Makapuku Forum

1963 - Ronald Koeman anazaliwa.

Beki wa zamani wa PSV, Ajax, Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi.

Pia amewahi kuwa kocha wa Ajax, PSV, Southampton na sasa Everton.

Moja kati ya mabeki bora wa kati wa muda wote, ambaye akiwa Barcelona aliifungia timu hiyo magoli 90 mengi yakiwa ni Freekick na penati.

Yeye ndio anaongoza kwa kufunga penati 46 kwa timu ya Barcelona katika La Liga mpaka sasa.

Pia anashika nafasi ya pili nyuma ya Leo Messi kwa kufunga goli nyingi za Freekick pale Barcelona.

Alitwaa ubingwa wa Euro mwaka 1988 akiwa na Uholanzi chini ya staa Marco Van Basten.

Kwasasa anapigiwa chapuo kwenda kurithi mikoba ya kocja wa sasa wa Barcelona, Luis Enrique.
 
1980 - Ronaldinho Gaucho anazaliwa.

Jina lake halisi ni Ronaldo De Assis Moreira.

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa PSG, Ac Milan, Barcelona na timu ya taifa ya Brazil.

Anatajwa kama mmoja wa wachezaji bora wa wakati wote kuwahi kutokea katika ulimwengu wa soka.

Ameshinda kila kitu katika soka, Kuanzia Copa America mwaka 1999, Kombe la Dunia mwaka 2002, Uefa Champions League mwaka 2006, ubingwa wa La Liga mara mbili.

Pia ameshinda Ballon D'or mara mbili.

Alisifika kwa chenga zake za madaha, uwezo wa kukokota mpra na hata magoli adimu.

Mpinzani wake mkuu wakati anacheza alikuwa Zinedine Zidane wa Ufaransa, mpaka leo hakuna jibu sahihi kati ya Zidane na Ronaldinho nani alikuwa zaidi?
 

Kumbe wachezaji wengi Wa Kijerumani wanaisikia Ballon d'or kwenye bomba nahisi kutokana tu na soka la shoka walilokuwa wanacheza
....
 

Alikuwa jembe
....
 
- World Poetry day.

Siku ya kimataifa ya Ushairi Duniani.

Katika siku hii, Watu wanahimizwa kusoma Mashairi mbalimbali kwani imejengeka dhana kwamba mashairi ni magumu sana.

Baadhi ya Washairi wetu toka Tanzania ni Kaluta Amri Abeid, Shaaban Robert, Euphrase Kezilahabi.
 

Nakumbuka goli lake v Chelsea
...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…