Transcend
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 20,553
- 63,058
Asieee!Kwa kuongezea mkuu;
Wakati wa vita, David Msuguri Alikuwa na cheo cha Brigedia Jenerali. Yeye ndio alikuwa kiongozi wa majeshi ya Tanzania katika vita ile.
Makamanda muhimu wakati wa vita ya Kagera ambao waliongoza Brigedi mbalimbali ni kama;
Luteni Jenerali Silas Mayunga a.k.a Mti Mkavu
Luteni Jenerali Imran Kombe ambaye Alikuwa Mkuu wa Intelijensia Jeshini wakati wa vita.
Mapema tu baada ya vita akahamishiwa idara ya Usalama wa Taifa kabla ya kuja kuuwawa baadae kwa kuvujisha siri za nchi kwa Mrema.
Meja Jenerali Chacha Marwa " Kambale "
Huyu na kikosi chake walikutana na battle kali hali iliyomfanya wakimbilie mto Kagera ndani ya maji ili kujipanga upya na ndipo jina la Kambale lilipoibuka.
Meja Jenerali John Walden aka Black Mamba.
Wanasema huyu alikuwa ni chotara hivyo alikuwa kama Mzungu, Brigedi yake ilikuwa moto wakuotea mbali ambayo ilikuwa na vijana wenye morali kubwa sana.
Some memories to keep! Sasa hivi hakuna courage na weledi kwa kizazi kilichopewa vijiti..
Lakini pia vetting na namna ya kupata mashujaa kama hawa hakuna...
Kuna ukakasi uliingia kipindi cha miaka ya 2000 hadi sasa ...umeharibu sana vyombo vya usalama

