Makapuku Forum

Mchana mwingine tena, narejea kukupa habari fupi na muziki unaotawaliwa na gitaa kwa sababu naamini kikundi chochote cha muziki chenye gitaa, ngoma na watendakazi kinakuwa ni sehemu ya kumfanya msikilizaji afurahie maisha kwa namna yoyote ile. Iwe ni kwenye furaha au huzuni, nyuzi za gitaa kwenye muziki zitakupa amani.

Mchana huu tumwangalie Ramadhan Mtoro aka Dr Remmy Ongala (Sauti ya Mnyonge), gwiji hili la muziki, alipata umaarufu wake mkubwa duniani akifanya muziki wake nchini Tanzania.

Muziki wake aliuita 'ubongo beat' maana yake 'radha za akili
Pamoja na umaarufu wake duniani, hakuna mwanamuziki ambaye anaweza kusema anajulikana kama Dr remmy, alijulikana sehemu nyingi tanzania iwe ni vijijini au mjini, alikuwa ni 'Michael Jackson' wa Tanzania. Ni mwanamuzi aliyefanya ziara nyingi za kimuziki zilizosimamiwa na WOMAD na hii ilimfanya kutumbuiza na magwiji wakubwa kabisa wa muziki duniani

mtaalamu wa kupiga gitaa na kutunga mashairi ya kutetea haki za mtu wa chini, na kuikosoa serikali na kufariji wanaosikiza vibao vyake,Dr remmy pamoja na kifo chake, muziki wake bado unaishi.

Sikiza clip hii ya YouTube , sikiza gitaa hapo, linalosikika zaidi alipiga yeye.

''walipewa madaraka wakashindwa kuwajibika...., barabara mashimo matupu, shehe anauza bangi, padri anauza sabuni za msaada, saa mbili asubuhi foleni kwenye supu, ofisi ipo na nani...'



Shunie anza na hii kwanza
 
Kweli siku gazifanani leo watu wanaingia km kwa foleni vile...
Siku mbaya
....
 
Nani kakupa mamlaka kutangaza Tanzania kuna njaa?

......
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…