Makapuku Forum

Makapuku Forum

Shunie , siku za ijumaa kuelewa huwa ni ngumu sana, ndo maana hata kazini tunakaaga nusu siku, masaa manne tu mnaaga kwenda kupumzisha akili (kivyovyote, kwa kusali , kuburudika kwenye wauzapo bar, ila bakulutu lazima) subiri weekend iishe utaelewa tu
Bhinamuu mbona umenipac haufiki ?? Nshaagiza na suruali niliyovaa imetoboka Bhinamuu
 
Simba SC vs Yanga SC....


KAPUKU twende sawa....

Kotei, Mkude na Zulu, kamusoko...... Hapa ndio Derby ya kariakoo inaanzia.... Katika muundo wa eneo la katikati mwa uwanja na katikati kwa kila timu kuna Kotei na Zulu katika kuokota mipira katika eneo lao na kuwahakikishia usalama golini kwao...... Kamusoko na Mkude wanafahamika katika kupokea mipira iliyookotwa na wale viungo wa chini ili kuisambaza katika matawi mengine yanayosubiria kazi yao.

Muundo wa pairs za kamusoko, Zulu pia mkude na Kotei hapana shaka wanaufanano wa karibu sana katika kazi zao ndani ya kiwanja...... Flow ya timu hususani katika eneo la kiungo inaanzia kutengenezwa na kiungo anayecheza mbele ya Kamusoko, Zulu, Mkude na Kotei...... Haruna Niyonzima na Mohamed Ibrahim "Mo" hawa ndio wenye ladha ya timu na mchezo kiujumla..... Aina ya uchezaji wa viungo hawa ukwaju wa kushambulia unatofautiana sana japo kuna wakati hucheza katika nafasi zinazolandana...... Hapa ndipo Mo huifanya flow ya timu kuonekana kwa ule ubunifu wake wa kutembeza pamoja na kutembea na mpira mpaka katika final third ya opponent, na aina hiyo ya uchezaji wake mara kadha wa kadha amekuwa akijikuta katika nafasi ya kufunga.....

Aina ya uchezaji wa Haruna Niyonzima huongeza ladha maridhawa katika mpira haswa wakati anataka timu isogee mbele kupitia mguu wake, kuna wakati ana endesha timu kwenda mbele ila kuna wakati timu inaendeshwa na pasi zake ndefu kwenda mbele..... Flow ya kiungo cha Yanga inaanzia miguuni kwa haruna baada ya kazi nyingi za Kamusoko na Zulu.....

Kama Yanga wanavyomkosa Ndemla wao katika benchi, basi vivyo hivyo na Simba nao wanamkosa Makapu wao katika benchi..... Ndemla ni miongoni mwa wachezaji bora wanaoisafisha mipira katika eneo la kiungo, kumkosa mtu wa aina hii kama option katika benchi ni kukosa fleva murua sana na mbadala mzuri wa Haruna Niyonzima pale kwenye mipira ya ukwaju. Ila pia Said Juma Makapu ni miongoni mwa viungo bora Wazawa wanaosifika kwa kuichafua mipira katika eneo la kiungo, kumkosa mwanadamu wa aina hii katika benchi kama mbadala mzuri wa James Kotei ni kukosa ladha mbadala katika kiungo cha chini kabisa.

Achana na miguu ya Juma Abdul, Haji Mwinyi pia Besela Bakungu na Mohamed Hussein...... Ubora wa mipango wa Ibrahim Ajibu na Saimon Msuva katika zile bampa tu bampa za kukimbia na mipira inaweza kuwalaza na viatu mabeki wa pembeni katika mchezo huu.

Acha tuisubiri Darby hii maana Mavugo na Tambwe wanaweza kutufundisha kitu katika akili za Banda na Yondani........

Tuende kwenye mchezo tukisahau mkono wa Tambwe na Kona ya kichuya maana tutarudi na mambo mapya.....

Kama hautaki usumbufu saa sita uwe ndani ya Mchina pale maana sisi tunakuja saa tano pale.

Nachosubiri ni kumuona refa wa Manara Haji

Tukutane baada ya mechi...
0c3be3f44e342848db222fa6ccf44d57.jpg
Shafii Dauda bhana!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom