Makapuku Forum

Makapuku Forum

b311e921bb7298dd661125ee2c44787b.jpg

Goodmorning kwa hisani ya kisheti Herrera
 
NUKUU YA LEO

I have always fought for concrete facts, for justice

Mara zote nimekuwa nikipigania ukweli na haki
ae48aab8bd3baf516c02890ccb72ff82.jpg

Haya maneno yaliwahi kutamkwa na mwanamapinduzi, mwanasheria na Rais wa 17 wa Jamhuri ya Cuba Bw. Fidel Alejandro Castro Ruz alizaliwa 13/08/1926 na kufariki dunia nchini Cuba 25/11/2016 akiwa na miaka 90. Na kuzikwa katika makaburi ya Santa ifigenia santiago de cuba.

Fidel atakumbukwa kwa kuwa mwanamapinduzi na muumini wa siasa za kijamaa. Fidel Castro alipigwa sana na mataifa ya kipebari ikiwemo marekani na washirika wake wa magharibi.

Fidel castro atakumbukwa kwa kuepuka majaribiao ya kumuuwa zaidi ya 600 yaliyopangwa na vyombo vya usalama vya marekani.

Leo ni tarehe ambayo ulinanza uvamizi wa Bay of pigs Invasion na ukadumu kwa siku 3. Ilikuwa vita ya kumpindua fidel castro iliyoratibiwa na CIA kipindi cha rais Dwight D. Eisenhower na kutekelezwa mwaka 1961 chini ya Rais John F. Kennedy

Marekani walitumia zaidi ya Us dollar 13.1 million kuaanda uvamizi huo ulifanyika kwa siku 3 na mwisho majeshi ya Cuba yakashinda.

Nirudi kwenye Nukuu.

Fidel castro alikuwa na msimamo, alitekeleza kile anachokiamini ni sahihi kwa watu wa Cuba . Misingi aliyoweka hai zamani ndio siri ya mafanikio ya nchi ya Cuba leo hii..

Leo Cuba wanatoa Elimu nzuri na huduma nzuri za afya zaidi ya nchi zingine za marekani ya kusini. Wana vyombo vya usalama vizuri . Hayo ndio matunda ya ukweli na haki aliyopigania Fidel Alejandro Castro Ruz.
9344407052d084758818128c0c0cfa3c.jpg

4bc4c65895674139a3adbf4175dacee0.jpg

Descanse en paz Fidel Castro
 
Asante mkuu kwa lishe ya ubongo

Tulikumis sana kiongozii ila vizuri kama umetukumbuka ukiwa salama ...welcome again
 
hatuna namna ndo mpira mkuu...
man u vs Chelsea review...

Kosa la kwanza katika mchezo huu lilikuwa ni la David Luiz kushindwa ku clear mpira aliokuwa nao kwa haraka na kusababisha lingard kublock na ukamkuta Rashford aliyekuwa na papara na kupiga mbali kabisa na begovic....... Hapo kidogo aigharimu timu kwa uzembe wake.

Kosa la pili kubwa katika mchezo huu ni pale Mwamuzi aliposhindwa kuuona mkono wa Andre Herrera ulipouongoza mpira kabla ya ku turn na kupiga pasi ya ndizi iliyokwenda kuzaa kosa la tatu la David Luiz kushindwa kuuingilia mpira ule na kuamua kuukimbilia pasi na kujua speed ni tatizo kwake na kujiruhusu kukaa mgongoni mwa Rashford wakati akilitizama goli......

Kosa la nne likikuwa katika himaya ya captain Cahill wakati luiz alifanikiwa kuuondosha mpira katika box la 6 la Chelsea Cahill yeye alikuwa bize kumyanyua Rashford katika wakati ambao alitakiwa kufanya making na kuuangalia mpira...... Herrera anakutana na mpira mzuri anapiga rebound na unazama golini na kuandika goli la pili.....

Pattern ni kitu kilichoingia katika mfumo wa Jose Mourinho na kikashirikiana na mfumo kuleta matokeo hayo...... Team work kwa upande wa Manchester united ilionekana kuwa na uwiano mzuri katika pattern kuliko majina watu waliyoyafikiria awali katika line up...... Binafsi nilipenda mbinu tata alizoingia nazo Mourinho za kuwatumia wavulana katika mchezo wa wanaume.

Ng'olo kante ni mfanyakazi bora pale Chelsea..... Na mara zote kazi yake ni kuwaweka salama wale watatu wa nyuma pindi timu haina mpira(kukaba) lakini pia kuifikisha mipira katika upande wowote mbele na karibu zaidi ya ule mstari wa kati. Eden Hazard ni mtu mwingine bora kabisa katika kupokea kile alichokitafuta Ngolo kante na kukiwasilisha vyema katika eneo husika na kuwafanya Chelsea wawepo hapo walipo kwa sasa....... Chini ya ulinzi wa Andre Herrera hakukua na ile kazi ya Eden Hazard tuliyoizoea ila pia chini ya ulinzi wa Fellain na Pogba hakukuwa na ile kazi ya mfanyakazi bora bwana ng'olo kante pale katikati ya uwanja.....

Hapa Patterns za Mourinho zilifanikiwa ku lock mfumo wa bwana Conte kwa kuua njia mbili za mafanikio katika muundo wa Chelsea..... Herrera alifanikiwa kuua mipira yote sumu iliyokuwa iwakute Diego Costa na Pedro kutoka kwa hazard lakini pia Fellain na Pogba wao walifanikiwa kwanza kuuwa kazi ya mfanyakazi ya bora ng'olo kante kwanza.

Zouma, Cahill na Luiz Bado wanahitaji tuition kubwa sana kutoka kwa babu John Terry kwa asilimia kubwa...... Speed ni kitu ambacho limekuwa tatizo kwao ila timing nayo imekuwa shida kubwa kama united wangekuwa makini haswa Ashley Young nadhani wangeweza kupanua zaidi result bord...... Marco Alonso ni pigo katika kikosi cha Chelsea kutokana na mchango wake katika eneo husika(wing back)... Hiki ni kipindi ambacho majeruhi yanaigharimu timu katika matokeo mabaya kuliko kipindi kingine chote.

Diego costa unavyondelea kuusahau kazi yako basi usiwe unajikumbusha mshahara wako pia..... Kuna wakati unacheza kama Diego na kuna wakati unafanya kama Costa. Hiki ni kipindi HR anapenda kukuona ukishangilia sana kuliko kukuona ukilalamika zaidi mbele ya Mwamuzi.

Mpira huelekea sana kule unapopigwa sana ndio maana huu ukawa Msimu wa lawama.

Manchester united 2-0 Chelsea
Ahsante kwa uchambuzi mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom