Makapuku Forum

1973 - Roberto Carlos anazaliwa.

Beki wa zamani wa kushoto wa Inter Milan, Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil.

Anatajwa kama beki bora wa kushoto kuwahi kutokea katika historia ya mpira wa miguu.

Alijulikana kama " The bullet man " kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga mashuti.

Anakumbukwa kwa freekick yake dhidi ya Ufaransa mwaka 1997 ambapo wengi walidhani mpira aliopiga unatoka nje lakini ghafla ulirudi ndani na kujaa wavuni.

Ametwaa Kombe la Dunia mwaka 2002 pamoja na Uefa Champions League akiwa na Real Madrid mwaka 2001.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…