nyuma, na wanaofuatilia miziki ya bakulutu, bendi ya Maquis Original ni bendi yenye umaarufu mkubwa hapa nchini ikiundwa na wanamuziki wengi toka Kongo na mmoja wao ni mpiga gitaa maarufu Dekula Kahanga almaarufu Vumbi. Mitindo kama Zembwela na Sendema haiwezi kukutoka kiurahisi.

Sikiza vibao cha Ngalula, Mayanga, Makumbele, Karubandika na vingine vingi katika mitindo ya Sendemaa na Zembwela. Gitaa utakalosikia linamuongoza muimbaji awe ni Tshimanga Assossa au Kasaloo basi ni la nguli Dekula Kahanga.

Bado yupo na anafanya muziki wake nchini Sweden akiwa na band yake ya Dekula Band.

Hapa nakuwekea baadhi ya nyimbo alizoweza kuzicharaza na kuzifanya zikavutia zaidi.

FYI: Upigaji wake mzuri umechangiwa zaidi na kufuatisha mipigo ya Nguza Viking (yupo jela sasa akitumikia adhabu ya maisha gerezani)

Dekula anaamini katika kuishi vizuri na watu, kwani huwezi kujua maisha yatakupeleka wapi.

hapa najiuliza nikuache na Ngalula au nitupie clip ya YouTube ambayo anacharaza baadhi ya nyimbo zake, isiwe ishu, nakuacha na zote mbili, suala la kukumalizia MB zako mpenzi msomaji liko nje ya uwezo wangu (joke)



 
Amen

Ahsante sana mama mchungaji kwa neno lenye kutia nguvu mioyo yetu.

Ubarikiwe sana
 

...ni sababu pekee iliyonifanya niwe mchangia damu bila malipo hadi leo (well, huwa wanatoa soda na biskuti-natamani wangekuwa wanatoa kinywaji kwa tusiokunywa soda, basi hata chai).

Sijawahi kupungukiwa damu labda hela, na mara nyingi nina furaha sababu naamini ni tendo jema kujitolea damu, linkufanya uwe na nidhamu.
 
Kalubandika ndio naielewa sana
 
Amina,nimefurahi sana..kutoa bila sababu..bila kutegemea malipo..bila kutafuta sifa..bila kutegemea shukurani..BILA SABABU YOYOTE NDIO KUTOA KWEMA
 
Ubarikiwe mkuu Jorowe
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…