Makapuku Forum

Makapuku Forum

tapatalk_1491132346071.jpeg
 
Mimi naomba kwanzia leo nichukue jukumu la "NUKUU YA LEO "


Itakuwa Segment ya kila siku ( siku za jumatatu mpaka jumamosi) asubuhi, kama nisipoweka asubuhi nitaweka jioni.


Naomba niitende haki hii..nitakuwa naweka kwa nukuu kwa lugha ya kiingereza na kiswahili..then nitadadavua kidogoo juu ya Nukuu..

Siku ambayo nitatingwa mtaniwia radhi wakuu..

All the best wakuu..
Asante ubarikiwe
 
Kuna kiyu kaongea bitozi kua kupost labda magazeti halaf watu hawampi sapoti hiyo inamvunja moyo mletaji. Nisiwe mnafiki mm ni mmoja wapo niliovunjika moyo ila kiasi chake lee anajitahidi kunipa spirit ya kuendelea kwa kuweka picha.
Pole sana mkuu ,ni vizuri useme nini kilikuvunja moyo mkuu ,kumbuka sisi ni binadamu hatujui mapungufu yetu nahitaji kutokukuvunja moyo,nini kinakuvunja moyo nisaidie nibadilike.
 
Bitoz na wadau wote wa Makapuku, heshima kwenu.

Kwanza, umeongea jambo zuri na la kufikirisha, yale mambo uliyotaja kuwepo kipindi hicho na kwa sasa yamekosekana yaweza kuwa sababu ya kuwepo kwa majukwaa mengine mahsusi kwayo, na ndiyo maana hakuna mdau anayejaribu kuweka kapuku songs japo za kubabia, lakini kwa mwongozo uliotoa basi hii segment inaweza kuwepo humu baada ya kuwa tumepata magazeti toka kwa lee empire na Shunie na historia ikiongozwa na Mussolin5 na bila kusahau kazi nzuri unayofanya Bitoz ya kunogesha historia kwa mapicha.

Kitu kinachoifanya Makapuku kuwa ya kipekee ni dhana nzima ya "acknowledgement" wataalamu wa maswala ya Utawala na Mahusiano wanasema ni muhimu kutambua mchango wa kila mmoja hata kama hukipendi na hii inatoa fursa ya kuelewana na kuelekezana, majukwaa mengine yamekosa hili isipokuwa hapa. kwingine ni kila mmoja kujidai anajua, anakaa Dar na ana gari, na kujiona bila 'yeye' jf au jukwaa fulani halip. Nimekuwa huku kitambo, nbajua naongea nini.
Kapuku forum ni 'da bomb'- 'Excellent, the best'
Thread kukosa mvuto, hii inaweza kuwa kweli au si kweli kutokana na nani anaitoa hoja hii, kwa mgeni huku anaona kapuku ndiyo forum iliyochangamka sana (bila kujali kinachochgangiwa na wadau-iwe ni story zisiszoisha, BS, na blah blah nyingi).

Well, bado kuna muda wa kuboresha kwa hoja chokonozi uliyoleta.
Heshima kwako na wadau wote. Usiku mwema.

Mondray mida ya swala usijesema nimekesha humu tena
Asante mkuu,nakuelewa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom