Makapuku Forum

Makapuku Forum

Siku zote huwa nasema; ili mtu afe sharti pawe na sababu aidha augue, apate ajali au vinginevyo.
Na ili utawala uanguke sharti pawepo na mambo ya kuchukiza raia, ni kama haya ya akina Roma nk
Una uhakika kuwa Roma amechukuliwa na watawala? Siamini kama watawala ni wajinga kiasi cha kufanya jambo la kijinga namna hii kwa mtu ambaye wala siyo hatarishi katika jamii.

Siasa ni mchezo wa kucheza na akili za watu. Sitashangaa kama mambo haya yanafanywa na kikundi fulani cha watu ambacho wala hakifungamani na watawala ili kuigombanisha na watawaliwa. Binafsi sikufurahishwa jinsi suala la Ben Saanane lilivyoshughulikiwa na mabosi wake huko chamani. Yaani ilikuwa kama vile kondoo kapotea na siyo mtumishi mtiifu mwenhe cheo cha Mwenyekiti wa Sera na Utafiti wa chama.

Yote kwa yote hata kama watawala hawahusiki, hawawezi kukwepa lawama kwa sababu ni wajibu wao kulinda raia na mali zao. Na siamini kama kweli TISS na vyombo vingine vya dola wameshindwa kujua walipo watu hawa. Ndiyo maana ni haki watu kuamini kuwa pengine watawala wanahusika.

Na kinachonishangaza zaidi ni jinsi serikali hii isivyojali. Haina hata ile dhana muhimu ya "political capital" - kutumia matukio kujiimarisha kisiasa na kufahamu kuwa tukio dogo tu linaweza kuwa na madhara makubwa sana kisiasa. Inashangaza sana!
 
Tatizo Polisi hawajielewi
*Hatuna taarifa za ROMA
*Zen tutahakikosha tunampata kabla ya J2
*Halafu eti kaparikana

Mbona hawasemi alikuwa wapi
Wanazingua
......
Unaelewa jinsi upelelezi unavyofanyika? Siyo rahisi kama unavyodhani unless kama huyo Roma walikuwa wanajua aliko.

Kuhusu kauli kutofautiana serikali hii haina coordination na ni kila mtu na lwake. Ndiyo maana unakuta waziri anasema hichi, Mkuu kabisa anasema hichi, Bashite naye akiibuka anasema hichi ali mradi vurugu tupu.
 
tatizo alilianza mzee wa kucheka kuminya demokrasia
Mzee wa kucheka ni mwanasiasa hodari sana lakini hatarishi mno! Naona yale matusi ya kuitwa Mr. dhaifu, Vasco da Gama, Mkwere, Mzee wa mipasho na mengineyo yalikuwa yanamwingia ndiyo maana jioni kabisa katika utawala wake akaamua kutunga na kutia sahihi hii sheria ya makosa ya mtandao tunayohangaika nayo. Halafu tena akageuza gia angani kuhusu mchakato wa katiba mpya baada ya kutumia mabilioni. Angekuwa legend kama angetuachia katiba mpya kwani hata matatizo mengi tunayohangaika nayo leo kisababishi kikubwa ni katiba mbovu inayompa rais madaraka makubwa mno ikiwemo kuteua wajumbe wa tume ya uchaguzi na mengineyo. Nimesema mara nyingi sana kwamba viongozi wetu masikini hata hawaangalii mbele na kuona jinsi watakavyokumbukwa na vizazi vijavyo. Wao wanaangalia maslahi yao na vyama vyao tu. Alipopima upepo na kuona kuwa pengine CCM wasingeshinda uchaguzi 2015 kama ungefanyika chini ya katiba mpya (tume huru ya uchaguzi bila Lubuva wala Jecha) basi akaamua kulitosa taifa ili kulinda chama chake. Na katika kufanya hivyo akapoteza nafasi nzuri sana ya kuwa mmojawapo wa viongozi bora kabisa tuliowahi kuwa nao. Inasikitisha sana!

By the way, hujambo Shunie? Nipo! Tupo!
 
umemdadavua vizuri mzee wa kucheka sijambo mm za ww musukuma kolomije wanasemaje
 
Nitakurudia, lakini endelea kuitafakari kauli hiii(tutampata Roma kabla ya jumapili by Makonda)
Una uhakika kuwa Roma amechukuliwa na watawala? Siamini kama watawala ni wajinga kiasi cha kufanya jambo la kijinga namna hii kwa mtu ambaye wala siyo hatarishi katika jamii.

Siasa ni mchezo wa kucheza na akili za watu. Sitashangaa kama mambo haya yanafanywa na kikundi fulani cha watu ambacho wala hakifungamani na watawala ili kuigombanisha na watawaliwa. Binafsi sikufurahishwa jinsi suala la Ben Saanane lilivyoshughulikiwa na mabosi wake huko chamani. Yaani ilikuwa kama vile kondoo kapotea na siyo mtumishi mtiifu mwenhe cheo cha Mwenyekiti wa Sera na Utafiti wa chama.

Yote kwa yote hata kama watawala hawahusiki, hawawezi kukwepa lawama kwa sababu ni wajibu wao kulinda raia na mali zao. Na siamini kama kweli TISS na vyombo vingine vya dola wameshindwa kujua walipo watu hawa. Ndiyo maana ni haki watu kuamini kuwa pengine watawala wanahusika.

Na kinachonishangaza zaidi ni jinsi serikali hii isivyojali. Haina hata ile dhana muhimu ya "political capital" - kutumia matukio kujiimarisha kisiasa na kufahamu kuwa tukio dogo tu linaweza kuwa na madhara makubwa sana kisiasa. Inashangaza sana!
 
Nitakurudia, lakini endelea kuitafakari kauli hiii(tutampata Roma kabla ya jumapili by Makonda)
Huyo jamaa kwangu hana credibility yo yote na naamini kuwa pengine ana matatizo ama ya kisaikolojia au zaidi ya hapo. Na katika hii serikali kuropoka ni kawaida. Kila mmoja anataka atoe mropoko wenye kuvuma zaidi ya mwingine. Na huyu kwa vile anajua kuwa hawezi kuguswa hata aropoke vipi basi kuropoka anaropoka kweli.

Kwa kutoa kauli hiyo ni wazi pengine alikuwa anajua Roma alipo. Wambane (kama kuna wa kumbana) aseme na Ben Saanane atapatikana lini. Hovyooooo!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom