Makapuku Forum

NUKUU YA LEO

I have always fought for concrete facts, for justice

Mara zote nimekuwa nikipigania ukweli na haki


Haya maneno yaliwahi kutamkwa na mwanamapinduzi, mwanasheria na Rais wa 17 wa Jamhuri ya Cuba Bw. Fidel Alejandro Castro Ruz alizaliwa 13/08/1926 na kufariki dunia nchini Cuba 25/11/2016 akiwa na miaka 90. Na kuzikwa katika makaburi ya Santa ifigenia santiago de cuba.

Fidel atakumbukwa kwa kuwa mwanamapinduzi na muumini wa siasa za kijamaa. Fidel Castro alipigwa sana na mataifa ya kipebari ikiwemo marekani na washirika wake wa magharibi.

Fidel castro atakumbukwa kwa kuepuka majaribiao ya kumuuwa zaidi ya 600 yaliyopangwa na vyombo vya usalama vya marekani.

Leo ni tarehe ambayo ulinanza uvamizi wa Bay of pigs Invasion na ukadumu kwa siku 3. Ilikuwa vita ya kumpindua fidel castro iliyoratibiwa na CIA kipindi cha rais Dwight D. Eisenhower na kutekelezwa mwaka 1961 chini ya Rais John F. Kennedy

Marekani walitumia zaidi ya Us dollar 13.1 million kuaanda uvamizi huo ulifanyika kwa siku 3 na mwisho majeshi ya Cuba yakashinda.

Nirudi kwenye Nukuu.

Fidel castro alikuwa na msimamo, alitekeleza kile anachokiamini ni sahihi kwa watu wa Cuba . Misingi aliyoweka hai zamani ndio siri ya mafanikio ya nchi ya Cuba leo hii..

Leo Cuba wanatoa Elimu nzuri na huduma nzuri za afya zaidi ya nchi zingine za marekani ya kusini. Wana vyombo vya usalama vizuri . Hayo ndio matunda ya ukweli na haki aliyopigania Fidel Alejandro Castro Ruz.




Descanse en paz Fidel Castro
 
Asante mkuu kwa lishe ya ubongo

Tulikumis sana kiongozii ila vizuri kama umetukumbuka ukiwa salama ...welcome again
 
Ahsante kwa uchambuzi mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…