Makapuku Forum

 
*CAMERAMAN WA ENZI HIZO....*


Makamera man walikuwa majeuri
kishenzi yaani! Kwanza unakuta hii
Kamera ina likamba fulani jeusi
inaning'inizwa shingoni.....
Kameraman ana kabaskeli kake hapa...
nyuma kana begi lina picha za watu ambao hawajamaliza madeni.
Kamera man anakupiga picha leo
anakwambia picha yako utaipata panapo
majaaliwa mkanda ukijaa... unaweza
kusubiri miezi miwili...
Enzi hizo kamera man ndiye anayekupangia pozi gani ukae ili upigwe....
Kamera man anampanga hadi baba yako
mzazi kwenye picha hahahahah! Baba
anakuwa mpoleeee! Kamera man anapita na kabaskeli kake
watu wanamuita anaringa huyoooo!....
ukute msimu wa sikukuu mnaweka oda
kwa kameraman wiki mbili kabla....... akija
anaanza kwanza kula pilau na soda yake
ipo amehifadhiwa.... baada ya hapo ndo anapiga picha......
Enzi hizo picha inatoka umefumba
macho, na unailipia... sio siku hizi mtu
anapiga picha mia anachagua moja ndo
anaipost mtandaoni......
*Enzi hizo sisi watoto* *tukililia picha tunapigwa* *flash kilio kinaisha*
*hapohapo.......*
 
Sana mama mchungaji!
Unakumbuka Amri kuu Yesu aliyowapa wanafuzi wake eeh?
1wakorintho 13:1 Hata kama nikinena lugha za watu na hata za malaika,lakini kama sina Upendo Mimi nimekuwa tu kama sauti ya debe tupu au kengele 2 Tena ,naweza kuwa na kipaji cha kutangaza ujumbe Wa Mungu,nikafahamu siri zote na kujua kila kitu;naweza kuwa na imani yote hata nikaweza kuihamisha milima,lakini kama sina Upendo Mimi si kitu 3 Nikitoa Mali yangu yote na kuwapa maskini,na tena nikiutoa mwili wangu uchomwe,kama sina Upendo hiyo hainifai chochote 4. Mwenye Upendo huvumulia,hufadhili,mwenye Upendo hana wivu,hajidai wala hajivuni. 5Mwenye Upendo hakosi adabu ,hatafuti faida yake binafsi wala hana wepesi Wa hasira haweki kumbukumbu ya mabaya 6 hafurahii uovu,Bali hufurahia ukweli 7 mwenye Upendo huvumulia yote huamini yote na hu stahimili yote. 8. Upendo hauna kikomo kamwe....

Lililo kuu ni UPENDO
 
 
Mbarikiwe sana mahali hapa asante Mussolin5 kwa historia asante Bitoz kwa picha Nyagei Lee Numbisa Transcend Van? Herera21 Clkey Werrason na. wooote Mungu awabariki muwe na siku njema yenye Upendo na furaha wapi Shunie Mondray ?Mbarikiwe
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…