1981 - Rais Ronald Reagan wa Marekani anashambuliwa kwa risasi kifuani alipokuwa akitoka katika Hotel huko Jijini Washington D.C
Risasi hizo zilimpata kwenye mbavu na kusababisha damu kuvuja ndani kwa ndani. Kama sio kukimbizwa Hospitali ya karibu angepoteza Uhai wake.
Kutokana na tukio hilo, kumekuwa na utaratibu wa kutembea na damu ya akiba katika gari la Rais wa Marekani ili kujaribu kuokoa maisha ya Rais pindi inapohitajika.
Alishambuliwa na John Hinckley Jr ambaye alikuja kuachiwa baada ya kuonekana ana tatizo la akili.
Watu watatu walijeruhiwa ambao ni walinzi wawili na katibu wa Rais, James Brady ambaye alipooza mwili wote.
Miaka mingi baadae ilikuja kusemekana, Makamu wa Rais wa Marekani kipindi hiko, George H.W. Bush alikuwa nyuma ya Jaribio hilo la kumuua Rais ili yeye achukue madaraka, kwani Katiba ya Marekani inasema endapo Rais atafariki Makamu wa Rais ataapishwa kuwa Rais.
Pia Rais Reagan vita yake dhidi ya madawa ya kulevya ndio ilisababisha jaribio la kujaribu kumuua.
Ndio Rais wa mwisho wa Marekani kupigwa risasi akiwa Madarakani lakini hakufa.