Makapuku Forum

9/Diasdado Cabello Huyu bwana alionja Urais wa Venezuela kwa muda wa siku moja pekee baada ya Rais kujiuzulu kufuatiia kuonekana anasapoti ubepari
Hivyo Cabello akachukua madaraka kisha akamchagua Hugo Chavez kuwa Makamu wake halafu yeye mwenyewe akajiuzulu na Chavez kuwa Rais...mchezo ndo ulivyochezwa
Yaani kautumikia urais kwa muda wa siku moja pekee
..........
 
8/Ratu Tevita Momoedomu
Huyu jamaa alikuwa Waziri mkuu wa Fiji katika muhula/vipindi viwili vifupifupi kama stuli za Manzese..
Mwaka 2000 alikaa madarakani kwa masaa mawili pekee wakati mwaka 2001 alikaa madarakani kwa siku mbili
Mwaka 2000 yalitokea mapinduzi/maasi ambapo yeye pekee akajikuta ndo amebaki kwenye jengo la serikali hivyo kuwa kiongozi kama ngekewa vile halafu mwaka 2001 akachaguliwa tena baada ya kuachia madaraka ili kukidhi matakwa ta kikatiba
............
 
Aisee siku mbili tu
 
Khaaa
 
7/Roger LaFontant
Huyu alikuwa kiongozi wa kijeshi huko Haiti ambapo mwaka 1991 alikuwa Rais kwa masaa 24 tu
Rais alijiuzulu hivyo Katiba ya nchi hiyo kumpa madaraka Jaji Mkuu Estha Pascal Trouillot ambaye aliitisha Uchaguzi wa kidemokrasia lakini Fountant akatumia fursa hiyo kufanya mapinduzi na kujitangazia Urais lakini ghafla bin vuuuu wajanja zaidi yake wajampindua ndani ya masaa 24 tu yaani wakati anaamka tu huko Ikulu hata swimming pool hakugusa!!
...........
 
hahahhh
 
Aisee
 
6/Joseph Goebbels Huyu alikuwa Kansela wa Ujerumani kwa muda wa masaa 5 pekee mwaka 1945 May 1
Wakati Vita Kuu ya Pili ikiendelea na Adolf Hitler kuonekana kuzidiwa akaamua kumteua swahiba wake Goebbels kuwa Kansela akiamini ni Waziri wa Propaganda ndo pekee anayeweza kumuokoa lakini hata kabla hawajaanza propaganda zao wakagundua wamezingirwa hivyo kuamua kujiua
Jamaa kaonja ukansela masaa yasiyozidi Matano pekee
........
 
5/Boris Yeltsin
Huyu mzee alijiteua mwenyewe kuwa Waziri mkuu wa Urusi mwaka 1998
Hii ilikuwa wakati yeye akiwa Rais na mgogoro wa kisiasa ukiwa umepamba moto hivyo akaamua kumpunguzia majukumu Waziri Mkuu kwa kujiteua yeye mwenyewe
Baada ya kukosolewa vikali na wananchi wake na wapinzani akaamua fasta kuachia huo Uwaziri na kumteua mtu mwingine
Yaani ndani ya masaa manne tu...kukurupuka ni kubaya!!!
.........
 
hahaha...h ata sura yake ipo kama aliyekurupuka
 
4/Skender Gjinushi
Huyu alionja Urais wa nchi ya Albania kwa muda machache kama masaa mawili au manne tu
Ilimuwa mwaka 1997 baada ya uongozi wa kibepari wa Sali Berisha kushindwa uchaguzi wa kidemokrasia halafu kukataa kuachia madaraka hivyo Spika Slender akaamua kuchukua madaraka kwa mujibu wa katiba kuwa Rais wa mpito
Kisha Bunge la Albania likaamua kumtangaza mshindi halali wa Uchaguzi Mkuu Rexhep Meidani kuwa Rais mpya wa Albania
Hii ilifanyika ndani ya masaa manne pekee
.......
 
hahahaha aisee hatar thana
 
Aisee
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…