Una uhakika kuwa Roma amechukuliwa na watawala? Siamini kama watawala ni wajinga kiasi cha kufanya jambo la kijinga namna hii kwa mtu ambaye wala siyo hatarishi katika jamii.
Siasa ni mchezo wa kucheza na akili za watu. Sitashangaa kama mambo haya yanafanywa na kikundi fulani cha watu ambacho wala hakifungamani na watawala ili kuigombanisha na watawaliwa. Binafsi sikufurahishwa jinsi suala la Ben Saanane lilivyoshughulikiwa na mabosi wake huko chamani. Yaani ilikuwa kama vile kondoo kapotea na siyo mtumishi mtiifu mwenhe cheo cha Mwenyekiti wa Sera na Utafiti wa chama.
Yote kwa yote hata kama watawala hawahusiki, hawawezi kukwepa lawama kwa sababu ni wajibu wao kulinda raia na mali zao. Na siamini kama kweli TISS na vyombo vingine vya dola wameshindwa kujua walipo watu hawa. Ndiyo maana ni haki watu kuamini kuwa pengine watawala wanahusika.
Na kinachonishangaza zaidi ni jinsi serikali hii isivyojali. Haina hata ile dhana muhimu ya "political capital" - kutumia matukio kujiimarisha kisiasa na kufahamu kuwa tukio dogo tu linaweza kuwa na madhara makubwa sana kisiasa. Inashangaza sana!