Makapuku Forum

Leo katika Historia:

1990 - Makubaliano ya Kuziunganisha Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi yanafanywa ili Kuirudisha Ujerumani moja.

Hii ni baada ya Nchi hizo mbili kutengana muda mfupi baada ya kumalizika kwa Vita kuu ya pili ya Dunia mwaka 1945 hali iliyopelekea Kujengwa kwa Ukuta mashuhuri wa Berlin ulioziyenganisha nchi hizo.
 
1933 - Paul Biya anazaliwa.

Ni Rais wa pili wa Cameroon ambaye ndiye aliyepo Madarakani sasa.

Ameshika Madaraka ya Urais kuanzia mwaka 1982 mpaka sasa amabapo ni sawa na miaka 35 akiwa madarakani.

Ni moja kati ya Marais wa Afrika waliokaa sana Madarakani na anayetawala Kidikteta kwa Mkono wa Chuma kando ya Museveni na Robert Mugabe.
 
1960 - Pierluigi Collina anazaliwa.

Refarii wa zamani kutoka nchini Italia aliyekuwa pia mwamuzi wa kimataifa aliyetambulika na FIFA.

Alijipatia Umaarufu kutokana na style yake ya kunyoa Kipara muda wote na macho makali yenye umakini awapo uwanjani.

Anatajwa kama Refarii bora wa wakati wote katika mchezo wa soka.
 
Yeah, Collina alikuwa bonge la refa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…